Miaka elfu saba ijayo, atheism itakuwa ndio dini kuu duniani. sababu zipo hapa chini

Hapo kwenye distance ya alpha centaur kutoka dunia sio sahihi... Ni 4.35 light years na sio hiyo 4367 uliyosema... That means mwanga unaweza kusafiri kutoka dunia to alpha centaur kwa muda wa miaka 4.35..

Na alpha centaur ni mfumo pekee wa sayari ulio karibu na mfumo wetu wa jua na wanasayansi wanauangalia kwa jicho la pekee..

Kuna sayari kadhaa tayari zimeshagunduliwa kuwa zipo katika eneo linaloweza kubeba maisha na zinafanana na dunia kwa karibu..
 
[emoji38][emoji38][emoji38]!
Mkuu kwenye bustani ya Edeni, Adamu na Eva walimfanyaje Mungu ndiyo akawatimua?
 
Hotuba ya Benjamin Netanyahu UN 2023.

Wenzetu Wana viongozi wenye maono, Sio Huku kwetu kufuga uchawa

Mabibi na mabwana, kama wakati wetu ujao utakuwa wa baraka au laana itategemea pia jinsi tunavyoshughulikia labda maendeleo muhimu zaidi ya wakati wetu. Kuongezeka kwa akili ya bandia AI - Artificial intelligence.

Mapinduzi ya AI yanaendelea kwa kasi kubwa ya kama spidi ya mwanga wa radi. Ilichukua karne nyingi kwa ubinadamu kufikia mapinduzi ya kilimo. Ilichukua miongo kadhaa kufikia mapinduzi ya viwanda. Tunaweza kuwa na miaka michache tu ya kukabiliana na mapinduzi ya AI.


Hatari ni kubwa, na ziko mbele yetu. Kuvurugwa kwa demokrasia, ubongo wetu kuchukuliwa na akili bandia , nafasi za kazi kupunguzwa, kuongezeka kwa uhalifu, na udukuzi wa mifumo yote inayowezesha maisha ya kisasa. Bado kinachosumbua zaidi, ni mlipuko unaowezekana wa vita vinavyoendeshwa na Akili Bandia -AI ambavyo vinaweza kufikia kiwango kisichoweza kufikiria.


Na nyuma ya hii labda kuna tishio kubwa zaidi, kilichokuwa simulizi za kusadikika ya mambo ya hadithi za kisayansi, kwamba mashine za kujifundisha zinaweza kudhibiti wanadamu, badala ya sisi watu kudhibiti mashine. Mataifa yanayoongoza duniani, hata yawe na ushindani, lazima yashughulikie hatari hizi. Ni lazima tufanye hivyo haraka. Na lazima tufanye hivyo pamoja. Lazima tuhakikishe kwamba zama za Akili Bandia ya AI utopia haigeuki kuwa tishio la AI.


Tuna mengi ya chanya ya kupata kupitia Akili Bandia . Hebu wazia baraka za hatimaye kubaini muundo wa kanuni za vinasaba chembe za urithi (gene), kurefusha maisha ya mwanadamu kwa miongo kadhaa, na kupunguza sana magonjwa ya uzee. Hebu fikiria huduma ya afya inayolengwa kulingana na muundo wa maumbile ya vinasaba vya kila mtu, na dawa ya kutabiri ambayo huzuia magonjwa muda mrefu kabla ya kutokea. Wazia roboti zinazosaidia kuwatunza wazee. Hebu fikiria mwisho wa msongamano wa magari, huku magari yanayojiendesha yakiwa ardhini, chini ya ardhi na angani. Hebu wazia elimu ya ziada kujifunza kibinafsi ambayo inakuza uwezo kamili wa kila mtu katika maisha yake yote.


Hebu fikiria ulimwengu wenye nishati safi isiyo na kikomo, na maliasili kwa mataifa yote. Hebu fikiria kilimo cha kisasa zaidi na viwanda vya kiotomatiki vinavyotoa chakula na bidhaa kwa wingi vinavyomaliza kabisa tatizo la njaa na upatikanaji chakula.


Najua huu maneno haya unayosikia ni kama mistari ya wimbo wa mwanamuziki nguli mtunzi John Lennon. Lakini yote yanaweza kutokea.


Hebu subiri kwa punde waza , fikiria kwamba tunaweza kufikia mwisho wa uhaba wa kila kitu!. Kitu ambacho kimeshindikana katika hali ya ubinadamu ndani ya historia yote. Haya Yote ni ndani ya uwezo wetu. Na hapa kuna kitu kingine ambacho tunaweza kufikia. Kwa matumizi sahihi ya Akili Bandia- AI, tunaweza kuchunguza mbingu za mbali kuliko hapo awali na kupanua tunachofahamu zaidi ya sayari yetu ya bluu.


Kwa uzuri au ubaya, maendeleo ya Akili Bandia - AI yataongozwa na mataifa machache, na nchi yangu Israeli tayari iko kati yao. Kama vile mapinduzi ya kiteknolojia ya Israeli yalivyoupa ulimwengu ubunifu wa kustaajabisha, nina imani kwamba Akili Bandia AI iliyotengenezwa na Israeli itasaidia tena wanadamu wote.


