Miaka 50 Ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Bado Kuna Maswali Bila Majibu -1

Kwa hiyo unachotaka kusema ni kuwa hata ASP wanamhitaji sultani?. Jitoeni CCM, rudisheni ASP muiteni Sulani arejee awatawale!.
Pasco.

Ninachosema ni kuwa ASP and so now CCM na watu kama wewe wasilete unafiki kuwa eti Sultan atarudi kutawala Zanzibar hiyo ndio Wimbo wa Taifa wa wahfidhina wasitaka mageuzi na maendeleo ya Zanzibar kwa kukinga nafasi zao.madarkani na mtu kama wewe kama una fikra timamu ukawa unawapigia debe.

Kwani unafiki wao ni kuficha ile historia kuwa wao ASP walitaka Constitutionql Monarchy kama ya UK na waliahidi kumlinda Sultan na ukoo wote wa Kifalme mpaka kufa.

Hebu nambie katika records za mauwaji ya 1964 kuna member gani wa Kifalme alouwawa?

Na wengine bado wapo wanaishi pale Zanzibar mpaka leo.

Sultan kama anataka.kurudi atarudi Oman kwenye ukoo wake amabako.anweza kupigania rights zake za kifamilia na pia kunautajiri mkubwa kuliko Zanzibar na ambako ni.chi yenye hadhi kubwa kimataifa.

Sultan aje kutawala Zanzibar kwa misingi gani?

Hivi huu Muungano lengo lake ni kuwa kaondoka Sultan wa Kiarabu ambae alikuwa just a paper Sultan alokuwa hana mamlaka hata kuruhusu matumizi ya nchi yake kama British Resident hajaruhusu, na badala yake ni Usultani mpya kutoka Tanganyika ambao unafanya yale yale yalokuwa yakifanywa n Muingereza!

Hivi wewe umeona wapi nchi ambayo imekuja ku exist after the scramble for Africa nchi amabayo imepata jina Tanganyika katika mwaka 1920 ikubalike kuifuta nchi ambayo ina exist since 9AD karne ya Tisa!!

Ushahidi upo kama Tanganyika, Kenya, Uganda, Burundi, Ruwanda, Malawi na zenginezo hazikuwapo mpaka baada ya 1885 mkutano wa Varseilles wa kuigawa Africa katika makoloni ya Wazungu lakini Zanzibar ilikuwako na ilikuwa Dola yenye Ustaarabu na Uchumi mkubwa na nguvu hata za kijeshi.

Hizo nchi zote nilizozitaja zilikuwa katika eneo moja tu kusini ya jangwa la Sahara eneo likiitwa Ethiopia ni neno la Kiyunani lenye maana ya Watu Walioungua Nyuso (Watu Weusi).

Pasco rudi maktaba pale UDSM katafute uchimbe uje ulikatae hili.
 
Ni dhahiri kwamba Tanganyika iliipindua/iliisogeza Zanzibar kutoka UN!
 

Pasco,

Unasema na nakunukuu: ''Nimekisoma na kukisoma na kukisoma na humu jf
pia ni mimi ndio nimekiweka na tumekiponda humu kama tulivyoyapobda
maandishi ya Maalim Mohamed Saidi na kisa cha wazee wake wa Gerezani!.''

Kwanza awali ya yote Pasco jifunze kuandika vizuri kisha ndiyo utoke ukumbi.
Pili jifunze adabu ya mnakasha.

Wewe hujafikia makamo ya ''kuponda'' kazi ya Dk Harith Ghassany kwa kigezo
chochote kile ukijuacho wewe na mfano wa wewe.

Tatu wewe hujafikia hali ya kukabiliana na mimi.
Mimi nikinyanyua kalamu huwa sikukusudii wewe na mfano wa wewe.

Asilani wewe Pasco huingii katika fikra zangu.
Utaingia kwa kipi khasa?

Mimi kuna watu nawakusudia na wao wakisikia Mohamed yuko uwanjani
hutoka kuja nisikiza na wengi hawachangii.

Wanakuja kusoma.

