SoC04 Miaka 5 /10 ijayo tunataka kuona mitaala ya elimu ya juu kusukwe upya ili imwezeshe mhitimu kuwa na ujuzi unaomwezesha kujiajiri/kujiajiri

SoC04 Miaka 5 /10 ijayo tunataka kuona mitaala ya elimu ya juu kusukwe upya ili imwezeshe mhitimu kuwa na ujuzi unaomwezesha kujiajiri/kujiajiri

Tanzania Tuitakayo competition threads

Simba Mwema

Member
Joined
Dec 5, 2023
Posts
38
Reaction score
71
Elimu ni nyenzo muhimu saana kwa mwanadam kupambana na mazingara yanamzunguka. Ikiwa elimu hiyo haimwezeshi kupambana na mazingira hiyo elimu inakuwa kiwazo kwake hivyo humpatia mazingira magumu saana.

Zamani mababu na mabibi zetu waliweza kufundisha vijana kwa kuwapatie elimu kwa vitenda ili kuweza kumuda kuifanya kazi hiyo. Mfano kijana wa kiume walifunzwa kuchongo/kutengeneza mipini ya jembe, shoka, hengo n.k kufunzowa kushona nguo, kutengeneza Kamba za kienyeji, vigoda, vitanda, huku wasichana wakifunzwa kupika, kufua, na kazi nyinginezo. Hizi zote zimwezesha kijana kuwa na ujuzi na wa kufanya kazi husika.

Elimu ya zama za mababu zetu ilkuwa inalenga kufundishwa majukumu ya kila siku na mifumo wa jumuiya zetu (daily routines and community systems)

Mfumo wa elimu ilikuja kuharibiwa wakati wa ukoloni, kwa walileta mitaala ya elimu tofauti na ya tamaduni zetu na kwa kuwa malengo yao yalikuwa tofauti basi jamii ikajikuta ikabdili mfumo wa mafunzo hivyo kuathiri mfumo mzima wa elimu

Tanzania kama ilivyo nchi nyingi za Kiafrika baada ya uhuru tulifuata elimu ya kikoloni ambapo kwa nyakati hizi za mabadliko makubwa ya teknoljia haitusaidii saana.

Nasema haitusaidii kwa sababu kuna wimbi kubwa la wahitimu wengi wa vyuo vikuu nchini wakishwindwa kushindana katika soko la ajira kutokana na kukosa kukosa ujuzi na maarifa kwa mahitiji ya kazi husika.

Hii ni kutokana na mitaala yetu tulioirithi kutoka elimu ya kikoloni kuwa hailengi kufundisha mwanafunzi kuwa na ujuzi wa kufanya jukumu Fulani katika fani aliosemea.

Mitaala ya elimu ya vyuo vikuu imejaa nadharia saana kiasi kwamba zao linalotakana na mitaala ya fani husika.

Hii inafanya wahitumi wengi kushindwa kuajirika au kujiajiri kutokana kukosa ujuzi. Kwa miaka ya hivi karibuni tumeshudia waajiri wengi kulalamika kuwa wanafunzi wengi kukosa sifa na vigezo vya kuajirika kwa hawana ujuzi

Haya ni matokeo ya kuendelea kukumbatia miitala ya elimu ya kikoloni iliharibu mfumo wa elimu wa Tanzania wakati na baada ya uhuru

