.
Kuna muda wale wanaosema tunapenda mara moja tu najaribu kukubaliana nao, haiwezekani baada ya miaka 20 kupita bado ananijia mpaka ndotoni, siku haipiti bila kumuwaza!
Ni hivi huyu mtu tumefahamiana kipindi hicho shule ya msingi,alihamia shule yetu akiwa std 6,kwao walikuwa na maisha standard tu maana baba yake alikuwa DC na mimi nilikuwa hoehae tu ambaye tayari nilishapoteza wazazi wote wawili.
Pengine ni uwezo wangu mkubwa darasani ndo ulifanya tukawa karibu sana,hakuna ambaye hakujua ukaribu wetu shule nzima, ila ndo hivyo mapenzi ya kitoto hakuna chochote cha maana kilichoendelea. Lakini tu niseme ni best feeling ambayo sijawahi kupitia tena popote. Tulifaulu std 7 kwenda shule moja, baada ya miezi kadhaa yeye alihama na kwenda shule ya girls, baada ya hapo sikuona tena ule umaana wa kubako hiyo shule, na mimi niliforce nikahama,tuliendelea kuwasiliana kwa barua tu, na kipindi chote hicho sikuwahi mtongoza japo maneno yalikuwa mengi sana kwamba sisi ni wapenzi!
Nakumbuka mwaka 2003/2004,nilifanya jitihada tulionana na ndipo nilipoamua kumueleza hisia zangu,kifupi alinikataa kwamba hatuwezi kuwa pamoja, na kikubwa dini itanisumbua (yeye alikuwa muislamu),na alisisitiza zaidi kwamba kuna watu walioa na wakafiwa na wake zao, ila maisha yakaendelea sembuse yeye!Kifupi siku na namna nilikubaliana na maamuzi yake. Ila kinachoniuma baada ya pale mawasiliano yaliyumba sana.
Bahati mbaya zaidi alienda advance mkoa wa mbali kabisa kabisa tofauti na mimi, ikafika kipindi mawasiliano yakakata kabisa.kila nilipojitahidi kurudisha ukaribu nilikwama kabisa maana yeye hakuwa na huo muda. Niliwaza sana, kwamba huyu mtu sawa hanitaki lakini hata ule urafiki tu ina maana miaka yote ulikuwa ni uongo?Kwanini mtu apotee mazima hivyo kana kwamba hajawahi kuexist kabisa kwenye maisha yangu? Yaan hapa ndo nilianza kuijua vizuri dunia!
Mbaya zaidi kilichokuwa kinanitesa, kila mtu anayenijua tukiwasiliama basi ataniuliza huyo mtu yuko wapi,ili mradi tu tafrani! Ilifika muda mpka magroup ya primary na sekondary nikaleft, hata wale rafiki zake ambao kila nikiingia fb lazima niwaone ikabidi niwahide na kuwamute. Hii yote haijanisaidia,kila siku bado anazurula akilini mwangu.
Kuna muda hii dhana ya kumove on hata siielewi,maana sio kwamba alikuwa mzuri sana hapana, tena hata tabia sikuijua lakini kwanini aendelee kunitesa hivi? Mbaya zaidi yeye ana maisha yake huko pengine hata hawazi kama amewahi kukutana na mimi maishani!Kuna muda najifariji pengine tu hakuwa wangu kwakuwa tulikuwa umri sawa, lakini nikienda kwenye uhalisia mbona watu wanaoa mpka watu waliowazidi umri.
NB;Nimewahi mpigia mara moja miaka kama 8 nyuma, tulipiga story fresh ila baada ya hapo ikawa imeisha.Bado natafuta mbadala wa huyu mtu, japo naona zoezi linaelekea kunishinda.