Miaka 20 ya JF: JamiiForums irudishe heshima yake ya Jukwaa La Great Thinkers

Gift mzalendo

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2019
Posts
4,675
Reaction score
6,428
Huwezi kuwa greater thinker alafu uwe mnafiki na mtu wa kupindisha pindisha maneno

wajinga waitwe wajinga , wapumbavu waitwe wapumbavu kulingana na sifa zao

Kwa wale wenye sifa za wanyama wachafu waitwe kulingana na sifa zao Wala sio matusi

Hili jukwaa lilianzishwa Kwa ajili ya Great thinker

Sifa mojawapo ya Great thinker ni KUCHUNGUZA na kuujua ukweli

Akishajua ukweli ANASIMAMA na ukweli bila kujali ni unamuhusu yeye binafsi yake jamii yake viongozi au chama chake

Kwa lugha nyingine hili jukwaa haswa hili la siasa lilianzishwa Kwa ajili ya WAZALENDO wanaopenda nchi na taifa lao kuliko wao vyama vyao siasa

Maanake maslahi ya Taifa na nchi ndo kipaumbele Chao kuliko vyama na viongozi wao

Miaka 20 ya Jf irudishe heshima ya jukwaa la Great thinker
 
Hii ni biashara mkuu, biashara watu,ukiona hapakufai achana napo,binafsi kwa wiki naweza ingia mara mbili,naona kabisa baada ya miezi sita ntakua nimeachana na jf
 
Wewe ndio unataka usikilizwe, wengine tuwe wasomaji?
 
Griti sinka🤣
 
Kiongozi hii itakuwa ni monopolization and it will be against freedom of speech that thing you preach always

Acha watu waandike mambo yao.Kama kweli wapo hao GT kitakuwa kipimo sahihi kwao.Hao ma-GT watakuwa na uwezo wa kubaini vitu vya hovyo na kutoa vitu safi.

Unadhani wakibaki GT peke yao pumba na mchele tutatofautisha vipi sisi walaji?
 
Ujinga ni pale great thinker wa jf anapimwa kwa kuipinga serikali,
Hili umeliona limeandikwa wapi na nani aliyeelekeza hivyo?
eti mzalendo ni yule anaeipiga serikali, eti ili uwe msomi lazima uipinge serikali kwa kila kitu.
Kuna sehemu yoyote ndani ya JF panapoagizwa haya unayosema wewe. Umeyatowa wapi haya?

Kwa maana yako, kutetea uovu unaofanywa na viongozi wa serikali, ndio uzalendo?
Huna akili za kufahamu matendo yanayowanufaisha waTanzania na yale yanayowakandamiza?

Kwa maana yako ya kuwa mzalendo ni kuunga mkono kila kinachofanywa na serikali, hata kama kinawaumiza waTanzania?
Hakuna atakayekupangia, lakini utaambiwa kuwa wewe ni mpumbavu, na utauelewa upumbavu wako huo, hata kama hutakiri kuwa wewe ni mpumbavu.
 
Ndani ya JF burudani inapatikana popote tu.
Tatizo linaanzia hapa katika mambo mengi tunayoyafanya kama waTanzania. Tunapoghairi kufanya mambo yetu kwa taratibu zinazoeleweka.
Kwa hiyo kwako unajiburudisha tu kila mahali; kama yule mtu wa kijijini anayekwenda porini "kuchuma dawa"!

Tusipoondokana na fikra za aina hii hattutafika popote.
 
Kwanza elewa maana ya neno 'burudani'.

Ndani ya JF yote burudani inapatikana, haijalishi ni jukwaa gani.

Mimi sijiburudishi tu kila mahali, bali naburudika pale burudani inakopatikana.

Hutanuelewa kama hujaelewa maana ya 'burudani'.
 
Mimi sijiburudishi tu kila mahali, bali naburudika pale burudani inakopatikana.

Hutanuelewa kama hujaelewa maana ya 'burudani'
Sasa huoni kuwa kama hutaki nielewe maana yako ya " burudani" ni nini sitaweza kuelewa?

Kama maana yako ya "burudani" ni kuja kumsoma na kufurahia kila anachoandika 'Tlaatlaah' humu, sema kuwa hiyo ndiyo burudani yako na tutaelewa hivyo; pamoja na kwamba binafsi siioni hiyo kuwa burudani katika jukwaa hili la siasa ihusuyo maslahi ya taifa letu.
 
Sijasema kila ninachokisoma kinaniburudisha katika jukwaa la siasa. Hata hivyo burudani hutofautiana kati ya mtu na mtu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…