Huja kama anavyopenda kusema Spike Lee huja ''kufyonza elimu.''

Lakini umenifurahisha kitu kimoja.
Umeniita ''Maalim.''

Jina hili mimi marehemu mama yangu alikuwa akiniita bado mie mdogo sana.
Akiniita hivyo kwa kuwa baba yake alikuwa sheikh akisomesha.

Mimi akanita ''Mohamed'' jina la baba yake yaaani babu yangu.
Kwa mila zetu akawa wakati mwingine anaona tabu kumkata baba yake jina.

Akawa sasa anaangukia katika ''Mwalimu Mohamed.''
Kanipa cheo cha kudarsisha.

Wakati mwingine akinita ''Sheikh.''

Bibi yangu Bi. Mwantum bint Rajab yeye akawa ananiita ''Bwana
Mohamed.''


Mimi mume wake.

Ikiwa lazima atutaje wote wawili kwa pamoja babu yangu kwa kuwa alikuwa
kafariki akawa anaiitwa ''Hayati Bwana'' na mimi ''Bwana Mohamed.''

Historia ya Gerezani nimeisomesha hapa na hivi sasa wachapaji wananiomba
niiifanye kitabu.

Mama yangu hakika kaishi na kaniona nikifuata nyayo za babu somo yangu
Mwalimu Mohamed.

Nasomesha kama alivyosomesha babu yangu.

Hii ni bashraf.
In Sha Allah subiri waimbaji watajitokeza katika jukwaa si muda mrefu.
 
Last edited by a moderator:
 
Mukulu......Hoja ya Pasco ni "BADO KUNA MASWALI AMBAYO HAYANA MAJIBU"....Kama ni kweli tutafute hayo majibu!

Hata hivyo mwambie basi huyo Pasco wako aache kabisa kupotosha history kwa kusema urongo!...ambapo mbadala wake yaezaleta amma kuzidisha farka,chuki na migongano katika jamii!?

Pia mwambie ajibu masuali kadhaa pia aulizwayo na Wanajamvi kwenye hii thread aloanzisha yeye mwenyewe!

Ahsanta sana.
 



Khawarizm,

Nakusoma kwa utuvu ulo mwingi.

Nataka huyo Mbara/Mtanganyika mpotofu wa Ilm na fikra ajiitae Pasco tumsomeshe na kumfunda hapa ukumbini mpaka akimbie!

Tupamoja mno Mkuu wangu!

Ahsanta.
 


Dah! Yaani wewe jamaa unazidi kunisikitisha mno!

Yaani hiyo Theory yako dhaifu hapo juu haina tafauti asilan na ile Theory ya kinyama au yenye umaluuni wa kitaaluma waliokua wakieneza wale maharamia wa South Afrikan Apartheid Regime kwenye propagandas zao...ati yakuwa walipofika ndani ya South/Sud Afrika wao hawakukuta mtu mweusi/Native yeyote zaidi ya wanyama na ndege wazuri/warembo!? Duh!

sifahamu kumbukumbu zako zikoje japo naanza kuzitilia mashaka kiduchu...lakini nakhis utakumbuka wakti ule wa ile Apartheid Regime pale South Afrika,hata taarifa ya khabari yao kuanza basi ilikua ikianza kwa sauti/mlio wa ndege mwanana...yaani hiyo ndo ilikua ikiashiria amma kutilia mkazo ile Theory yao ya kiharamia na ubadhilifu wa kitaaluma!

Kwa kifupi,maelekezo yako hayako balanced asilan!...kama unajisoma kwa utuvu,yaani kwa sasa unatuchanganya hata sisi Wanajamvi wenzio humu!? Dah!

Unaropokwa na kuji-contradict kwa mangi!...

Unadai yakuwa hakuna kumbukumbu yoyote ya kihistoria inayoonyesha yakuwa Sultan alifanza makubaliano yoyote na labda Wenyeji/Natives wa Visiwa vile vya Zanzibar ili kuvitwaa/kukabidhiwa kuviendesha!?

