Miaka 6 ya Utetezi wa Wananchi: Happy Birthday ACT Wazalendo 5-5-2020

Miaka 6 ya majaribu mengi katika maisha yetu ya kila siku, Watanzania. ACT Wazalendo tumekuwa upande wa Wananchi muda wote, wakati wote bila kujali ‘Consequences’.
  • Tumekuwa na Wazanzibari walipoporwa haki yao ya kuchagua Kiongozi wanayemtaka!
  • Tumekuwa na Wakulima wa Mbaazi, Korosho, Pamba, Tumbaku na Karafuu walipoharibiwa masoko ya Bidhaa zao na kudhulimiwa Fedha zao zinazotokana na jasho lao.
  • Tumekuwa na Wavuvi wa Baharini na Ziwani - walipochomewa nyavu zao na kuharibiwa maisha yao
  • Tumekuwa na Wafugaji walipovamiwa kuondolewa eneo la malisho ya Mifugo yao.
  • Tumekuwa na Wafanyabiashara wanabambikiwa Kodi kubwa, kutolipwa Fedha zao za marejesho na kufunguliwa kesi za utakatishaji
  • Tumekuwa na Wanaharakati wa Haki za Binaadamu na Waandishi wa Habari wanapobambikiwa kesi na kuwekwa jela, kutekwa, kupotea na hata kuuawa.
  • Tumesimamia Uhuru wa Taasisi za Uwajibikaji kama CAG na kuhakikisha Katiba ya Tanzania inalindwa na kuheshimiwa
  • Tumekuwa na Wanasiasa wenzetu wanapoonewa na kunyimwa haki zao bila kujali Vyama vyao.
  • Tumekuwa na Wananchi kuwaelemisha kujikinga na virusi vya Korona ili kuzuia vifo vya Watu wetu na kuiwajibisha Serikali kwa kushindwa kuongoza vyema Vita dhidi ya Ugonjwa wa COVID 19.
Kila mwenye kuonewa, kudhulumiwa na kukandamizwa anasikia sauti ya ACT Wazalendo bila kujali chama chake, Dini yake, kabila lake wala hali yake. Hakika, ULIPO TUPO!

ACT Wazalendo ni chama cha Watu. Ni Chama chako. Ni chama chenu. Ni chama chetu. Leo kimetimiza miaka 6 tangu kusajiliwa kwake hapo tarehe 5-5-2014.

ACT Wazalendo itaendelea kuwa upande wa Wananchi. Ninaomba tuendelee kwa MSHIKAMANO kupigania Uchaguzi Huru, wa Haki na unaoaminika. Ninaowaomba muipe dhamana ACT Wazalendo ili ijenge Tanzania yenye Watu wenye Raha na Furaha #KaziNaBata

Zitto Kabwe
Kiongozi ACT Wazalendo
May 5, 2020.
We mnafiki sana Zitto huwa nakuangalia tu, ilaunajua ulichokifanya awamu ya nne, sasa wizi wa namna ile umekomeshwa unabaki kutapatapa na wanawake zako wakiongozwa na (Mo...sa Malapa)
 
Yule sufiani umemchinjia mbali maana chama ni cha waha tu kina Nondo

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiki ni chama cha Watanzania wa Bara na Visiwani
Mimi najivunia Kuwa ACT wazalendo na Mimi ni Mtanzania kutokea Zanzibar
Hngera Kiongozi Mkuu Zuberi Kabwe
Hongera Mwenyekiti wa chama Maalim Seif Sharif Hamad.
Iwe tena miaka 6 na kumi na ishirini na Iwe mwaka huu wa Kushika Dola Tanzania Nzima
Amin
 
Waha na Wapemba ni chama cha kibaguzi .Hata yule Maganja wamemuondoa kwa maslahi yao ya kinafiki sasa hivi wanajulikana kama islamic brotherhood of Tanzania.
Wagonjwa wengi sana humu Jf.

