Hili swala la udini linatoka wapi?. Maswali muhimu ya kujiuliza.
Uhuru ulipiganiwa na wakristo pekee?. Ili wakristo peke yao wawe huru
Uhuru ulipiganiwa na waislamu ili waislamu wawe huru pekee wenyewe na wengine wawe bado chini ya mkoloni?.
Swali hilihili kwa dini nyingine nazo?..
Mleta uzi kwani ame-aknowledge kwamba hawa ndio waislam walioshiriki kupigania uhuru??.. Kama Jibu ni hapana basi haipaswi kubezana kwa mitazamo na fikra za uelewa(Perception and understanding).
Kama kuna mtu ataliona hili kwa angle ya udini, Basi kuna mwingine atakuja kwa angle ya ukabila. Mzanaki atamwambia Muha nilikuletea uhuru, vivyohivyo na makabila mengine.
The Chosen 1,
Mimi nimetafiti historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika na kuna mengi nimeyaona na nimetaka kujua sababu yake ni nini?
Nimejiuliza kwa nini waliokuja kuandika historia ya TANU na uhuru walifuta majina ya watu muhimu sana katika harakati zile?
Nikapata majibu.
Kwa nini Waislam walikuwa mstari wa mbele katika kupigania uhuru wa Tanganyika?
Nikapata majibu.
Kwa nini Wamanyema walikuwa mstari wa mbele katika TANU?
Nikapata majibu.
Kwa nini leo inapoandikwa historia ya kweli kuna watu wanaumia sana na wengine kufika hata kunitukana matusi?
Nini kinachowaghadhibisha?
Hawapendi kusikia neno Uislam ukinasibishwa na harakati za uhuru?
Kwa nini?
Je hii ndiyo sababu ya kuibadili historia?
Sasa hakuna Mzanaki anaeweza kusema kuwa kaleta uhuru wala hakuna mtu mmoja au kabila moja linaloweza kuja na madai haya.
Ila ipo historia ya watu na makabila ambayo yalijipembua katika harakati hizi kiasi mtafiti makini atagundua na ikiwa ataandika ataeleza.
Haya mambo si ya leo.
Ukisoma historia ya Kleist Sykes: ''Kleist Sykes The Townsman,'' (1968) anasema kuwa wenyeji wa Dar es Salaam yaani Wazaramo, Wangindo, Warufiji na makabila mengine ya pembezoni ambao walikuwa wengi hapo mjini wakiwaita Wazulu, Wamanyema, Wanubi, ''Watu wa kuja,'' na wakiwaambia wanajitia kimbelembele sana katika siasa na mambo yote ya jamii.
(Katika hawa, ''watu wa kuja,'' ni babu yangu Salum Abdallah muasisi wa TANU Tabora na muasisi wa Tanganyika Railways African Union (TRAU) 1955).
Ukienda African Asociation utawakuta akina Kleist na Mzee bin Sudi hawa Wazulu na Wamanyema, Maulidi Commitee Wazulu, Wamanyema na Wanubi wako akina Kleist, Ibrahim Hamisi na Mzee bin Sudi.
Ukienda Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika utamkuta President Mzee bin Sudi na Secretary Kleist Sykes.
Kila mahali wanachukua nafasi za uongozi.
Ukienda Yanga Afrika utamkuta Hassan Machakaomo, Mzulu kizazi cha kwanza kuzaliwa Tanganyika.
Hii ikiwaudhi sana wenye mji wao wazawa ingawa na hawa, ''watu wakuja,'' wamezaliwa Dar es kizazi cha pili cha Wazulu, Wamanyema na Wanubi kutoka Mozambique, Belgian Congo na Sudan.
Nenda Tabora 1948 wanaunda TAA uongozi na uanachama umeshikwa na Wamanyema akina Abdallah na Maulidi Kivuruga.
Shida kukuta Mmanyema Mkristo na vitu kama hivi ndivyo vilivyotawala historia ya TANU na harakati za kudai uhuru.
Ukijaribu kuukwepa ukweli huu na ukaandika historia kwa msukumo wa nafsi yako na si kwa ukweli wa hali halisi balaa lake kubwa pale anapotokea mtafiti akaandika ukweli kama ulivyokuwa.
Hiki ndicho kilichoipata historia ya Kivukoni.
Ndiyo maana leo tunaisoma upya historia ya TANU na harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.
Ndiyo maana hii leo tunaisoma upya historia ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Angalia hiyo picha hapo chini hii ni 1955/56 wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.
Ukisoma historia za hawa watu ndipo utawathamini wazalendo hawa.
Wote hawa historia zao zimo katika kitabu cha Abdul Sykes.
Nikisema niweke links zote mtachoka kusoma.
Haruna Taratibu muasisi wa TANU Dodoma, Saadan Abdul Kandoro muasisi wa TANU Kanda ya Ziwa, Sheikh Mohamed Ramia muasisi wa TANU Bagamoyo na Iddi Faiz Mafungo yeye alikuwa Mweka Hazina wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na Mweka Hazina wa TANU na yeye ndiye aliyekuwa mkusanyaji wa fedha za safari ya Nyerere UNO 1955.
Historia yake ni ya kusisimua sana.
Lakini Sheikh Mohamed Ramia yeye kaandikwa kwa kirefu na August Nimtz, ''Islam na Politics in East Africa.''
Kulia ni Haruna Taratibu (Mmanyema), Saadan Abdu Kandoro (Mmanyema), Julius Nyerere (Mzanaki), Sheikh Mohamed Ramia (Mmanyema) na Iddi Faiz Mafungo (Mmanyema).
Iddi Faiz Mafongo TANU Card No. 24 Iddi Tosiri TANU Card No. 25 Ndugu Wawili Katika Kupigania Uhuru wa Tanganyika, 1954 ushoto K...
mohamedsaidsalum.blogspot.com
Kushoto: Iddi Faiz Mafungo, Sheikh Mohamed Ramia, Julius Nyerere, Saaadan Abdu Kandoro na Haruna Taratibu Katika TAA kulikuwa na mtu ...
mohamedsaidsalum.blogspot.com
kashata said: ↑ Mzee Muhammed nimekupata juu ya lengo la uzi wako ni kuonyesha ulimwengu mchango wa akina sykes ktk kupigania u...
mohamedsaidsalum.blogspot.com