Miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika 1961: Historia ya wapigania uhuru haifahamiki

Miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika 1961: Historia ya wapigania uhuru haifahamiki

1639887808541.png

Kulia Bi. Chiku bint Said Kisusa (Mama Sakina), Bi. Titi Mohamed, kushoto wa mwanzo Bi. Tatu bint Mzee
 
Jambo jema sana mleta mada mohamed saidi kutukumbusha kuhusu historia ya Tanzania.
Waandishi wengi wa historia ya Tanzania wamekuwa wakiandika yale tu yaliyofurahisha utawala badala ya kujikita zaidi kwenye historia halisi ya Tanzania.
Na kutokana na kuwa na viongozi/wataalam wenye hulka ya kujipendekeza kwa Utawala,wamekuwa wakiandaa mitaala iliyokuwa ikipendelea/kuwatukuza Utawala hivyo kupoteza historia ya wachangiaji wengine katika maendeleo ya nchi yetu.
Mfano mzuri Mr.JPM kabla hajafa alitaka kubadili mitaala ili kufundishwe historia ya Tanzania mashuleni kwenye ngazi zote.Ambapo japo vitabu havikufika/havikutoka sokoni lakini inasadikika ilikuwa na mrengo wa kumsifia yeye...nachelea kusema hata JK Nyerere naye alitengeneza mazingira ya yeye pekee kuonekana ndio aliyepigania uhuru na wengine kawa dis
 
Jambo jema sana mleta mada mohamed saidi kutukumbusha kuhusu historia ya Tanzania.
Waandishi wengi wa historia ya Tanzania wamekuwa wakiandika yale tu yaliyofurahisha utawala badala ya kujikita zaidi kwenye historia halisi ya Tanzania.
Na kutokana na kuwa na viongozi/wataalam wenye hulka ya kujipendekeza kwa uongozi,wamekuwa wakiandaa mitaala iliyokuwa ikipendelea/kuwatukuza viongozi hivyo kupoteza historia ya wachangiaji wengine katika maendeleo ya nchi yetu.
Mzee haandiki wala kusimulia kuhusu historia ya Tanzania. Yeye yuko busy kufuatilia na kuandika kuhusu Wazee wake wa Kiislamu.

Ninyi mnaosema anaandika historia ya Tanzania ndio mnamchanganya.

Yeye anaokoteza hapa na pale majina ya wazee wake wa kiislam ambao hata kwa namna moja au nyingine waliwahi kumpa Nyerere maji ya kunywa, inatosha.
 
We mzee unawashwa sana,uko vizuri kwenye kutupa history ukiingiza siasa unaharibu.
Base on one thing ,history or politic.
Utaundiwa zengwe hapo ushangae
Babu...
Niandikie kistaarabu mimi mzee nakimbilia miaka 70 si adabu kuniita, 'We,'' na kuniambia "nawashwa," hilo ni tusi kubwa.

Kunitukana mimi ni sawa na kumtukana baba au mama yako.

Kama kuwashwa basi nimewashwa kwa miaka mingi sana maana nimeandika vitabu 10 na makala wala sijui hesabu yake.

Search hapa JF utazikuta.
Sasa hivyo vitisho vya nini?

Nani nchi hii umesikia kaadhibiwa kwa kuandika historia?

Mbona haya ninayoandika hapa yamo kwenye maandishi yangu mengi sasa zaidi ya miaka 40?
 
Mzee haandiki wala kusimulia kuhusu historia ya Tanzania. Yeye yuko busy kufuatilia na kuandika kuhusu Wazee wake wa Kiislamu.

Ninyi mnaosema anaandika historia ya Tanzania ndio mnamchanganya.

Yeye anaokoteza hapa na pale majina ya wazee wake wa kiislam ambao hata kwa namna moja au nyingine waliwahi kumpa Nyerere maji ya kunywa, inatosha.
Jaribu kutofautisha historia na siasa uweze kuwa na uwanja mpana zaidi wa fikra.
 
Mkaruka,
Siokotezi.

Mengi na muhimu niliyoandika ni historia ya wazee wangu kwa hiyo nayafahamu.

