Tamasha la miaka 30 ya Bongo Fleva liliyofanyika usiku wa kuamkia Julai 11 yalikuwa ya shangwe, burudani na kumbukumbu za safari ya muziki huo. Hata hivyo, tukio lililovuta hisia za wengi halikuwa muziki pekee, bali mwitikio wa watazamaji kwa baadhi ya wasanii waliojaribu kuzungumzia siasa jukwaani. Miongoni mwa waliokumbana na kuzomewa ni MwanaFA, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, pamoja na Stara Thomas na Dully Sykes.
Pia soma MwanaFA azomewa na wananchi baada ya kutaka kusifia Awamu ya 6 kwenye Tamasha la miaka 30 ya Bongo Fleva
Tukio hilo limezua mjadala mpana kuhusu uhusiano kati ya burudani na siasa. Kwa upande mmoja, linaweza kutafsiriwa kuwa sehemu ya wananchi wanataka majukwaa ya burudani yabaki kwa ajili ya sanaa na muziki, bila kuingiliwa na mijadala ya kisiasa. Kwa upande mwingine, baadhi ya wachambuzi na wananchi wanaona kuwa mwitikio huo unaweza kuakisi uchovu au kutoridhishwa na ujumbe wa kisiasa unaotolewa katika matukio ya kijamii.
View attachment 3626829
Tafsiri hiyo imepewa uzito zaidi na ukweli kwamba katika miaka ya karibuni serikali ya awamu ya sita imekuwa ikikosolewa na baadhi ya vyama vya upinzani, asasi za kiraia na watetezi wa haki za binadamu kuhusu madai ya utekaji na kupotea kwa watu, matukio ya mauaji, kupanda kwa gharama za maisha, tuhuma za ufisadi, pamoja na kile wanachodai kuwa ni kubanwa kwa shughuli za vyama vya upinzani na uhuru wa kisiasa.
Kwa muktadha huo, kuzomewa kwa wasanii waliojaribu kuzungumzia siasa ni tafsiri kwamba majukwaa ya burudani yanapaswa kubaki kuwa sehemu ya kuunganisha Watanzania, badala ya kuwa uwanja wa mijadala ya kisiasa inayoweza kugawa wananchi kwa misingi ya itikadi.
Burudani hukutanisha watu wa mitazamo, dini, makabila na vyama tofauti, hivyo wengi huamini kuwa jukwaa hilo linapaswa kutumika kuleta umoja, furaha na mshikamano. Miaka 30 ya Bongo Fleva haikutakiwa kuwa jukwaa la ujumbe wa kisiasa, hasa katika kipindi ambacho kuna mijadala na maoni yanayokinzana kuhusu utendaji wa serikali na hali ya kisiasa nchini.
AIBU MTAONA NINYI SERIKALI