Miaka 61 bila huduma ya maji Dar es Salaam

Kipindi stendi kuu ya mabasi Mbezi inafunguliwa na mzalendo namba moja wa karne ya 21 Mh dk John Pombe Joseph Magufuli alitoa maelekezo ya kwamba barabara kutokea stendi hiyo kwenda mpigi magoe ianze kujengwa kwa kiwango cha lami pamoja na maji yapelekwe huko jimbo la kibamba lote

Na kweli kesho yake tu pilikapilika zikaanza.

Magari yakawa yanapishana tayari kwa ujenzi. Dawasa nao hawakuwa nyuma. Mabomba yakaanza kutandazwa sehemu mbali mbali za jimbo la kibamba kuelekea maeneo ya mbezi misumi,msakuzi na mpigi magoe ambako watu hawajawahi kuona maji toka Nchi ipate uhuru mwaka 1961.

Bahati mbaya haikuchukua mda mrefu mzalendo katutoka.zile shughuli zilizokuwa zinaendelea zikaanza mwendo wa kobe na hatimaye zikafa kabisa hadi leo watu wa kibamba maeneo ya Mpigi Magoe, Msakuzi na kwingineko huduma hizi wanazisikia tu. Inawalazimu kununua maji kwenye visima vya watu binafsi kwa unit shilingi 5000-6000 kwa usawa huu kweli?

Hivi ninyi viongozi mliopewa dhamana mnataka tuwasimamie kwa mijeredi ndo mpeleke hizo huduma? Kama pesa hazitoshi muuze hizo V8 zenu mnunue Vitz. Haiwezekani huduma hizo muhimu zikosekane ndani ya jiji la kibiashara Dar es Salaam. Wananchi tunataka maji, hatutaki V8.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tuko na Tanzania royal T ndugu na wengine tunakula kwa urefu wa kamba zetu hayo sio muhimu kwa sasa.
 
Siyo kila sehemu mkuu,area ninayoishi mimi maji yalikuwa yanatoka ni hujuma wanafanya wapemba na wachagha wenye vi-Canter vya maji ya madumu kuhonga engineers wa Dawasa wasifungue maji ili wao watuuzie na madumu yao machafu.

Nime-plan kuchimba kisima nivune maji ya mvua tu maana nchi hii hakuna mtetezi zaidi ya kuishi jinsi hali inavyotaka.
Wachaga huwa ni watu wabaya sana aisee, wana ukatili wa ajabu.
 
Mbunge wenu ni nani?
Mimi ni victim wa haya yote

Naishi Mbezi Makabe mwaka jana mwanzoni nilifunga bomba tena kwa gharama kubwa maji yakatoka kama miezi mitatu mfululizo kufika mwezi August ukaanza mgao hadi napoandika hapa maji hayatoki ukiuliza sababu kwanini hayatoki huambiwi wapumbavu Dawasa wamehongwa na wenye Canter za kuuza maji kwa madumu ili wauze maji,hilo la barabara hizo za jimbo la ubungo stuff wa halmashauri kupitia TARURA na TANROAD ndo wanakopigia hela.

Tujiulize,leo TMA wakitoa utabiri wa kunyesha mvua kubwa Dar kesho grader zinaingia site kuchonga barabara ikija kunyesha hiyo mvua barabara zote zinavurugika so wanakuwa wanajua kabisa awamu hii ya mvua tukichonga barabara hii mpaka mvua ije kukata itakuwa haifai tena so tumeshachukua fungu tukae tena tukisubiri msimu unaokuja kama wana nia nzuri kwanini wasizichonge kipindi hiki cha kiangazi?

Mbunge amekaa kimya hatumsikii hata akikohoa huko bungeni angalao angezungumzia hili la wizi wa pesa za umma kuchonga barabara zinazoharibika hata vifaa vya kazi havijatoka site.
 
