Miaka 50 imetimia Tangu Dunia Isimame kushuhudia Pambano Kubwa La Ngumi Kutokea

Miaka 50 imetimia Tangu Dunia Isimame kushuhudia Pambano Kubwa La Ngumi Kutokea

ankol

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2012
Posts
2,355
Reaction score
4,260
Ilikua jumatano kama ya leo Tarehe hii hii mwezi huu huu mwaka 1974, Ndio miaka 50 pale Dunia iliposhuhudia mpambano mkubwa wa ngumi haukuwahi kutokea kati ya bondia George Foremen (Big George) na Muhammed Ali (The Greatest).

Pambano hilo la aina yake lililopewa jina la Rhumble in the Jungle liliweka record ya kutazamwa na idadi kubwa ya watu 60,000 uwanjani na zaidi ya watu bilioni moja kwenye TV.(Haikuwahi kuvunjwa rekod hii)

Foremen ambae alijipatia umaarufu mkubwa enzi hizo kwa kupigana mapambano 40 bila kupigwa ambapo 37 yalikua kwa Knock out. Alikabiliana na Bondia (Underdog kipindi hicho) Muhammda Ali ambaye alikua ana miaka mi 3 tu tangu atoke jela akitumikia kifungo cha miaka 5 kwa kosa la kukataa kujiunga na jeshi la marekani ili akapigane viat Vietnam. Akipokonywa mikanda yake yote aliyoshinda.

Ali ambaye alikua na misimamo hakuona sababu ya kupigana vita na kuua binadamu mwenzako for no reason.

Deal la mpambano huo lilimfikia promota machachari wa ngumi za heavy weit Mr Don King. Lakini kutokana na Dau kubwa lililowekwa na Mabondia hao la $5million (Enzi hizo pesa ndefu Sanaa) hakuweza kulimudu hivyo kutafuta wadhamini hata nje ya nchi ili mradi tu Zipigwe!

Nyeti hizo anazipata rais kijana wa kiafrika mwenye nchi iliyojaa gold Zaire Mh Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu. Ananyanyua simu mpaka kwa Donking!

Baada ya makubaliano hayo sharti linakuja lazima mtanange huo ufanyikie Zaire!

Mobutu kujicheki $5m parefu na asingeweza kua ford ndipo anamtafuta rafiki yake Presdaa Muammar Muhammad Abu Minyar Al-Ghadafi, raisi aliyekua na mbwembwe nyingi sana ikiwemo ya kulindwa na mabinti arobaini.

Yes alikua na mabodigadi wa kike tu tena alikua akiwachagua wakiwa bikra na akawapa training ya kijeshi. Alikua hawali????

Ghadafi bila hiyana akamtumia mpunga huo kwa makubaliano tu asitajwe kuhusika dhoo ikaja fahamika baadae. (Nafikiria angempigia Mwalimu (Nyerere) aanavyopenda taito angempa mpunga na kuhamishia pambano Uhuru stediam).

Tarehe ikapangwa September 24 wamarekani wakamiminika Africa kwa wingi.

Wamarekani waliamini Africa ni pori tupu ndipo wakalibatiza pambano hilo RHUMBLE IN THE JUNGLE.

Mabondia wakawahi kuja ili ku experience hali ya hewa NO EXCUSE!

Baaasi wakati wa training ya kufa mtu Bondia George Foremen akakumbana na Jab kali sana kutoka kwa trainer wake wakati wakifanya sparing akapasuliwa kope hivyo kufanya ashonwe nyuzi 11. Pambano likabidi lipelekwe mbele mpaka apone majeraha ndioo likapangwa siku ya leo 30.10.1974.

Basi watumbuizaji toka sehemu mbalimbali wakamiminika akiwamo Miriam Makeba (Mama wetu wa Africa) kina James Brown (Wale wahenga wa ITV mtakumbuka kuna kipindi cha vichekesho miaka ile kilikua kuna jingo yake ya I feel good Talalala, so good tata, so good tata agaryeeah).

Mpambano wa round 15 ukaanza

Zilipigwa ngumi kali, George ambaye anasemekana ndi bondia mweye heavy punch kutokea ulimwenguni (Ngumi yenye uzito wa 40ft) alimpopoa nazo Ali ambaye muda mwingi alionekana ameshikilia Kamba .

Makelele yakatoka kwa watazamaji ali daance. Yaani aruke ruke mana anaweza akakutana na kitu kizito.

Still aliendelea na stile yake ileile ambayo ailkua kuulizwa akasema inaitwa rope a dope. (Usiijaribu hii kama unataka kuishi)

Ilipofika round ya nne Ali alionekana dhoofu wa hali akaruhusu punch nyingi tu ula akikwepesha sura yake (si unajua ni bondia mhendsam?) Kila mtu alijua hatomaliza round.

