SoC02 Miaka 25 – 30 na afya ya akili ya kijana

Stories of Change - 2022 Competition

Chambou255

Member
Joined
Feb 15, 2019
Posts
16
Reaction score
19
Mwaka ni 2012, kijana Hope amemaliza kidato cha nne akisubiria matokeo ya kwenda A level. Kwenye kichwa chake unacheza mkanda wa namna Maisha yake yote yaliyobaki jinsi yatakavyokuwa. Ameshafika miaka 25 anajiona amemaliza chuo, ana kazi nzuri, ana gari na tayari ameshaoa.

Asichokijua Hope ni kwamba Maisha sio mstaari ulIonyooka, Maisha hayaendi kama tunavyopanga na kuna mengi yanayoweza kutokea yakasitisha mipango ambayo tunayo. Hope yeye halifahamu hili, ni kijana mdogo tu ambaye bado hajayajua Maisha.

Ni miaka kadhaa imeshapita na Hope amekuwa kijana wa makamo sasa, ameshamaliza chuo kikuu cha Dar es Salaam akichukua shahada yake ya kwanza akiwa na miaka takribani 23 akikaa kwa wazazi wake, anaanza kuomba kujitolea, kutafuta kazi.

Mwaka wa kwanza unakatika, mwaka wa pili nao unakatika Hope bado yupo mtaani anaomba kazi lakini hata ile kujibiwa email tu kwamba kakosa kazi hajibiwi. Kumbuka Hope ndiye mtoto wa kiume nyumbani kwao na ni wa kwanza akiwa na wadogo zake Watatu.

Vijana wengi watakaosoma hili andiko watauelewa mtihani ambao amepitia Hope, kuna kina Hope wengi mitaani, vijana wa miaka 23 -28 ambao wamemaliza masomo yao ya chuo ila hamna dalili yote ya kupata kazi, wapo nyumbani hawana.

Nakumbuka mimi na marafiki zangu tulikuwa na jina tunaitana la ‘Tarmac warriors’ tukimaanisha shujaa wa lami, kwamba sisi kila siku ni tunatembea kwenye maofisi ya watu na CVs zetu mikononi.

Wakati huohuo, kuna kijana mwingine umri kama wako, utakuta mumesoma wote au mumekua wote lakini kimaisha tayari amekuacha mbali. Utakuta ameoa, ana kazi ya kueleweka, yaani kwa ufupi Maisha yake yana muelekeo.

Sasa hapo mwenzangu na mie kila ukijaribu kutuma CV kwa ajili ya kazi, wapi hola, hata kujibiwa hujibiwi. Wale wajomba waliokuambia ukimaliza chuo uwatumie CV na cheti kwa matumaini ya kazi hawaonekani, Ndugu na marafiki wengine wanaona kila ukiwatafuta basi sijui unataka kuwaomba kitu na kila ukiingia mitandaoni unaona tu agemates zako wanavyokula Maisha.

Mbaya zaidi wewe ni mtoto wa kiume, una miaka 23 na kuendelea, huna mchakato wowote wa kukuingizia hela, umekaa ndani unasubiri ugali wa kengele. Kama ukiwa unaagizwa nyumbani unaoweza kuona unadharauliwa (inaweza kuwa kweli) kwa sababu huna kazi.

Uzuri iwe kwenu mnajiweza kwa uwezo wa maisha, lakini tofauti na hapo utajihisi tu unaongeza mzigo nyumbani. Ikiwa sasa unatokea familia ya kimasikini, una wadogo zako kibao wanakuangalia, wengine wanasoma na wanasomeshwa na wazazi, kula na kulala yao ni nyumbani. Na wewe sasa umeenda kubanana na wadogo zako hapo hapo, hakuna unachochangia, sio maji umeme sio maji, hata chumvi ya 200 huchangii.

