Miaka 95 ya Mzee Leopold Rwizandekwe II

Miaka 95 ya Mzee Leopold Rwizandekwe II

Mtoto wa Shule

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2014
Posts
15,133
Reaction score
11,914
Leo katika Kijiji cha Katendagulo, Kata ya Bugandika, Tarafa ya Kiziba, Wilaya ya Missenye, Mkoa wa Kagera kulikuwa na Sherehe ya Kuzaliwa ya Mzee Leopold Rwizandekwe II. Kumbuka huyu Mzee, Mwl. Nyerere akiwa Uingereza alimkabidhi glass yake ya wine alipoitwa kwenda kutoa neno kwenye podium. Ndiye Mwana CCM pekee aliyewahi kuchukua fomu ya kugombea Urais kuchuana na Mwl. Nyerere! My icon. My mentor!

Mwandishi mahiri Joas Kaijage ameandika kitabu kuhusu Mzee huyu. Naamini kitakuwa moja ya "bestsellers" ya vitabu vya Tanzania. Kitabu kimoja kinauzwa sh. 39,000/= tu!

IMG_20240727_185515_470.jpg
IMG_20240727_164147_702.jpg
IMG_20240727_185515_470.jpg
 
Leo katika Kijiji cha Katendagulo, Kata ya Bugandika, Tarafa ya Kiziba, Wilaya ya Missenye, Mkoa wa Kagera kulikuwa na Sherehe ya Kuzaliwa ya Mzee Leopold Rwizandekwe II...
Wahaya wakiziba(warangira) ni tofauti na wahaya wengine, wana maono uthubutu wanajiamini sana wana akili za maisha na darasani, ukisome historia ya huyu jamaa ndo chazo cha nyerere kusema hamna mwenye kiti wa chama (raisi mtarajiwa) kutoka Uhayani chanzo ni huyu mwamba, mwalimu Nyerere hakupenda wa haya katika maisha yake ya uraisi.
 
Wahaya wakiziba(warangira) ni tofauti na wahaya wengine, wana maono uthubutu wanajiamini sana wana akili ya maisha na darasani, ukisome historia ya huyu jamaa ndo chazo cha nyerere kusoma hamna mwenye kiti wa chama (raisi mtarajiwa) kutoka Uhayani chanzo ni huyu mwamba
Kweli mkuu kuhusu AKILI na kuwa visionary tupo hivyo
 
Kiziba hatari sana kwenye harakati zangu nishapanda bodaboda Amushenye tukapita vijiji vya kiziba mpaka kwenye tingatinga nikaambiwa hapo ndio mpaka na Uganda kimsingi ilikuwa moment nzuri kuzipitia.

Namkumbuka Mama Michael kwa ukarimu wa hali ya juu
 
Mkuu karibu tena kwetu. Mandhari nzuri sana! Baada ya kutoka kwenye Sherehe ya Omutwale Rwizandekwe II tupo sehemu hapa upepo mzuri tunashushia "Kalinya"! Ahahahahaha!!!
 
Mkuu karibu tena kwetu. Mandhari nzuri sana! Baada ya kutoka kwenye Sherehe ya Omutwale Rwizandekwe II tupo sehemu hapa upepo mzuri tunashushia "Kalinya"! Ahahahahaha!!!
Mkuu nimekaa kipindi kirefu mkoa wa Kagera wilayani Missenyi Bunazi kutokana na sababu kadhaa kubwa ni kiuchumi niliona kama mkoa wa Kagera umenikataa pressure ya kuhama ilikuwa kubwa na nilivyopata nafasi sikusita kuondoka..

Observation yangu kwa mazingira ni mkoa mzuri sana hali ya hewa nzuri sio baridi wala joto uwepo wa Ziwa Victoria mto Kagera kimsingi umebarikiwa kuwa na resources.

Utamaduni wa kula ndizi japo mie sio mpenzi wa ndizi kuenzi lugha yao kuanzia mjini mpaka vijijini ukikaa mwaka mmoja na ushindwe kuelewa kilugha chao basi utakuwa na kichwa kizito.

Kitu ambacho sijakipenda ni mabinti kupendo zile ndoa za sogea tukae.
 
Waganda kyaka - ni waziba ambao huongea lugha ya kiganda fluency
(Kwa ufasaha since wakiwa watoto)
Wakina Saida kalori anaongea kiganda cha kiziba na kihaya cha kiziba, nilishawshi kusikilza wibo wake wa kiganda kumbe kinafanana na kiziba
 
Mzee Leonard Rwizandekwe aliwashangaza Watanzania mwaka 1965 kwa kukiomba chama cha TANU kimpendekeza kwa wananchi awe mgombea pekee wa urais badala ya Mwalimu Nyerere, akiwa kijiji kwake Katendaguro Wilaya ya Misenye Mkoa wa Kagera alipofanyiwa mahojiano na Elisa Muhingo na Mathias Byabato, Bukoba, anasema wakati huo ilikuwa ni nadra na vigumu mtu yoyote kutaka kugombea nafasi hiyo kwa kuwa wananchi wengi walidhani kuwa hapakuwepo mtu mwingine zaidi ya Mwalimu Nyerere ambaye angeweza kuwa Rais wa nchi.