Bado wana mawazo ya udini udini kwa kuanngalia majina ya watu?,
UONGOZI WA CCM.jpg

Mbona Chama hicki hamusemi kuwa kina Udini? kwa kuwa Viongozi wake 80% ni wa majina ya Kikiristo?
Mbona chadema 90% ni wakiriso ,hakisemwi, au kosa udini ni kuwa na majina ya kiislamu tuu?
Pelekeni note basi kwa Msajili mumlaumu kwa kutokutimiza wajibu wake.
Kama nyerere angelikuwa hai ange sema PuMbaFU zenu.
 
Wagonjwa wengi sana humu Jf.

Bado wana mawazo ya udini udini kwa kuanngalia majina ya watu?,
View attachment 1440479
Mbona Chama hicki hamusemi kuwa kina Udini? kwa kuwa Viongozi wake 80% ni wa majina ya Kikiristo?
Mbona chadema 90% ni wakiriso ,hakisemwi, au kosa udini ni kuwa na majina ya kiislamu tuu?
Pelekeni note basi kwa Msajili mumlaumu kwa kutokutimiza wajibu wake.
Kama nyerere angelikuwa hai ange sema PuMbaFU zenu.
Wewe mwenyewe unahisi ni 80% lakina chama chenu umekiri ni 100% . Islamic brotherhood of Tanzania.
 
Miaka 6 ya majaribu mengi katika maisha yetu ya kila siku, Watanzania. ACT Wazalendo tumekuwa upande wa Wananchi muda wote, wakati wote bila kujali ‘Consequences’.
  • Tumekuwa na Wazanzibari walipoporwa haki yao ya kuchagua Kiongozi wanayemtaka!
  • Tumekuwa na Wakulima wa Mbaazi, Korosho, Pamba, Tumbaku na Karafuu walipoharibiwa masoko ya Bidhaa zao na kudhulimiwa Fedha zao zinazotokana na jasho lao.
  • Tumekuwa na Wavuvi wa Baharini na Ziwani - walipochomewa nyavu zao na kuharibiwa maisha yao
  • Tumekuwa na Wafugaji walipovamiwa kuondolewa eneo la malisho ya Mifugo yao.
  • Tumekuwa na Wafanyabiashara wanabambikiwa Kodi kubwa, kutolipwa Fedha zao za marejesho na kufunguliwa kesi za utakatishaji
  • Tumekuwa na Wanaharakati wa Haki za Binaadamu na Waandishi wa Habari wanapobambikiwa kesi na kuwekwa jela, kutekwa, kupotea na hata kuuawa.
  • Tumesimamia Uhuru wa Taasisi za Uwajibikaji kama CAG na kuhakikisha Katiba ya Tanzania inalindwa na kuheshimiwa
  • Tumekuwa na Wanasiasa wenzetu wanapoonewa na kunyimwa haki zao bila kujali Vyama vyao.
  • Tumekuwa na Wananchi kuwaelemisha kujikinga na virusi vya Korona ili kuzuia vifo vya Watu wetu na kuiwajibisha Serikali kwa kushindwa kuongoza vyema Vita dhidi ya Ugonjwa wa COVID 19.
Kila mwenye kuonewa, kudhulumiwa na kukandamizwa anasikia sauti ya ACT Wazalendo bila kujali chama chake, Dini yake, kabila lake wala hali yake. Hakika, ULIPO TUPO!

ACT Wazalendo ni chama cha Watu. Ni Chama chako. Ni chama chenu. Ni chama chetu. Leo kimetimiza miaka 6 tangu kusajiliwa kwake hapo tarehe 5-5-2014.

ACT Wazalendo itaendelea kuwa upande wa Wananchi. Ninaomba tuendelee kwa MSHIKAMANO kupigania Uchaguzi Huru, wa Haki na unaoaminika. Ninaowaomba muipe dhamana ACT Wazalendo ili ijenge Tanzania yenye Watu wenye Raha na Furaha #KaziNaBata

Zitto Kabwe
Kiongozi ACT Wazalendo
May 5, 2020.
Zitto kila kitu unafanya mwenyewe
 
Back
Top Bottom