Miaka 50 Ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Bado Kuna Maswali Bila Majibu -1



Mkuu Pasco,

Duh! Mbona hayo maelekezo yako yamejaa jazba,chuki,farka na urongo ulokubuhu...umekumbwa na nini Mkuu!?

Nakhis wewe hufahamu asilan hiyo society ya Kizanzibary na mahusiano/maingiliano baina yao!...yaani Historia ulosomeshwa ndo ile ile tu ya upotoshwaji alotengeneza yule Nyerere na genge lake!? Dah!

Au wewe umesomeshwa history ya Zanzibar kwa perspective ya wale Wazungu!? Je ushawasoma na Waarabu wenyewe wanasemaje!?

Kabla ya kwenda mbali mno...embu tupe maana ya neno "Waswahili" kama ulivyolitumia hapo juu!?

Je unafahamu family Tree/branches za huyo Mohammed Shamte!?...tafadhali tudadavulie hapa jamvini...ukimaliza tufahamishe je yeye ana-qualify huo "Uswahili" kama ulivyotaja hapo kwenye bayana yako au Uarabau ambao wewe usotaka kuusikia asilan!? Dah! Teeh! Teeh! Teeh!

Tashkuru mno kukusikiza.

Ahsanta.
 
nasubiri rebutal toka kwa Mohammed Said na Harith Ghassany

wote wameandika vitabu

hakuna aliyekuja na vitabu ku rebutal thesis zao

of course ilikuwa ni Pasco pekee ambaye alisema kuwa Harith Ghasany alipewa PHD na Harvard University

Toka niliposoma ile comment toka kwa pasco sikumwona mtu ambaye ni serious na hasa ukizingatia naye ni msomi miongoni mwa wasomi wa JF
 

Wala huhitaji kufanya utafiti mkubwa. Thabit Kombo ambaye alikuwa ASP damu amelieleza hili waziwazi kwamba ASP walichagua constitutional monarch na nadhani ilikuwa March 1963.

Cc: Pasco
 
Nani alikwambia kwamba swali zuri hapa duniani jibu lake litoke kwa Pasco? Hii ni dhahiri kwamba huna jibu hata wewe.

Cc: Pasco
Nilijibu.
 
Hiyo ni fact!.
Maoni yangu kumhusu huyo jamaa ni haya.
Merry Chrismass
Pasco
 
Nilijibu.


Pasco nikurekibishe Mohamed Shamte hakuwahi kuwa mwana ASP yeye kabla ya kuundwa kwa asp alikua rais wa Shiraz Association. Muungano wa African association na shirazi association ulifadhiliwa na TANU na usimamizi wa nyerere ulifanya bila ya kuwashirikisha viongozi wa shirazi association wa Pemba akiwamo Shamte. Thabit kombo na sheikh Tajo walikubali miungano huu bila ya wenzao na ndipo ZPPP ikanzishwa chini ya shamte.
So shamte hakuwahi kuwa Asp. Na hakika hapa ndio kisa cha Asp na sasa CCm haina ushawishi Pemba kwa sababu zilizo wazi
 
Hiyo ni fact!.
Maoni yangu kumhusu huyo jamaa ni haya.

Merry Chrismass
Pasco

Kitabu Cha Okelo? OKELO mchonga matufali ya matumbawe kasoma wapi akajuwa kuandika aubkasomeshwa na Mungu wake wa Waafrika?

Kitabu cha Okelo kimeandikwa na Mzungu je yeye kashiriki hayo the so called mapinduzi?
 
Hiyo ni fact!.
Maoni yangu kumhusu huyo jamaa ni haya.

Merry Chrismass
Pasco

wewe umekisoma Kitabu cha Ghassany? Kakisome kwanza kija uje na hoja za maana. Pia kasome tena uwajuwe serikali ya mseto walikuwamo nani. Hakuna record hata moja inayosema kama Shamte alikataa serikali ya Umoja wa Kitaifa. LAKINI IKO RECORD YA ASP YA UHURU ZUIA!!
 
Mkuu nakusoma kwa umakini sana endelea kutoa darsa.
 

Ufahamu wa Historia unatofautiana ndugu yangu Pasco. Naomba kuuliza, ina maana Waarabu walipofika Zanzibar walikuta visiwa ni vitupu havina watu wa aina yoyote?
 
. Nikakisome wapi tena wakati kimeletwa humu jf, kitabu kizima kipo!. Ninayo nakala nimepewa na rafiki yangu binti wa Kizanzibari, yule mwanahabari Salma Said. Nimekisoma na kukisoma na kukisoma na humu jf pia ni mimi ndio nimekiweka na tumekiponda humu kama tulivyoyapobda maandishi ya Maalim Mohamed Saidi na kisa cha wazee wake wa Gerezani!.

