mjukuu2009
Member
- Jul 6, 2009
- 89
- 4
Bei ya mkate yapunguzwa Msumbiji
Msumbiji
Msumbiji itabadilisha ongezeko la bei ya mikate iliyosababisha kuibuka kwa ghasia wiki iliyopita.
Tangazo la kubadilisha sera zimetolewa na waziri wa mipango, Aiuba Cuereneia, ambaye amesema pia kwamba nchi hiyo itarejesha baadhi ya ruzuku ya umeme na maji.
Ongezeko la bei ya vyakula na bidhaa nyingine zilisababisha maandamano ya siku tatu.
Serikali ilisema zaidi ya watu 400 walikamatwa wakati wa maandamano hayo, iliyosababisha watu 13 kufariki dunia.
Taarifa ya waziri ilisema kwamba serikali " itaendelea kuuza mkate kwa bei ya awali huku wakipanga ruzuku."
Awali serikali ya Msumbiji ilisema ongezeko la bei "haibadiliki".
Kuweka bei ndogo ya bidhaa nchini humo ni ngumu kwani kiwango kikubwa cha chakula chao hutoka nchi za nje.
Taifa hilo lililopo kusini mashariki mwa bara la Afrika linazalisha asilimia 30 tu ya ngano inayohitaji.
Ongezeko kubwa la bei ya vyakula lilisababishwa kwa upande mmoja na thamani ya pesa ya Msumbiji dhidi ya randi ya Afrika Kusini, ambapo wachambuzi wanasema bidhaa kutoka nje zinazidi kuwa ghali.
Pamoja na hayo, bei ya ngano imeongezeka kufuatia ukame nchini Urusi, muuzaji mkuu wa ngano duniani.
BBC Swahili - Habari - Bei ya mkate yapunguzwa Msumbiji
Angalizo;
Kwanini sisi watanzania atuonyeshi kushituka kila siku bei ya mafuta,soda,beer,ngano vinapanda lakini sisi wala atujigusi hivi sisi tumelogwa au tuna matatizo ya akili?
kama wenzetu mkate unapanda sisi je kila kitu kinapanda tumeka kimya utafikiri atuvitumi hivyo vitu,kama tumeshindwa basi tuondoe huu utawala wa majambazi.
Tumeluwa tukiongozwa na majambazi kwa miaka 50 kila kitu kinazidi kuwa juu tokea nimezaliwa sasa miaka 30 sijawai kusikia bei ya kitu ikishuka apa Tanzania,tumpe kura Dk.Slaa angalau tushuhudie bei ya vitu muhimu ikishuka kwa wengi wetu itakuwa ni neema kubwa.Miaka 50 ya utawala ccm imesha expire tumpe Dk.Slaa ilitu renew nchi yetu jamani tupate tanzania mpya yenye mtazamo mpya ccm haiwezi imesha shindwa kwa miaka 50 kwaiyo ata wakipewa madaraka awataweza tena,nasikitika sana ninaposoma na kuambiwa uchumi wetu ulikuwa sawa na Singapore miaka ya 60,70 sasa hivi ata Rwanda waliopigana miaka mingi wanatushinda aibu gani hii.