Natoa wito kwa viongozi wa dunia kuja pamoja ili kuchagiza mabadiliko makubwa yaliyo mbele yetu. Lakini kufanya hivyo kwa njia ya kuwajibika na ya kimaadili. Lengo letu lazima liwe zaidi kulinda kuwa Akili Bandia- AI inaleta uhuru na sio kiduchu, inazuia vita badala ya kuvianzisha na kuhakikisha kuwa watu wanaishi maisha marefu, yenye afya, yenye tija na amani. Ni ndani ya uwezo wetu.


Na tunapotumia nguvu za Akili Bandia -AI, ngoja kwanza tukumbuke kila wakati thamani isiyoweza kubadilishwa ya ubinadamu na hekima ya mwanadamu. Hebu tuthamini na undani wa uwezo wa huruma, ambao hauwezi kuchukuliwa na nafsi ya Akili Bandia AI.
 
Nimesoma uzi nimekasirika.

Atheism ni kutokuamini kwenye uwepo wa Mungu. Ni mtindo wa maisha unaotokana na msimamo huo.

Kichwa cha uzi kina mashiko, ila uzi wenyewe umeanza kuongelea conspiracy theories za ajabu, na ukaanza kurudi tena kulekule kwenye vitu vya kusadikika.

Atheism ni mtindo wa maisha hauhusiani na hizo conspiracy theories unazoziangalia youtube.
 
Inafikirisha sana
 
Ni 4.367 light years ambayo uki convert kwa miaka ya kawaida unapata miaka elfu saba
 
Hiyo miaka ya dunia mnatumia reference gani? Maana sidhani kama mnaelewa zile law za physics hasa relativity na issue za light travel..

Hapo mkumbuke tunaongelea umbali kwa kulinganisha na mda ambao mwanga ungesafiri kutoka duniani.

Thats means kama kuna possibility ya kusafiri kwa speed ya mwanga ndio utatumia miaka hiyo 4.3 kusafiri na hiyo ni miaka ya dunia..

Issues zinakuja kwenye relativity theory kuwa kwanza there is no possibility (kwa currently technology) kuweza kusafiri kwa hiyo speed..na hicho ndio kinachopelekea kuonekana kuwa ni muda mrefu kufika huko sababu technology tuliyonayo kwa sasa duniani inatulimit hapo so tukitumia chombo chochote kwa hii technology tutatumia miaka mingi mno.

Mfano kwa sasa moja ya vyombo pekee vilivyoweza kutoka nje ya mfumo wetu wa jua ni voyagers probe.. Zipo 2 na zinatembea kwa wastan wa speed 56,000km/h (ambazo ni moja ya speed ya juu kwa vyombo vilivyotengenezwa hadi sasa) ila bado vitachukua si chini ya miaka 80,000 kuweza kufika kwenye mfumo huu wa centauri. Alpha Centauri: Nearest Star System to the Sun

Na pia hata ukitokea kuwezekana kusafiri kwa speed ya mwanga(kitu ambacho theory of relativity ndio inaelezea kuwa haiwezekani kwa vitu vyenye mass zaid ya proton kuweza kusafiri kwa speed hiyo) ndio inakuja swala la relativity theory. Hapo inakuja issue ya relative, yaani unasoma mda kwa aspect ipi.. Mfano ukiweza kusafiri kwa speed ya mwanga.. Anayesafiri (traveller) atachukua miaka hiyo 4 tu kufika huko na 4 kurudi jumla miaka 8. Ila wale watakaokuwa wamebaki duniani (observer) wataona huyo mtu (traveller) amechukua zaidi ya hiyo miaka 4 (hapa sasa kuna ma calculation ya time dilation ya kufa mtu) ila hapo ndio hiyo theory of relativity inapoingia kuwa mda utakaopita kwa traveler na observer utakuwa tofauti.. Kuna video nyingi sana YouTube zinazoelezea hii kwa undani
View: https://youtu.be/b_TkFhj9mgk?si=HM4sk4vTNQUIACYy
Kwaiyo ndio maana nikauliza nyie hiyo miaka ya dunia mna sema kwa base ipi?
 
Miaka 100 tu, dunia nzima inapitia secularization, watu wanaacha dini kwa maamuzi yao binafsi bila kulazimishwa.

Halafu atheism sio dini, ni mtindo wa maisha.
Again sio mtindo wa maisha ( as it is not as set of belief). Ukishaamini au ukishakuwa na mtindo wa maisha, basi hiyo ni DINI. ATHEISM NI KUTOTAMBUA UWEPO WA MUNGU SABABU HAIJATHIBITIKA UWEPO WAKE. UKISHAAMINI KUTOKUWEPO KWA MUNGU, Hauna tofauti na ANAYEEMINI UWEPO WA MUNGU. SO atheist is not a non-believer, he is a REJECTOR.
 
Niliposoma na kuishia hizo habari za Alpha Century nikajua (labda ni yule Kijana wa Nyerere, ikabidi niangalie tena avatar yako) tu humu duniani maisha ni kuishi kama digidigi. Labda hao viumbe wakishuka tu, sisi binadamu ndio tutakuwa kitoweo chao...
 
Kusema kweli napata tabu sana kutofautisha hivyo viwili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…