Mwaka wa pili sasa; tunaendelea kusubiri.
Gagnija,
Unataka kujua yaliyomkuta Prof. Malima?
Katika kitabu cha Abdul Sykes nimeweka tabaruku hiyo hapo chini:
‘’Nakitoa kitabu hiki kwa Profesa Kighoma Ali Malima (1938-1995) ambae akiwa kijana mdogo anapata miaka 19 na hali akiwa mwanafunzi hodari, alikatisha masomo yake Shule ya Sekondari Tabora ili ajiunge na TANU katika harakati za kuikomboa Tanganyika kutoka katika utumwa wa ukoloni wa Waingereza.
Alipotambua kuwa baada ya miaka mingi ya uhuru, kuna jamii moja kwa njama na hila ilikuwa imejenga himaya ya utawala wao ndani ya chama na serikali, utawala uliokuwa na chuki kwa Waislam na Uislam alijitokeza kupinga dhulma hii.
Chama tawala na serikali kikajenga uadui dhidi ya Profesa Malima kwa sababu ya msimamo wake huo.
Profesa Malima hakutikisika.
Aliendelea kudai haki kwa bidii, kwanza akiwa ndani ya chama na serikali yake na baadae akajiuzulu ili kuongoza chama cha upinzani, National Reconstruction Alliance (NRA) na akasimama kugombea uchaguzi wa rais wa nchi ili arudishe haki na usawa kwa raia wote.
Wakati Waislam wanajiandaa kumuunga mkono Profesa Malima kama vile walivyomuunga mkono Julius Nyerere wakati wa kudai uhuru, Profesa Malima akakumbwa na umauti ghafla na kwa njia za kutatanisha tarehe 5 Agosti, 1995 akiwa London (akitokea Maka alikokwenda kufanya umra), siku chache baada ya yeye kutangaza azma yake ya kugombea urais wa Tanzania katika mkutano wa hadhara mjini Tabora.
Daima nitaenzi na kukumbuka ucheshi na kipaji cha hali ya juu cha usomi cha Profesa Malima nilichoshuhudia katika mazungumzo yetu katika siku za mwisho za uhai wake; tukitafakari kuhusu hatma ya nchi yetu.
Kwa kumbukumbu ya Profesa Malima katika kuhisi kwake janga litakaloikumba nchi yetu katika siku za baadae na katika kuenzi ushujaa wake wa kuliweka wazi tatizo nyeti la Uislam na katika kulikumbusha taifa maadili yake na katika bidii yake ya kuurejesha uongozi katika mstari wa haki na usawa kwa raia wote nakitoa kitabu hiki kwake.''
Mohamed Said
Dar es Salaam