African Believer
JF-Expert Member
- Jul 30, 2015
- 436
- 426
Leo January 12, 2022 ni sikukuu ya kitaifa ijulikanayo kama Mapinduzi ya Zanzinar ikiwa ni miaka 58 toka mapinduzi hayo yafanyike January 12, 1964 ili kuuondoa utawala wa Kisultan uliokuwa chini ya waarabu kutoka Oman.
Ikiwa imepita miongo mitano toka mapinduzi hayo yafanyike bado kumekuwa ni sintofahamu nyingi kuhusiana na namna mapinduzi hayo yalivyopangwa na kutekelezwa pamoja na matokeo yake hivyo kuacha maswali mbalimbali.
Swali kuu, ni nani alikiwa kiongozi wa mapinduzi yale? Je, anapewa heshima anayostahili kulingana na kili alichokifanya, kama kinahesabika kama mchango chanya, au je anapata lawama za kutosha kama kinahesabika kama mchango hasi?
Je, katika mapinduzi yale kuna watu walikufa? Na je walikuwa kina nani, na kwa nini vitabu vingi vya upande unaounga mkono mapinduzi havilisemi hili kwa uwazi?
Je, kuna raiya waliokimbilia uhamishoni mara baada ya mapinduzi yale, na kama wapo, jitihada za kuwarejesha nyumbani zilishafanyika?
Ni upi ulikuwa mchango wa John Okello?

Je, Umefika wakati wa kuzungumza waziwazi juu ya kile kilichotokea Zanzibar miaka 58 iliyopita?
Au, kombe lilishafunikwa na mwanaharamu alishapita?
Ni hayo tu wanajamvi.
Niwatakie heri ya sikukuu ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar!