Tatizo la nchi hii sio CCM mleta mada bali ni aina ya watu wanaopatikana katika hii nchi ndo tatizo. CCM kama chama hakikujiumba kilianzishwa na watu kama mimi na wewe, kanuni, taratibu na miongozo yote ilioko CCM iliwekwa na watu wanaopatikana katika nchi hii. Watu walioko CCM ambao wengine walishafariki na wengine kuzaliwa ndo hawahawa watu wanaopatikana katika vyama vingine kama CHADEMA, ACT ,CUF nk. Jamani si kuna wimbi la watu walitoka vyama vya upinzani kwenda CCM na wengine walitoka CCM kwenda upinzani lakini hakuna kilichobadilika coz tatizo la msingi ni lilelile(WATU).
Mbuzi hata ukimvisha tai na suti kutoka brand maarufu na ghali duniani ataendelea kuwa mbuzi tu.
TATIZO KUBWA NI CCM, period. Si vizuri wala si haki kuwabeza Watanzania kiasi ulichoandika hapa.
Watu wenye akili, wenye weledi mkubwa katika fani mbali mbali, wenye maadili, wenye utimilifu (integrity), wapo Tanzania tena wengi kama ilivyo sehemu nyingine duniani. Wako watanzania wanafanya kazi za kutukuka nje ya nchi. Walipokuwa hapa nchini hawakutambulika wala kuthaminiwa. Wengine walifanyiwa visa hadi wakaachia ngazi.
Utawala wa CCM umetengeneza mazingira ya kutumikia na kunyenyekea viongozi wa nchi (
subservience) kama kigezo kikubwa cha kupewa fursa na kufanikiwa kazini. Taaluma, utendaji maadili, havithaminiwi kabisa. Mafanikio ya mwajiriwa ni jinsi atakavyojikomba na kufanikisha malengo ya wakubwa hata kwa kuvunja sheria.
Huo mfumo umewatupa nje wenye uwezo wengi na wengine kuwalazimisha kuwa vilaza na machawa ili kufurahisha waliowateua.
Effects zinaonekana. Angalia watu kama Prof. Kabudi, Prof. Mruma, Dr. Mwakyembe, Polepole, etc. walivyopitia mabadiliko ya kushangaza chini ya viongozi wa CCM. IPO mifano mingi tu katika ngazi zote za serikali. Ni
domino effect ya uchawa iliyotamalaki nchini.
Weledi wamebakia kuugua tu wanapoona nchi inavyohujumiwa na
idiots. Halafu anatokea mtu anawafunika wote na blanketi la IDIOCY. That’s grossly unfair!