Baija Bolobi
JF-Expert Member
- Feb 25, 2009
- 1,093
- 1,733
Wana JF
Mtakumbuka wiki hii mwanzoni ilisikika clip yenye sauti inayodaiwa kuwa Christopher Ole Sendeka - Mkuu wa Mkoa wa Njombe. Clip hiyo ilizungumzia hali ya demokrasia nchini pamoja na mkakati wa kuzima njama za kubadili katiba ili kumwezesha rais kuongoza kwa miaka 7 badala ya miaka 5 iliyo katika katiba ya sasa. Sauti ilisikika ikidai kama bunge lingekuwa na meno, linapaswa ku - impeach rais ili kuokoa hali ya mambo. Sendeka aliikana hata kama Spika ameagiza Kamati ya maadili kumuita na kumhoji. Katika thread Fulani iliyozunguka, ilidaiwa Sendeka anakiri kuwa sauti ile ni yake.
Taarifa ya Ikulu iliyoripoti mazungumzo kati ya rais na Humphrey Polepole na kwamba rais anasikitishwa na mjadala huu, yaweza kuwa imechochewa na clip ya Ole Sendeka kwa sababu zifuatazo:
-Rais amegundua kuwa kuna unafiki mwingi serikalini na kwenye chama. Kumsikia mteule wake naye akiteta negatively juu ya rais, inashtua na kumfanya aamini kuwa wapo wengine hata kama wako kimya.
-Kwa nini amuite Polepole badala ya kumuita Komredi Kinana ambaye ndiye mtendaji mkuu wa chama? Si ajabu ana habari kuwa hata yeye hapendi pendekezo hilo. Mdhamini mkuu wa pendekezo hili amekuwa ni Polepole kwa chini chini.
-lip ya Sendeka inafunua ukweli mchungu kuwa hali ya demokrasia ndani ya nchi na ndani ya chini si nzuri hata kidogo. Kila jambo lina mwisho.
--/Baija