Round ya nane hii hapa Punch za George hazikua na uzito tena kiviile alishajitutumua sana round za awali hivyo akaingia 18yard ya Ali na kupewa uppercut moja akisindikizwa na jab iliyomfanya alewe, wakati akienda kuisalimia sakafu Ali akataka amalizie na Left Hook akakumbuka (Usiue bila sababu maalum)

Pambano likamalizika kwa Ali kutangazwa Bingwa mpya wa World Boxing Champion, watu hawakuamini, Minongono ikaanza kua second wa George alipewa mlungula akapewa chupa ya maji yenye madawa (drugs) ili ampe George alewe aweze kupoteza, ambapo inasemekana The Don King ndio alidhamini mpango huo.
Je Mzee mwenzangu unakumbuka chochote kuhusu mpambano huo? Tiririka.
 
Watazamaji elf 60 alafu unasema haijawahi vunjwa rekodi ya watazamaji wengi namna hiyo au mimi sijakuelewa?

Mapambano ya Antony joshua unayafuatilia kweli wewe siku hizi ukajua yanaingiza idadi ya watu wangapi
 
Shikamoo baada ya salami,sita changia chochote maana pamoja na uhenga wangu ila si mhenga kihivyo kushudia ya 74 maana miaka kumi na sehem baadae ndo nilizaliwa
 
Watazamaji elf 60 alafu unasema haijawahi vunjwa rekodi ya watazamaji wengi namna hiyo au mimi sijakuelewa?

Mapambano ya Antony joshua unayafuatilia kweli wewe siku hizi ukajua yanaingiza idadi ya watu wangapi
60k live, zaidi ya B on TV, pambano recently amablo limetazamwa na wengi ni Mayweather na Manny. ambapo no 4.6m. umeelewa mjukuu? haya vaa pempasi ukacheze!!
 
Hapo ulipoandika

"..ngumi ina uzito wa 40ft.." nikajua kabisa utakua ngwini wa KLF ua HKL (Bora hata wa HGK na HGL wanakutanaga na hesabu kwenye geography).
 
Watazamaji elf 60 alafu unasema haijawahi vunjwa rekodi ya watazamaji wengi namna hiyo au mimi sijakuelewa?

Mapambano ya Antony joshua unayafuatilia kweli wewe siku hizi ukajua yanaingiza idadi ya watu wangapi
Watu elfu 60 ni uwanja wamkapa ujae full house hao niwaliopo live, acha kwenye ma tv hii sio mchezo ujue
 
Hapo ulipoandika

"..ngumi ina uzito wa 40ft.." nikajua kabisa utakua ngwini wa KLF ua HKL (Bora hata wa HGK na HGL wanakutanaga na hesabu kwenye geography).
Ww mwenyew najua hujui haya twambie
 
Hapo ulipoandika

"..ngumi ina uzito wa 40ft.." nikajua kabisa utakua ngwini wa KLF ua HKL (Bora hata wa HGK na HGL wanakutanaga na hesabu kwenye geography).
Hizo ni adverb mjukuu, haya acha kula kamasi, si nilikwambia uwe unapenga?
 
Mzee Ali makonde ya Foreman ndiyo yalikuja kumpa Parkinson’s disease baadae kwenye maisha yake.

Inadaiwa siku hiyo alipigwa makonde mengi na mazito sana kutoka kwa mpinzani wake and well kipindi hiko ndiyo kulikuwa na watu wanaopiga mawe hasa siyo kama leo mtu anapigwa ngumi mbili za pua na haangaiki hata kuzifuta na gloves.
 
Watu elfu 60 ni uwanja wamkapa ujae full house hao niwaliopo live, acha kwenye ma tv hii sio mchezo ujue
Uwanja wa Wembley stadium unajaza watu wangapi? Ndo Joshua huwa anapigia show zake na uko full house
 
Watazamaji elf 60 alafu unasema haijawahi vunjwa rekodi ya watazamaji wengi namna hiyo au mimi sijakuelewa?

Mapambano ya Antony joshua unayafuatilia kweli wewe siku hizi ukajua yanaingiza idadi ya watu wangapi
Na yanatazamwa na watu billion moja live?
 
Uwanja wa Wembley stadium unajaza watu wangapi? Ndo Joshua huwa anapigia show zake na uko full house
Joshua hajawahi weka record ya most viewed boxing match, by the way si nilikwambia ukavae pempasi? Ona sasa umejinyea!!
 
1974 nilikuwa bado mdogo sana,familia haikuwa na TV,labda kama wazazi walienda kuangalia kwenye jumba la sinema,ila hapo kwenye ngumu za George Foremen zenye uzito wa 40ft naomba urekebishe,nadhani ulimaanisha 40kg au tones......
 
Back
Top Bottom