Ina maana hapo ndo Ilm na fikra zako zilipogota Mkuu!? Wewe umesoma au umeona Manuscripts zoote kuhusu Natives wa Zanzibar!?...nina hakika jibu lako ni hapana!

Pia kama Theory yako ipo based na yayo ulonena hapo kwenye hiyo post yako...hapo itakua unaathiri haki ya Natives takriban woote ndani ya dunia hii bila ya wewe mwenyewe kufahamu au labda kwa makusudi!?

Hata wale Maharamia wa Ki-Spanish na Ki-Portugese nao pia walikua waki-report au kuhadaa wale mabwana zao Wakuu wa Makanisa waliokua wakiwatuma au kudhamini ile misafara yao ya kiharamia/ya "kivumbuzi"...yakuwa ati baadhi ya maeneo/nchi the so called colonies ati hawakukuta watu/Natives wowote!? Duh!

Hii ni khatari mno...khasa tukichukulia yakuwa history takriban zoote humu duniani huwa zaandikwa na Winners/wenye maguvu!

Ahsanta sana.
 
Swali zuri sana Ritz tunasubiri jibu Pasco.

shamte angekuwa kibaraka angewezaje kuitambulisha zanzibar huru un? na bila aibu unalikubali jukumu hilo! Shamte alikuwa kiongozi mzalendo wa zanzibar mwenye asili ya pemba, Waunguja kwa uchu wa madaraka na kutopenda kutawaliwa na wapemba wakaamua kuipindua serikali halali ya shamte na kuikabidhi nchi kwa wanaume wa TANGANYIKA
 
Kwa vile bado kuna maswali mengi hayana majibu, historia zote hapa zitakua paukwa pakawa hazina majibu ya ukweli hasa!!

Kawaida ya watawala duniani wanapoingia kwenye utawala hasa kwa njia hizi za mapinduzi na nguvu, huibadili historia ya kweli ili iwe inawasifia wao na kuwakrbehi waliokuwepo kwa kila aina ya kebehi, wengine hubadili kabisa historia hasa kwa miaka tunayoizungumza wasomi walikua wachache sana. Hivyo ni mara chache kumpata mtu kuhoji kwa kuhofia nguvu za utawala mpya.

Binafsi naichukua zaid historia ya Ghassany kwa wanamapindizu wengi wanaiunga mkono akiwemo mzee moyo na wengine.

Kubwa nimwambie mwandishi Muungano wowote duniani unadumu kwa ridhaa ya walioungana, ndio mana mwakani 2014 kuna kura ya maoni juu ya muungano wa Scotland na U.K muungano ulidumu kwa miaka 290 had sasa.

Utadumu endapo marekebisho ya msingi yatafanyika bila kuoneana haya ila kwa ukiritimba wa CCM si rahisi muungano huu kuchukua muda.


Tuwaachie wazanzibar Nchi yao na sisi tujenge Tanganyika yetu, tulipofika sasa ni pabaya huko mbele kutakuja vita.


Solution ya muda mfupi serikali 3 ila nazo hazitadumu hata miaka 10 kila mmoja atajikata kivyake.
 


Mkuu wangu Al Khawarizm!

Shukran mno kwayo! Duh!

Yaani hata nami nalitaka kuandika/kumjibu japo kiduchu...basi Wallahi sintathubutu tena kutia maguu yangu humu...yaani umemchana huyo Pasco na sidhani kama atathubutu kurejea humu tena!? Teeh! Teeh!

Wajua hawa jamaa wangi wao hawana walijualo kiundani...history zao za kudanganywa na Wazungu au mle Makanisani zawapotosha mno na kuwazidishia chuki pasi kiasi! Dah!

Ahsanta sana.
 

Narekebisha mistake transposition ya tarehe kuondolewa utumwa sio 1879 : Utumwa ulifutwa kabisa Zanzibar on 6 April 1897 by decree na Sultan Seyyid Hamoud bin Muhammad bin Said bin Sultan.