Huku wilaya ya chalinze walikuwa na CHALIWASA wakaivunja CHALIWASA wakaiweka pamoja na DAWASA tangu iwe chini ya DAWASA maji hayajawahi kutoka hadi leo
 
Maisha ya mtanzania ni taabu na mateso mpaka mwisho wetu

Haikuwa na haja ya late magu kuwaaambia nni cha kufanya la msingi ni kuwa na mpango mkakati wa muda mrefu na mfupi kwa ajili ya watanzania

Haina haja ya kutegemea hisani ya mtu wala matakwa binafsi zaidi ya kuwa na mpango mmaridhawa
Tatizo ni moja, siku zote Aliye shiba hamjui mwenye njaa !!
 
Miaka mitano ya kwanza hakuwaona? Nitajie nani alikuwa anaishi Mpigi miaka ya 1970 ili apelekewe maji na barabara.
 
Kipindi stendi kuu ya mabasi Mbezi inafunguliwa na mzalendo namba moja wa karne ya 21 Mh dk John Pombe Joseph Magufuli alitoa maelekezo ya kwamba barabara kutokea stendi hiyo kwenda mpigi magoe ianze kujengwa kwa kiwango cha lami pamoja na maji yapelekwe huko jimbo la kibamba lote

Na kweli kesho yake tu pilikapilika zikaanza.

Magari yakawa yanapishana tayari kwa ujenzi. Dawasa nao hawakuwa nyuma. Mabomba yakaanza kutandazwa sehemu mbali mbali za jimbo la kibamba kuelekea maeneo ya mbezi misumi,msakuzi na mpigi magoe ambako watu hawajawahi kuona maji toka Nchi ipate uhuru mwaka 1961.

Bahati mbaya haikuchukua mda mrefu mzalendo katutoka.zile shughuli zilizokuwa zinaendelea zikaanza mwendo wa kobe na hatimaye zikafa kabisa hadi leo watu wa kibamba maeneo ya Mpigi Magoe, Msakuzi na kwingineko huduma hizi wanazisikia tu. Inawalazimu kununua maji kwenye visima vya watu binafsi kwa unit shilingi 5000-6000 kwa usawa huu kweli?

Hivi ninyi viongozi mliopewa dhamana mnataka tuwasimamie kwa mijeredi ndo mpeleke hizo huduma? Kama pesa hazitoshi muuze hizo V8 zenu mnunue Vitz. Haiwezekani huduma hizo muhimu zikosekane ndani ya jiji la kibiashara Dar es Salaam. Wananchi tunataka maji, hatutaki V8.

Sent using Jamii Forums mobile app
Alikuwa mzalendo nyumbani kwako.

Sent from my TECNO-L8Plus using JamiiForums mobile app
 
Hizo v8 ni matakwa ya sheria ambazo magufuli alikuwepo bungeni kuzipitisha. Kuhusu hizo v8 anza kumlaumu magufuli.
Kwa kweli hayo mavieite yanavyopishana halafu tunasema eti nchi ni masikini kila mwenye akili anatushangaa !! " Land Cruiser hardtop ndio gari zinazofaa kwa sababu hata kwenye barabara za tope zenyewe zinapita tu !! LA sivyo msituambie nchi yetu ni masikini !!
 
Huku wilaya ya chalinze walikuwa na CHALIWASA wakaivunja CHALIWASA wakaiweka pamoja na DAWASA tangu iwe chini ya DAWASA maji hayajawahi kutoka hadi leo
Hahahaaa pole mkuu...
Naona imekuwa tofauti.
Maeneo ninayoishi mimi tangu waanze DAWASA ndio tumeanza kupata maji,enzi za Chaliwasa ilikuwa unaweza kukaa hata miezi 6 bomba halitoi maji.
Hivi asubuhi hii nimetoka kukinga maji bombani kwenda kuoga[emoji23]
 
Mbunge wenu ni nani?
Jumanne Mtemvu yule jamaa aliyemuomba Magufuli hizi huduma siku ya uzinduzi wa stand ya mkoa pale Mbezi.

Simsikii tena akipiga chapuo hadi kuna wakati huwa nahisi nae anafaidika na hizi hujuma.
 