Vilevile nimefanya utafiti mwingi.
Nimeshiriki katika tafiti kubwa nne.

Utafiti wa kwanza nilipokuwa naandika historia ya TANU nikitumia Nyaraka za Sykes.

Kitabu hiki ni maarufu kimechapwa mara nne toka 1998 kilipochapwa kwa mara ya kwanza London.

Utafiti wa pili kuandika vitabu vya kufundisha Kiingereza na Historia shule za Msingi mradi wa Oxford University Press Nairobi.

Utafiti wa tatu nilishiriki kama Research Assistant wa Dr. Harith Ghassany wakati anatafiti historia ya mapinduzi ya Zanzibar na akaandika kitabu "Kwaheri Uhuru Kwaheri Ukoloni."

Utafiti wa nne nilishiriki kuandika Dictionary of African Biography (DAB) mradi wa Harvard na Oxford University Press New York.

Toa hofu mimi si muokotezaji ni mtafiti.

Kuhusu Waislam katika historia ya uhuru wa Tanganyika nipe ushauri vipi tufute mchango wao.

Wajaluo Kenya hawawapendi Wakikuyu na ndiyo walio na elimu kubwa lakini wameshindwa kufuta mchango wa Wakikuyu katika kupigania uhuru wa Kenya.
 
Jaribu kutofautisha historia na siasa uweze kuwa na uwanja mpana zaidi wa fikra.
Msingida,
Specialisation yangu ni political history.
Nimesoma vyote na niandika vyote.

Ingia: mohamedsaidsalum.blogspot.com
 
Mzee haandiki wala kusimulia kuhusu historia ya Tanzania. Yeye yuko busy kufuatilia na kuandika kuhusu Wazee wake wa Kiislamu.

Ninyi mnaosema anaandika historia ya Tanzania ndio mnamchanganya.

Yeye anaokoteza hapa na pale majina ya wazee wake wa kiislam ambao hata kwa namna moja au nyingine waliwahi kumpa Nyerere maji ya kunywa, inatosha.

Mzee ni mdini na mzandiki
 
Rudia kusoma uelewe. Kama huna fikra za kuelewa acha.
Mkaruka,
Hakuna sababu ya kukasirika ikiwa unaniona ni mzito wa kuelewa nihurumie tu.

Soma "In Search of Excellence," kitabu cha Peters and Waterman,'' wana kitu wanaita "stick to knitting."
 
Idugunde,
Wapo watu wameelimika sana kwa juhudi zangu za kusahihisha historia ya Tanganyika.

Huu si udini wala uzandiki.
Kusahihisha historia ya Tanganyika sio kuangalia upande mmoja wa shilingi. Kwani hili taifa ni waislamu pekee ndio walipigania uhuru wa Tanganyika? Mbona unataka kuaminisha umma kuwa ni akina Sykes na waislamu ndio walikuwa na mchango mkubwa kudai uhuru.
 
Babu...
Niandikie kistaarabu mimi mzee nakimbilia miaka 70 si adabu kuniita, 'We,'' na kuniambia "nawashwa," hilo ni tusi kubwa.

Kunitukana mimi ni sawa na kumtukana baba au mama yako.

Kama kuwashwa basi nimewashwa kwa miaka mingi sana maana nimeandika vitabu 10 na makala wala sijui hesabu yake.

Search hapa JF utazikuta.
Sasa hivyo vitisho vya nini?

Nani nchi hii umesikia kaadhibiwa kwa kuandika historia?

Mbona haya ninayoandika hapa yamo kwenye maandishi yangu mengi sasa zaidi ya miaka 40?
Huwa unajisifu kwamba umesomesha historia ya kweli na kwamba sasa watu wameifahamu hiyo historia. Sasa mbona unarudia rudia yale yale? Mbona kwenye title ya hii thread, umeandika kuwa historia hiyo haifahamiki?

Juhudi zako za kufanya waislam wajisikie wanyonge na wawachukie wasio waislam, ZIMEFELI NA ZITAENDELEA KUFELI.
 
Back
Top Bottom