Ghassany anaandika historia ya Mapinduzi kwa kuwahoji watu waliohadithiwa hayo mapinduzi according to waarabu waliopinduliwa!, huku anawaacha walioyafanya mapinduzi hayo huku wakingali hai!. Anatukuza biashara haramu dhalimu ya utumwa ilioletwa na Waarabu kwa kusingizia ililetwa na wazungu!.


Ghasani kaleta uzushi wa Mapinduzi kwa kuandika hadithi za fasihi simulizi kwa watu baki!. Wakati akiandika mashujaa wengi wa Mapinduzi walikuwa wakingali hai!, kwa nini asiwahoji hao, anakwenda kuhoji watu baki waso jina ndani ya mapinduzi yenyewe halisi?!.

Kwa faida ya wengine ambao hawajakisoma kitabu, link hii hapo someni kitabu!. Kwaheri Ukoloni- Kwaheri Uhuru...Dk. Harith Ghassany ...

Hoja yangu kwenye uzi huu bado inasimama, bado kuna maswali mengi kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar kuliko majibu!.

Hoja yangu kwenye uzi huu, ni baadhi ya hoja zenye maswali yasiyo na majibu kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar!. Kuna vitu nimewauliza, majibu mnayo leteni!, majibu hamna, tulieni kimya kama mlivyitulia, tuacheni tuendelee na maandalizi ya kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, tukimaliza tusherehekee Muungano Adhimu.
Pasco.
 
Kama kawaida yako....Bichwa kama nazi vile!
Mkuu Kihega, yanatoka wapi haya?!. Usifikiri wale .... wote ni mpaka waokote makopo!, wengine ni .... ila wao hawaokoti makopo bali ...wao utambua kwenye mabandiko yao!. Tafadhali tuondolee ...chako kwenye uzi huu!. Please!.
Pasco.
 
Ufahamu wa Historia unatofautiana ndugu yangu Pasco. Naomba kuuliza, ina maana Waarabu walipofika Zanzibar walikuta visiwa ni vitupu havina watu wa aina yoyote?
. Hawakukuta mtu!, inasemekana mwanzo visiwa hivi vilikaliwa na Wahadimu na Watumbatu, ila hakuna kumbukumbu yoyote ya kihistoria inayoonyesha Sultan Sayyid Said hakunegotiate na yoyote kuvitwaa visiwa vile as if aliviokota!. Yaani alipofika hakukuta wenyewe!. Ila excavations na ruins ndio zilithibitisha kuwepo maisha kabla ya Waarabu!. Inamaanisha waliokuwepo waliteketea wote!, au waliteketezwa!, maana Waarabu! usipime!.

Sio kama Kilwa Hassan Bin Amiri, alikinunua kisiwa cha Kilwa kwa wenyeji kwa gharama ya kitambaa cha kukizunguka kisiwa chote!.

Katika safari za Ibin Batuta, anazungumzia wenyeji wa Kilwa na sio wenyeji wa Zanzibar!.

Ya Zanzibar ni kama ile hadithi ya Bistani ya Aden ni Ngorongoro Creater!, Dr. Richard Leakey na Mkewe ndiko walikolivumbua fuvu la mtu wa kale kabisa anayesemekana atakuwa ndio Adamu!.
Pasco
 

Sasa kwanini na wewe huendi kwa hao watu baki ukawakadhibisha kuwa wanasema uwongo?

Ivo mapinduzi yamekuja kuondosha utumwa? Kama si Seyyid Sultan bin Saif Al Yaarubi kuwatowa Wareno East Africa labda wewe ungalizaliwa Cabo Verde au Sao Paulo maana Wareno walikuwa wakikamata waafrika kinyama kama vile ngedere na kuwauwa na kuwabaka wanawake.

Kule Tabora kama si Rumaliza ambaye babu yake Ali Muhsin mzaa mama basi wajerumani wangaliwamaliza waafrika na mpka leo hakuna hata mmoja anaemtaja Rumaliza kama ni shujaa sababu ni Mwarabu.

Mnakataa kutambua ukweli wa kitabu cha Ghassany sababu kinasema ukweli hasa pale alopwahoji kina Mkwawa na wenzake walio hai. Zaidi kuwa mauwaji ya 1964 pia yanaonyesha hata hao ASP waliuliwa nao kwa winhi na hao manamba wa kimakonde walioshindwa kutofautisha baina ya waarabu na machotara wa kishirazi na kihadimu.

Tena usiwatukane wazanzibari hasa wahadimu na watumbatu sababu ni.makabila yaliyokuwa huru na hawajawahi kuingizwa utumwani.

Utumwa Zanzibar ulipigwa marufulu since 1879 iweje Zanzibar ukaweko utumwa 1964. Rudi darasani ukasome historia ya mabwana zenu wa kiingereza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…