Tukifanya yafuatayo kwa miaka 5-10 ijayo tutapata wahitumu wanaoweza kuajirika/kujiajiri
  • Kufumua mitaala ya vyuo vikuu na kuisuka upya, kama nilivyosema hapo awali kuwa mitaala yetu urithi toka kwa ukoloni, haipaswi kuendelea kutumika, Wizara ya Elimu kupitia Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inapaswa kuandaa mitaala yenye kulenga elimu ya kutenda zaidi kuliko nadharia. Inaweza kushirikiana na mamlaka zingine za vyuo vya ufundi kama vile Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Stadi (VETA) na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) kufanikishwa jambo hilo. Mamlakazi hutoa mafunzo ya elimu ya ufundi nay a kati ambapo wahitimu wake ni tafauti saana na wahitimu wa vyuo vikuu. Kama ili vyuo vya ufundi kwenye sera ya elimu wakati wa Azimio la Arusha mwaka 1967 likilenga kujitegemea kuwa kuzalisha nguvu kazi yenye ujuzi, na ni kweli vyuo vingi ya elimu ya ufundi viliweza kuzalisha wahitimu wanaoweza kutegemewa na kujitemea. Hivyo tunaweza kuiga mfumo huu pia ili kuzalisha wahitimu wanaoweza kutegemea na pia kutegemewa na taifa.
  • Vyuo vya elimu ya Juu viwe na miundombinun toshelezi ya kujufunzia na kufundhishia, uanzishwaji wa vyuo vya elimu na matawi yake uwe na miundo mbinu ya kujifunza na kufundishia, vifaa vya kufanyia majaribio na mazozi, baabara, karakana, maktaba, n,k viwe na vifaa vya kutosha kuendana na idadi ya wanafunzi ili kila moja anufaike na vifaa kwa kuvitumia ili kuwa na ujuzi stahiki. Kuwa na miundombinu mibovu, kuchaa kwa madarasa, na ukosefu wa vifaa vya kufundisha na kujifunzia kunaathiri utoaji wa maarifa na ujuzi.
  • Kuwa na wakufunzi/wahadhiri wenye ujuzi, Moja kati ya kanuni ya TCU katika kuajiri mwalimu anapaswa kuwa na GPA ya 3.5 na kuendela. Kipimo cha kanuni hii ni namba kubwa ya ufaulu, tunapaswa kuwa na wahadhiri wenye ujuzi na uzoefu mkubwa kufundisha unaoleta matokeo chanya, unakuta mhadhiri anafundishwa Sheria lakini hajawahi hata hata kuingia mahakamani, mkufunzi anafundisha masuala ya ujenzi wa barabara, mekanika uandishi wa habari, udakitari, n.k mwalimu huyo hajawahi hata kufanya kazi hizo wala kuijua mitambo inayohusiana kazi hiyo. Hapa anaeleza tu kwa nadharia saana, ameajiriwa tu kwa kuwa ana namba nzuri ya ufaulu aliokariri kwenye vitabu wakati anasoma, lakini fani zinahitaji mtu afundishwe kwa vitendo ili apate ujuzi. Mamlaka zikilifanyia kazi suala hili tutapata wahitimu wenye ujuzi na kutegemea na taifa
  • Kuona elimu kuwa ni huduma zaidi kuliko biashara, vyuo vikuu vina idadi kubwa, hapa unakuta darasa moja lina wanafunzi kuanzia mia tatu na zaidi, udahili wa aina hii ni kulenga kupata ada ya kutosha malengo makubwa hapa ni biashara, na siyo huduma, mkufunzi hawezi kuhudumia wanafunzi hao wote kwa uwiano sawa, hii inaathiri saana elimu yetu
  • Vyuo kushirikiana na taasisi, makumpuni au asasi zingine za elimu na ajira, hapa naamanisha kuwa na taasisi ambazo zinaingia mkataba na vyuo ili wakufunzi na wanafunzi wanaenda kufanya mafunzo kwa vitendo. Ratiba ziwekwe kwa ajili ya mafunzo haya zaidi, achalia mbali mbali “field attachments” za baada ya muhula kuisha ambazo hazina pia usimamizi mzuri.
  • Kwa ujumla mamba matano niliyoyaeleza hapo juu ni iwapo kila mtu atawajibika kutokana na nafasi yake basi miaka mitano mpaka kumi tutashudia mabadiliko mkubwa ya wahitimu wetu kuajirika na kujiari hiyo tutatengezea ajira za kutosha.
……………………………mwisho………………………………………….
 
Upvote 2
Back
Top Bottom