Mimi nahisi hawa Tanganyika wanaogopa Zanzibar ikiwa huru labda siku moja itadai haki yake ya kiutawala over Tanganyika kwani 1893 ni katika utawala wa Seyyid Hamed bin Thuweiny wakati huo Zanzibar ishakuwa chini ya Himaya ya GB since 1890; ndipo in 1895 Zanzibar Protectorate ilopoingia katika itifaki na UK kuiendesha utawala katika Mwambao wa Pwani (Mrima kwa wakati ule) kwa niaba ya Sultan wa Zanzibar. Baada ya kufa Seyyid Hamed ambae kwa kweli aliukacha ufalme na kufia Saint Helena Island. Katika 1896 akatawala Hamoud bin Muhammad na kutangaza kuwa kuazia 1897 mtu yeyote ataekanyaga au kuzaliwa Zanzibar atakuwa ni mtu huru na tarehe 6/4/1897 was officially implimented.

Kuanzia hapo ndipo Muingereza kutumia hadaa na akiwemo mjerumani kuipora Zanzibar mapato ya forodha waliyokusanya Bara na wakiilipa Zanzibar only rupia 11,000/- kwa Mwaka ndipo baadae Sultan nae akarudisha Mapigo kwa kuitangaza Zanzibar as Free Port so uatona huu ujanja na hizi kero za sasa za muungano kama hizi za hujuma ya kiuchumi dhidi ya Zanzibar hawa viongozi wanaiga tu kwa Mabwana zao wa Kikoloni and they are much worse maana wao wanataka hata kuifuta Zanzibar in the map of the world.
 



Mkuu Khawarizm,

Dah! Yaani shukran mno kwayo!

Nafikiri labda tumfanzie sabra kwa sasa ili atakaporejea yule Pasco aloanzisha hii thread, labda tujue nae ataleta majawaba yapi!? Teeeh! Teeh! Teeh!

Au pia atujuze nae Pasco anafahamu yapi mangine kwa undani ulo mwingi,maana hii mipini uloshusha hapa ni balaa tupu!? Duh!

Ahsanta.
 


Yaani unachofanza hapa ni kujidhalilisha na kuonyesha yakuwa huifahamu asilan history ya Zanzibar au Wazanzibary!?

Mie takujibu kwa kifupi tu...maana bado pana masuali mangine mangi toka kwa Wanajamvi wangine nayo pia yataraji/yastahili majawaba yako!?

Kwa kifupi wewe nakhis unashindwa kutafautisha baina ya social struggle na Slavery!?

Ukiwa tayari mie binafsi takutajia hapa hapa jamvini majina ya the so called Natives/Blacks Zanzibaris kadhaa ambao waliowahi kuoa ndani ya zile Aristocracy families za hao wewe uwaitao ati ndo "Waarabu"!?

Je wafahamu yakuwa enzi hiyo weye unayodai ndo ilokua na Utumwa pale Zanzibar...mbona pia palikua na Natives/Blacks wengi tu ambao ndani ya majumba na mashamba/kondeni mwao walikua na wafanyikazi wa Kizanzibary waliokua na asili ya Arabuni,Persia,Goa,Indian Sub Continent,China na pahala kwingineko kwingi mno!?

Je wafahamu yakuwa the so called Natives/Blacks Zanzibaries...pia walikua wakiruhusiwa kumiliki ardhi!?

Sasa Slavery ya aina gani hiyo unayodai wewe humu mpaka ifikie ati kuna watu humo humo kati ya Slaves nao wana haki zoote kama walizo nazo hao ulowaita ati ndo Mabwana/Waarabu au waendesha huo ulodai ati ndo utumwa!? Duh!

Hivi unafahamu ile Slavery ilokua pale Amerika kiundani na impact yake kwa Blacks dunia nzima mpaka kesho!?

Hizo sehemu zoote ulizotaja kwenye post yako hapo juu...hizo sehemu walikua wakikaa wengi wao ni Immigrants/Wahamiaji tokea sehemu mbalimbali za Mainland au Afrika!