Alizaliwa tarehe 14 juni mwaka 1929 katika kijiji cha Katendaguro na kusoma shule ya msingi ya Rukurungo na baadae alipelekwa katika jumba la Mugorola lililokuwa Bunge la jadi ambapo hapo alikaa humo akilelewa na wazee ikiwa ni pamoja na kufundishwa maadili, utii, na uwajibikaji.

Mwaka 1948 alichaguliwa kujiunga na shule ya Serikali Ihungo iliyopo Bukoba kwa masomo ya Sekondari ambapo baada ya kuhitimu aliajiriwa katika idara ya mahesabu katika Wilaya ya Buhaya.

Rwizandekwe aliamua kujisomea mwenyewe masomo ya sheria na alipofanya mtihani wa Chuo cha Kibete cha nchini Uganda alifaulu vizuri na baada ya kupata cheti aliajiriwa katika sekta mbalimbali serikalini ambapo juni 1 mwaka 1959 aliteuliwa kuwa Hakimu wa Mahakama ya Rufaa ya Buhaya.

Mwaka 1960 alichaguliwa kama mtumishi bora kutoka Halmashauri ya Buhaya kwenda kuhudhuria semina ya sheria za Afrika nchini Uganda ambapo kupitia huko alichaguliwa pia kuhudhuria masomo ya shahada ya sheria za mila za Afrika katika Chuo Kikuu cha London nchini Uingereza.......
 
Wakina Saida kalori anaongea kiganda cha kiziba na kihaya cha kiziba, nilishawshi kusikilza wibo wake wa kiganda kumbe kinafanana na kiziba
Kyaka
Igayaza
Kabwela
Hadi mpakani Mutukula
 
Mkuu nimekaa kipindi kirefu mkoa wa Kagera wilayani Missenyi Bunazi kutokana na sababu kadhaa kubwa ni kiuchumi niliona kama mkoa wa Kagera umenikataa pressure ya kuhama ilikuwa kubwa na nilivyopata nafasi sikusita kuondoka....
Ahahahahaha! Umeongea vizuri kuhusu kwetu, lakini hiyo ya wadada! Ahahahahaha!!
 
Mzee Leonard Rwizandekwe aliwashangaza Watanzania mwaka 1965 kwa kukiomba chama cha TANU kimpendekeza kwa wananchi awe mgombea pekee wa urais badala ya Mwalimu Nyerere, akiwa kijiji kwake Katendaguro Wilaya ya Misenye Mkoa wa Kagera alipofanyiwa mahojiano na Elisa Muhingo na Mathias Byabato, Bukoba, anasema wakati huo ilikuwa ni nadra na vigumu mtu yoyote kutaka kugombea nafasi hiyo kwa kuwa wananchi wengi walidhani kuwa hapakuwepo mtu mwingine zaidi ya Mwalimu Nyerere ambaye angeweza kuwa Rais wa nchi.

Alizaliwa tarehe 14 juni mwaka 1929 katika kijiji cha Katendaguro na kusoma shule ya msingi ya Rukurungo na baadae alipelekwa katika jumba la Mugorola lililokuwa Bunge la jadi ambapo hapo alikaa humo akilelewa na wazee ikiwa ni pamoja na kufundishwa maadili, utii, na uwajibikaji.

Mwaka 1948 alichaguliwa kujiunga na shule ya Serikali Ihungo iliyopo Bukoba kwa masomo ya Sekondari ambapo baada ya kuhitimu aliajiriwa katika idara ya mahesabu katika Wilaya ya Buhaya.

Rwizandekwe aliamua kujisomea mwenyewe masomo ya sheria na alipofanya mtihani wa Chuo cha Kibete cha nchini Uganda alifaulu vizuri na baada ya kupata cheti aliajiriwa katika sekta mbalimbali serikalini ambapo juni 1 mwaka 1959 aliteuliwa kuwa Hakimu wa Mahakama ya Rufaa ya Buhaya.

Mwaka 1960 alichaguliwa kama mtumishi bora kutoka Halmashauri ya Buhaya kwenda kuhudhuria semina ya sheria za Afrika nchini Uganda ambapo kupitia huko alichaguliwa pia kuhudhuria masomo ya shahada ya sheria za mila za Afrika katika Chuo Kikuu cha London nchini Uingereza.......
Hayo yote yapo kwenye kitabu chake hicho hapo juu kilochoandikwa na Mwandishi Mahiri Joas Kaijage!
 
Back
Top Bottom