Miaka 50 ya JWTZ na somo alilojifunza Mwalimu Nyerere

Miaka 50 ya JWTZ na somo alilojifunza Mwalimu Nyerere

MBATATA

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2013
Posts
542
Reaction score
209
Miaka michache iliyopita baadhi ya wanajeshi wakiungwa mkono na wakazi wa kisiwa kimojawapo cha vinavyounda nchi ya Komoro waliasi na kutaka kujitenga kwa kutumia nguvu ya wanajeshi walioasi.

Tanzania ilipata umaarufu baada ya kuombwa na kufanikiwa kuyasaidia majeshi ya serikali ya Komoro kuzima maasi hayo, huku kiongozi wao akijaribu kutoroka nchini humo. Inasemekana alitumia mbinu ya kubadili mwonekano wa kijinsia kwa kuvaa baibui (buibui) - vazi linalotumiwa sana na wanawake katika jamii mbalimbali za Arabuni, Mashariki ya Kati, na pwani ya Afrika Mashariki.

Hata hivyo mbinu hii haikumsaidia maana alikamatwa na hadi hivi sasa wengine hatujui hatma yake ilikuwaje.

Rejea miaka 50 iliyopita (1964) nchini Tanzania. Baadhi ya vikosi vya jeshi nchini wakati huo likiitwa "Tanganyika Rifles" viliasi kwa madhumuni ya kushinikiza kuboreshewa maslahi (sina hakika kama kusudio lilikuwa ni kuipindua serikali ya Bwana Nyerere au la, wakati huo ikiwa madarakani).

Vikosi hivi vilizua tafrani kubwa haswa mjini Dar es Salaam naTabora ambapo kambi za vikosi vyenye dhamana ya bohari za silaha vilikuwepo.

Kwa mujibu wa mashuhuda na simulizi tulizokujapata baadaye, inasemekana katika tafrani hiyo, mashaka makubwa yaliwakumba viongozi wa serikali akiwemo Bwana Nyerere na watu wake wa karibu. Suala moja muhimu likawa ni namna ya kumwepusha yeye binafsi na madhara yoyote, haswa endapo wale askari waasi wangeelekeza hasira zao dhidi yake kama Amiri Jeshi Mkuu.

Inasemekana tena, kwamba kuna mtu mmoja (Kambona?) aliyewasaidia kuwaweka salama aliyetoa wazo kwamba njia nzuri ya kuwaokoa ni kuwavisha Nyerere, Kawawa, na wengine vazi la baibui (buibui) na kuwatorosha kwa siri toka sehemu waliokuwepo na kuwapeleka mafichoni (kuwapakiza kwenye mtumbwi na kuwavusha kwenda Kigamboni?).

Kama ni kweli anastahili pongezi kwa ubunifu huo uliowasalimisha viongozi!

Baada ya hapo mambo yalipokuja kutulia Nyerere akalifumua jeshi na kuliunda upya na ndipo lilipoundwa jeshi la"Wananchi" ili kuendana na dhana ya kwamba uhuru uliopatikana miaka michache kabla ya tukio hili, ulikuwa uhuru wenye lengo la kupigania maslahi yaWatanzania wote na sio kundi moja lililokabidhiwa silaha za kivita.

Lakini kwa kweli kama mwalimu alivishwa"buibui" najaribu kutafakari hasira aliyokuwa nayo kutokana na kudhalilishwa kiasi hicho.
Ukiachia mbali kuvishwa buibui akina Nyerere, ni suala lenye ukweli kihistoria kuwa maasi yaliwahi tokea nchini
mwetu, na yale waliyofanya waliomnusuru kutokana na dhahama hiyo yanastahilikurejewa na kuwekewa kumbukumbu stahili.

Aliyoyafanya Nyerere baada ya hayo hayakuwa rahisi na yalihitaji ustadi mkubwa na tafakari ya hali ya juu.
Wapo kina marehemu Kambona na wengine waliochangia kutuliza mambo na hata kwa kuwashawishi
Maaskari kuacha fujo wakati ule na walifanikiwa.

Na ndipo Nyerere katika kuliunda upya Jeshi akaweka mkakati wa kujihami yeye na serikali yake kwa utaratibu wa Jeshi kuchukua vijana wengi zaidi kutoka mikoa fulani ya kaskazini mwa nchi.

Tunapoadhimisha tukio kama hili la miaka 50ya "Jeshi la Wananchi", tusisahau mambo 2 ambayo yana umuhimu mkubwa kwa nchi hii:

1. Kwanza, usalama wa viongozi unategemeapia utulivu wa walinzi wetu

2. Ili taifa liwe salama ni muhimu kwanza kwa kiongozi mkuu kuwa salama.

Lisije likatokea tenala kuvishwa buibui viongozi wa kitaifa.
 
MBATATARiport yako imejaa mambo ya kufikirika na kusadikika na mambo ya story za vijiweni si sahii, hata hivyo ngoja tusubiri wengine watasemaje.
 
Kwa hiyo unataka kutuambia kwamba kuanzishwa kwa jwtz ilivyo hadi leo ni kutokana na kwa hasira za nyerere kuvishwa buibui?
 
Kwa hiyo unataka kutuambia kwamba kuanzishwa kwa jwtz ilivyo hadi leo ni kutokana na kwa hasira za nyerere kuvishwa buibui?