Wengi ya wakaazi wa sehemu hizo kwa tajriban miaka mingi mno...hawakua asilan ati ni Wazanzibary,Hasha,abadan asilan!...walikua wengi wao ni pia askari waliorejea tokea zile WWI&WWII!

Na mmojawapo alikua Mzee Hussein Onyango Obama...Babu yake yule Baraka wa Amerika!

Si wafahamu yakuwa huyo Mzee Hussein Onyango...alipewa hisham na hadhi kubwa mno pale Unguja na mpaka akasilimu kwa khiyari yake mwenyewe na kupewa mke na makazi/nyumba na nduguze wa Kiislamu pale Kwa Mtipura!

Aliishi Unguja kwa miaka kadhaa na kwa raha zake!...sasa hivi kweli nchi yenye utumwa inakuwa na nafasi au takrima kwa vijakazi/watumwa wake kufikia hali hiyo!?

Ndo maana lazim ujue kiundani maana ya Slavery na social and/or political struggle!?


Ni ukweli usiopingika yakuwa wengi wao walikua ni working class blacks!...na pia wengi wao walikua si Wazanzibary wala hawakua na asili ya Zanzibar asilan!

Wengi ya Wazanzibary the so called Natives/Blacks ambao waliokua hawana uwezo/working class... walikua wakiishi mashamba/Vijijini ambako ndiko walikozaliwa au kwenye asili zao!

Hivi unafahamu kiundani yakuwa...wakti huo unaojaribu kupotosha humu jamvini ati ilikua slavery hapo Zanzibar...palikua na Wazanzibary wengi mno waliokua na asili za Kiarabu,Persia,Indian Sub Continent na kwingineko ambao walikua ni watu wa kawaida mno/working class...tena wakitumwa kuwa madobi,matopasi,wafagizi wa marikiti/masokoni,wauza samaki,wasonga halua na shughuli nyanginezo nyingi ambazo hata kwa wakti huo zalikua zikionekana pia si za hadhi ayu hishma kubwa!

Na wakti huo huo palikua na the so called blacks/natives ambao walikua na shughuli mujarab bila pingamizi zozote na wakijikimu pasi kiasi!?

Sasa Taifa lipi katika dunia hii ambalo lili-practice Slavery khalaf wakti huo huo pakawa na social intergration/fair proportion of equality to that extent and/or degree!?

Wewe unafahamu pale Amerika au Biritish Colonies ilichukua miaka mingapi hata Blacks kuanza kuruhusiwa labda japo kumtazama/kumtongoza Mwanamwari wa Kizungu!?...hata baada ya kufanza zile propagandas zao za kujitangazia ati wao Western World ati ndo walokataza/walositisha majambo/uharami wa ile Slave Trade!?

Mkuu...fahamu yakuwa hapa hakuna hata mmoja anayetetea Waarabu kama nao walifanza uharamia wa aina yoyote kwa Bin-Adam wenzao!? Hasha abadan!

Hakuna asilan mwenye kupinga yakuwa Zanzibar ilikua ni Slave Market kubwa mno!...lakini hii nayo pia ni Topic nyangine kubwa mno na pana saana! Maana italazim tuchambue kiundani hao wanunuzi wakubwa/maarufu wa Slaves walikua akina nani/mataifa yao,athari za huko waliokokamatwa/kununuliwa na jamii zake,hao wanunuzi walikua ni akina nani,wapi walipelekwa hao Slaves kwa wingi mno,mataifa/maharamia wapi ndo pia walofaidika na huo ushuru wa Watumwa kwenye ile Zanzibar Slave Market,na mabo mangine mangi pita kiasi!

Kinachotatiza kiduchu hapa ni;your unfair potrayal of Zanzibar society during those times and its Arabs Rulers,Ok!?

Ahsanta.
 
Nimepitia hizi bayana zako Pasco kwa faida ya wanaukumbi na wale wote wanaofuatilia huu mnakasha ungetufahamisha hizi habari umezipata wapi kuna kitabu umekisoma au kuna mtu amekuadithia.
Tujuze ili tufyonze Ilm.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…