Nusu saa nyingi mpaka naandika Uzi huu. Nimetoka kukaguliwa/kupekuliwa begi langu nilipokuwa nimetoka soko la samaki feri kujununulia kitoweo.
Ile njia ya ikulu nyuma mkabala na soko la kukaangia samaki. Tulikuwa watu wengi tuu waenda kwa miguu, wengi tuu Cha ajabu wakanisimamisha mm tuu.
Kwa kiufupi wakanisindikiza mpaka nilikoacha usafiri Ili waone vitambulisho. Wakapekua begi na gari kidogo then wakaniachia.
Ila niliwauliza kwa nini Mimi? Wakaniambia tuu Wana wajibu wa kunipekua hivyo hawajanioonea kunipekua.