Mkuu Maalim Mohamed Said, ni kweli uwanja unachafuka,
Mimi Pasco nimewakosea adabu wapi?, au kumpenda binti wa Kiarabu huko Zanzibar ni kosa?, nimesema sikuweza kumuoa kwani nilisema tumefanya kitu chochote?!. Au huko ukipenda ndio umemaliza kila kitu?!.
Sasa kuanza kutukana watu kunatoka wapi?, mimi kama muanzisha mada, kutikanwa halali yangu, nitukanwe wanavyotaka!, kisha ameletwa Nyerere katukanwa!, ameletwa mke wangu, katukanwa, wameletwa mapadri wametukanwa!, na kuna mtu kamleta hadi Mtume (SAW) na katukanwa!. Huku tunakokwenda sasa siko!. Kama hivi tuu ndio series ya kwanza!, jee niilete ya pili?!, naombo utumie ukubwa dawa wako kuwadhibiti vijana wako, naamin i watakusikiliza na mimi nitawadhibiti wale ninaowamudu tuumalize huu mnakasha kwa amani niufungue wa pili, huko ndiko hswa wewe unakohitajika!. Tukiona inashindikana hawadhibitiki, then nitamshauri Mode, tuufunge, niufungue ule wa pili!.
Tafadhali sana!, ila kwa wale wanaijisikia raha kunitukana mimi Pasco wa JF, nitukaneni mpaka mwisho wa raha zenu, ila msinitukanie, wala msiwatukane wengine wowote wasio husika!.
Binafsi, sitatizwi kabisa na kutukanwa hata nitukanajwe kwa sababu najua fika kuna watu wana laana!. Na kila siku huwa nasisitiza humu, kuwa kichaa sio mpaka mtu aokote makopo!, tunavichaa wengi humu kuliko tunavyojinua!.
Pasco.