Huwa ninasema na ninaendelea kusisitiza kuwa Magufuli hajawahi kupambana na ufisadi, na hatakaa apambane na ufisadi, sana sana anapambana na matumizi ya neno ufisadi. Magufuli kama Magufuli ana wivu na nongwa ya kisiasa dhidi ya cdm, na kwakuwa cdm ilikubalika kutokana na ajenda hiyo ya ufisadi, basi akaipoka akidhani ccm nayo itapata mvuto kama cdm. Lakini alipotaka kupambana na ufisadi, akakuta ndio mti waliojenga ccm, tena karibia viongozi wote waliokuwa waandamizi wa ccm, na akajua fika akichukua hatua hata yeye atakuwa muhusika.
Baada ya kujua yeye binafsi na wanaccm wenzake ndio hasa mafisadi, akaifuta mahakama ya mafisadi, akapiga marufuku vyama vya siasa kufanya shughuli za kisiasa nchi nzima, na lengo hasa ilikuwa ni kuizua cdm. Akabana uhuru wa vyombo vya habari, ili uchafu usiendelee kuweka wazi, kisha akaanzisha kitengo cha propaganda kuhadaa umma kuwa anapambana na ufisadi. Bunge nalo akalifunga mikono na miguu ili limtii yeye na kuuza uhuru wake. Kiongozi wa aina hiyo hawezi kupambana na ufisadi.
Sasa hivi miaka mitano imetimia muda wa kutoa mahesabu, wanaccm wote hawako tayari Magufuli aingie kwenye ushindani, wanataka apite bila kupingwa, maana wanajua fika akibanwa kwenye hoja zote, lazima atachemsha. Hivyo wanaccm kutaka Magufuli asishindane ni kwakuwa wanajua fika akitokea mshindani akaweka mapungufu yake hadharani, basi atajikuta kwenye wakati mgumu kama JK dhidi ya Dr. Slaa uchaguzi wa 2010. Kimsingi ccm wanaweza kucheza hiyo rafu ili Magufuli awe mgombea pekee, ila hofu yao ni hii hali ya Marekani kushikia bango uchaguzi wetu wa sasa. Hivyo wanajaribu kuweka mazingira ili asiwe na mshindani, lakini mazingira ya kisiasa waliyoweka sio rafiki, hivyo wamemkamata Mbatia na Lipumba ili wawasaidie kwenye huu mziki.