PreGE2025 Miaka 64 unaongoza serikali, Ni wakati sasa CCM ipishe mawazo mbadala kwa maslahi ya Tanzania

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Abraham Lincolnn

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2018
Posts
3,189
Reaction score
6,140
Tangu nchi hii ipate uhuru, hakuna chama cha upinzani kilichowahi kushika hatamu, Je, hii ni kusema CCM ni bora sana? Je, CCM pekee inazalisha genes za wazalendo wa kweli? Kwamba CCM ndiyo chama pekee chenye watu wenye weledi kwa miaka yote hii 64? Kwamba CCM ni malaika? Miaka 64 hawakosei?

Katika michezo, Simba na Yanga angalau na timu zingine kama Mtibwa sugar na Cosmopolitan zilipokezana vijiti kwa miaka zaidi ya 100. Haijawahi kutokea timu moja ikatwaa ubingwa kwa miaka 64! Labda iwe timu ya Malaika!

Tanzania ni nchi kubwa, Yenye utajiri wa maliasili, Mungu ameijalia ardhi kubwa yenye rutuba, mito mabonde na maziwa. Ni wakati sasa kupisha mawazo mbadala, na kupata changamoto mpya katika kuhakikisha tunatumia vyema rasilimali zetu kupiga hatua kubwa zaidi kimaendeleo.

Ni aibu Mtanzania kuzungumzia changamoto za kukosa madawati miaka hii 64! Ni aibu miaka yote hii 64 bado tunazungumzia ujenzi wa vyoo na vyumba vya madarasa! NI AIBU KUBWA!

NI WAKATI WA KUPATA CHANGAMOTO MPYA. NI WAKATI WA MABADILIKO.
 
Halafu mtu anakisimamisha anaomba miaka mitano...kana kwamba hii miaka 60haikuwahi kuongozwa
 
Hofu kuu ni kupoteza kila kitu. Tunahitaji mtu asiye na makando kando ili awapeleke jela wahuni wote wanaocheza rafu kwa sasa.
 
Mawazo Mbadala Yako wapi?
 
Hofu kuu ni kupoteza kila kitu. Tunahitaji mtu asiye na makando kando ili awapeleke jela wahuni wote wanaocheza rafu kwa sasa.
Kichaka Cha amani na usalama wa taifa ndo imekuwa kauli mbiu ya majizi ya Mali za umma kuendelea kuiba,huku wakitumia vyombo vya dola vyenye muundo wa kikoloni.
 
Ngonjera ni "Tuilinde amani yetu kwa gharama yeyote" ilihali wao wanavunja haki za wengine kwa kukataa mawazo mbadala.
 
Back
Top Bottom