Kipindi stendi kuu ya mabasi Mbezi inafunguliwa na mzalendo namba moja wa karne ya 21 Mh dk John Pombe Joseph Magufuli alitoa maelekezo ya kwamba barabara kutokea stendi hiyo kwenda mpigi magoe ianze kujengwa kwa kiwango cha lami pamoja na maji yapelekwe huko jimbo la kibamba lote

Na kweli kesho yake tu pilikapilika zikaanza.

Magari yakawa yanapishana tayari kwa ujenzi. Dawasa nao hawakuwa nyuma. Mabomba yakaanza kutandazwa sehemu mbali mbali za jimbo la kibamba kuelekea maeneo ya mbezi misumi,msakuzi na mpigi magoe ambako watu hawajawahi kuona maji toka Nchi ipate uhuru mwaka 1961.

Bahati mbaya haikuchukua mda mrefu mzalendo katutoka.zile shughuli zilizokuwa zinaendelea zikaanza mwendo wa kobe na hatimaye zikafa kabisa hadi leo watu wa kibamba maeneo ya Mpigi Magoe, Msakuzi na kwingineko huduma hizi wanazisikia tu. Inawalazimu kununua maji kwenye visima vya watu binafsi kwa unit shilingi 5000-6000 kwa usawa huu kweli?

Hivi ninyi viongozi mliopewa dhamana mnataka tuwasimamie kwa mijeredi ndo mpeleke hizo huduma? Kama pesa hazitoshi muuze hizo V8 zenu mnunue Vitz. Haiwezekani huduma hizo muhimu zikosekane ndani ya jiji la kibiashara Dar es Salaam. Wananchi tunataka maji, hatutaki V8.

Sent using Jamii Forums mobile app
Una Nia nzuri ya kuweka mada ya mahitaji ya maji lakini uwasikishaji wako una mapungufu. Kwamba eneo la Mbezi Stendi ya Magufuli hakuna maji kuanzia mwaka 1961 tulipopata uhuru, Mimi nipo hapa Dar kuanzia 1979. Makazi ya Mnezi yalikuwa ni mapori tu kwenye miaka 1979
 
Nime-plan kuchimba kisima nivune maji ya mvua tu maana nchi hii hakuna mtetezi zaidi ya kuishi jinsi hali inavyotaka.
Naona kule mpiji ndio wameanza kupitisha mabomba...,, nna ka Ujenzi ka kibanda changu huko,, but visima vya watu binafsi now havitoi maji so tuliovuta ni kama tulipoteza tu pesa,,,na Serikali ndio ipo mwendo wa kobe sana...

But hizo barabara ndio changamoto,,,zinachongwa karibu kila mwezi,,,kila ninapopita kwenda site nakuta imechongwa,,na ikinyesha mvua hizo njia gari huwezi tembea hata speed 40km/h..

Hii Nchi ni kuishi kadri nguvu yako ilivo,,hakuna mtu atakutetea.
 
Huko hakufai kuishi mimi nimehama,nilikuwa na kajumba kangu Makabe kwa Moyo nimekimbia,Barabara Mbovu Maji hakuna,Mwaka jana huyo Aweso alikuja njiapanda Makabe akapigapiga tuneno na kusaini Vikaratasi na Wakandarasi wake mwaka umepita nikiuliza walioko huko wanasema Maji hakuna na Mbunge haonekani.
 
Hahahaaa pole mkuu...
Naona imekuwa tofauti.
Maeneo ninayoishi mimi tangu waanze DAWASA ndio tumeanza kupata maji,enzi za Chaliwasa ilikuwa unaweza kukaa hata miezi 6 bomba halitoi maji.
Hivi asubuhi hii nimetoka kukinga maji bombani kwenda kuoga[emoji23]
Ubena hapa nimekimbia nyumba yangu nimehamia Morogoro mjini
 
14 October 2022
Mivumoni, Madale
Tanzania

MIAKA KUMI HAWANA MAJI MADALE DSM

inabidi watumie muda mrefu kusaka maji mbali, suala hili ni la kijinsia ndiyo maana halishugulikiwi na watendaji wanaume ? Kampeni ya mtue ndoo mwanamke imeishia wapi wanahoji wakaazi wa kitongoji cha Mivumoni jijini Dar es Salaam.
Source : EATV
 
Back
Top Bottom