Mkuu Mavumbi,
La msingi hapa ni kwamba Nyerere alipata somo ambalo hakulisahau mpaka mwisho wa maisha yake. Na kwa namna moja ama nyingine somo hilo lilituathiri hata sisi wengine
 
Mkuu Mavumbi,
La msingi hapa ni kwamba Nyerere alipata somo ambalo hakulisahau mpaka mwisho wa maisha yake. Na kwa namna moja ama nyingine somo hilo lilituathiri hata sisi wengine

Uliathirikaje? WEWE mwenyewe umesema ili taifa liwe salama lazima kwanza kingozi mkuu awe salama! Au ulitaka kazi ya uanajeshi ukakosa?
 
kwanza kabla ya yote tell us the motive behind your thread.usikute ni mnyarwanda wewe.
 
Kuna topiki hazitakiwa kuwa kwenye jukwaa la historia bali zipelekwa kwenye jukwaa la siasa. Jukwaa la historia linatakiwa kuwa na historical facts ambazo zimeshafanyiwa research ya uhakika na wala siyo mahali pa malumbano na hisia bali ni mahali pa kuelimishana kuhusu matukio ya zamani. Thread hii haiko panapostahili!
 
kwanza kabla ya yote tell us the motive behind your thread.usikute ni mnyarwanda wewe.

Tunapoadhimisha tukio kama hili la miaka 50ya "Jeshi la Wananchi", tusisahau mambo 2 ambayo yana umuhimu mkubwa kwa nchi hii:

1. Kwanza, usalama wa viongozi unategemeapia utulivu wa walinzi wetu

2. Ili taifa liwe salama ni muhimu kwanza kwa kiongozi mkuu kuwa salama.

Lisije likatokea tenala kuvishwa buibui viongozi wa kitaifa.

SOMO TOSHELEZA
 
Na ndipo Nyerere katika kuliunda upya Jeshi akaweka mkakati wa kujihami yeye na serikali yake kwa utaratibu wa Jeshi kuchukua vijana wengi zaidi kutoka mikoa fulani ya kaskazini mwa nchi.

Duh Hapo ndio nimechoka kabisa na Historia Sahihi ya Miaka 50 ya JWTZ
 
Kuna topiki hazitakiwa kuwa kwenye jukwaa la historia bali zipelekwa kwenye jukwaa la siasa. Jukwaa la historia linatakiwa kuwa na historical facts ambazo zimeshafanyiwa research ya uhakika na wala siyo mahali pa malumbano na hisia bali ni mahali pa kuelimishana kuhusu matukio ya zamani. Thread hii haiko panapostahili!
Adhimisho la tuko kuu kama hli ni la historia, na huwa linakwa na hisia tupende tusipende.

Aidha ili historia iwekwe katika muktadha muafaka, yapo mambo ambayo huibuliwa kwa lengo la kuzipata hizo historical facts........Mfano: Nani aliyeongoza mapinduzi Zanzibar?
 
Kwani ungeandika Baba wa Taifa badala ya bwana Nyerere ungepungukiwa nini.?

Stori haina mvuto zaid ya chuki tu.
 
Hujaibua hoja bali umehubiri imani yako.

Swala la jaribio la mapinduzi ya mwaka 1964 tulishalijadili sana hapa mpaka zikatolewa rekodi za majabiliano na Brigadier Douglas ambaye ndiye aliyekuwa mkuu wa majeshi wakati huo na kuonyesha role ya Kambona katika maasi yale, na jinsi ambavyo Nyerere na Kawawa walivyofichwa Kigamboni. Kuna references nyingi za uhakika kuhusu swala hilo ambapo maasi yalianzia kambi ya Colito (Lugalo) na kusambaa hadi kambi ya Nachingwea na Tabora. Kuzimwa kwa maasi yale ilikuwa ni kutokana na msaada wa makomadoo wa kiingereza ambapo pamoja na mambo mengine wanajeshi wa kambi ya Colito walileweshwa hadi wakatekwa kirahisi na makomando hao waliokuwa wameletwa kutokea ghuba ya uajemi.

Baada ya maasi kuzimwa Nyerere alitangaza redioni akisema "Jana nililazimika kuomba msaada wa Mwingereza. Kwa bahati akakubali. Asubuhi hii kikosi cha kwanza kikawasili …yote sasa ni shwari. Nasikia maneno ya wajinga kwamba eti Waingereza wamerudi Tanganyika."

Ni katika hotuba hiyo ndiyo alisema maneno "…Askari wametuvua nguo. Tuko uchi. Jamaa wanasema tuazime nguo, nasema nguo ya kuazima bwana! …Unaweza kwenda kuazima ukapata baibui."

Tumeshaelimishwa vizuri sana kuhusu jambo hilo, na ingekusaida iwpo ungetafuta hapa JF kuhusu topiki hiyo kabla hujaandika mambo yasiyokuwa na ushahidi kwa kuhisi eti "inasemekana....."
 
Kwani ungeandika Baba wa Taifa badala ya bwana Nyerere ungepungukiwa nini.?

Stori haina mvuto zaid ya chuki tu.

Tunapoadhimisha tukio kama hili la miaka 50ya "Jeshi la Wananchi", tusisahau mambo 2 ambayo yana umuhimu mkubwa kwa nchi hii:

1. Kwanza, usalama wa viongozi unategemeapia utulivu wa walinzi wetu

2. Ili taifa liwe salama ni muhimu kwanza kwa kiongozi mkuu kuwa salama.

Hata ingekuwa wewe ndio Rais bado ningesema unastahili kuwa salama........hili nalo ni chuki? Kuna shida gani Nyerere kutoitwa Baba wa Taifa?

Back
Top Bottom