Kibaya zaidi kuna wale Ndugu na jamaa zetu ambao ukiwa kwenye majaribu hayo ni kejeli tu muda wote, wengine wanazionesha hata waziwazi. Kibaya zaidi wengine wanaonesha hizo kadhia wazi wazi, yaani unaweza kujiuliza kwani huyu mtu nimemkosea nini, la kufanya huna, ukiongea utaonekana Maisha yashankufanya uwe chizi!.

Kwa kipindi hiki ambacho nimekielezea hapo afya yako ya akili itapata changamoto kubwa, usipoangalia unaweza kukufuru mungu na kujiuliza hivi kwa nini mimi mungu, uwe na kifua kweli.

Ninayekuambia haya fahamu kwamba sio naongea tu bali kila nilichokiandika hapa ni kitu binafsi nimekipitia ama nimeona mtu wangu wa karibu amepitia. Na pengine kwa sasa sipo ambapo nataka niwepo lakini sipo ambapo nilipokuwa.

Nachoweza kukuacha nacho kijana mwenzangu ni kwamba usikate tamaa,kwa sababu hakuna njia nyingine kwenda mbele, hakuna njia Mbadala. Njia ya kutoka ulipo ni kuhakikisha unaendelea kutafuta kazi, unaendelea kutafuta fursa. Na wakati unaendelea kutafuta fursa endelea kujiongezea thamani kwenye kitu unachokifanya.

Kama una kipaji tafuta namna ya kukiendeleza, jaribu kukuza mtandao wa marafiki zako, hii itakusaidia kupata mawazo mapya na pengine hata ikawa sababu ya wewe kukwamuka. Na kuhusu marafiki, ukiona una marafiki ambao nyie mkikaa ni soga tu kila dakika, achana nao! Wanakukwamisha kwa kiasi kikubwa na wewe ndio umewakumbatia. Sikatai kwamba marafaiki hawapigi soga ila ukiona yeye muda wote ni anachukukumbuka wewe ni kwenye mambo ya starehe, kuongelea mipira, movie mpya ipi imetoka, jua ana wadau wake wanaojadili maendeleo ila wewe ni rafiki wa bata.

Kingine, jitahidi usiiwekeze furaha yako mitandaoni utapata tabu sana. Kila ukiingia Instagram ni jamaa zako ambao umesoma nao wanakula Maisha mpaka unajiuliza unafeli wapi. Mwenyewe nilikuwa muathirika wwa hili mpaka nilipokuja kujua kwamba Maisha ya mtandaoni na Maisha halisi ni vitu viiwili tofauti.

mitandao inakupa viwango visivyo halisi ambavyo unaoweza kuhisi inabidi uendane navyo, lakini sio kweli kwa sababu wale wote wanaopost na kuvimba mitandaoni , kiuhalisia hali ni tete, unaoweza kujihisi unakwama kumbe mumekwama wote, ni kutishana tu.

Ila yote kwa yote, hayo yote hayotafaa kama hutamtanguliza mungu mbele, kwa imani yako, muombe mungu wako. Mimi nashuhudia mungu yupo, nimeshuhudia mungu akifanya miujiza kwenye Maisha yangu kwenye sehemu ambazo ni kiza.

Hii ni kwa sababu kuna muda hakuna kitu kingine kitakachoiokoa akili na nafsi yako zaidi ya imani yako kwa mola wako, kuna muda imani ya kwamba kuna aliye juu na ana mipango bora zaidi ya uliyonayo ndio kitu pekee kitakachonusu afya ya akili yako.

Rai yangu kwa kwa vijana wote ni kwamba ndio ni kweli huoni njia ya kwenda mbele, hakuna mwanga na hakuna mwisho na haujui hupo wapi. Nakuelewa kwamba ni jambo ambalo linakatisha tamaa na kukufanya hata kufanya afya yako ya akili kuwa rehani. Nakwambia hali hiyo haitokaa milele, utatoka ulipo, kumbuka kiza kikiwa kinene ndio alfajiri inakaribia.
 
Upvote 6

Very impressive
 
Ujumbe mzuri
 
Back
Top Bottom