Mwl Mwakujonga
JF-Expert Member
- Jun 29, 2023
- 384
- 758
Miaka 20s iliyopita, Mlango unafunguliwa mwalimu wa biology anaingia akiwa na mitihani ya kidato cha kwanza. Mwalimu anasalimia darasa na kutangaza matokeo wa kwanza anamtangaza kapata 99% na wa mwisho kapata 0% , kisha anaanza kugawa karatasi
Wakati namwangalia mwalimu anagawa karatasi naona karatasi ya jina imeandikwa kwa kutumia ruler zamani kulikuwa na zile rula zenye alphabet na nakumbuka mtihani huo nilitumia rula kuandika majina yangu
Kadri mwalimu alivyokuwa anagawa daftari ndivyo mapigo ya moyo yanaongezeka, mara miguu inaishiwa nguvu na machozi yanaanza kutoka kwa mbali
Mara jina langu linatajwa kwamba mimi ni mwanafunzi wa mwisho napewa karatasi yangu, mara baada ya kipindi siku hiyo sikula chochote mchana nilibaki tu nikiwa naudhuni nyingi sana
Nikapitia ule mtihani nikaangalia swali moja hadi mwisho hakuna hata swali moja ambalo halikuwepo katika mtihani
Nikawaza kumbe kama ningesoma notisi vizuri nisingepata sifuri, wakati narudi nyumbani nikawa natafakari kwanini mimi nimekuwa wamwisho.
Mawazo yakaingia ndani yangu nyumbani hakuna umeme hivyo sio rahisi kusoma usiku, shule tunatoka saa 8 mcha a hadi nafika nyumbani na kumaliza kazi zote ili niweze kwenda kucheza mpira na wenzangu ni saa 10 jioni na muda ambao ninarudi nyumbani wazazi wametoka kibaruani ni saa 12 au saa 1 jioni
Nikajisemesha moyoni kila siku nitahakikisha kila somo litakalofundishwa darasani ninalisoma nikajipa masaa 2 tu ya kusoma kila siku
Hakuna kaka aliyenipangia mida wa kusoma wala dada wala mama , nilipata msukumo moyoni naamini maombi ya mama yalikuwa yanafanya kazi ndani yangu na Mungu aliona huyu kijana anavyo enenenda hata fika mbali, naamini ni roho wa Mungu alisema na moyo wangu maana kipindi hicho siku nimeokoka wala sikujua kuokoka ni kitu gani, ila moyoni mwangu kulikuwa na kikao.
Kikao hicho kilichofanyika moyoni mwangu na kufikia muafaka kila siku lazima nitenge masaa 2 ya kusoma kile ambacho nimefundishwa, hakuna cha kujitetea.
Kesho yake mara baada ya kurudi shule na kumaliza kazi za nyumbani, nikaanza na kusoma biology , nikasoma yote ambayo nilifundishwa.
Kadri nilivyokuwa nasoma ikawa kawaida yangu, marafiki zangu wakawa wananiuliza hatukuoni siku hizi, nikawa nawaambia kweli shule imebana tutakuwa tunacheza jumamosi na jumapili
Utaratibu ukaendelea hadi namaliza kidoto cha kwanza na kwa kweli matokeo ya kidato cha kwanza hayakuwa ya kawaida
Nakumbuka kuna kipindi hatukuwa na fedha ya kulipa school fees , nakumbuka mama yangu alikuja shuleni kuongea na Mkuu wa shule , mkuu wa shule wakipindi kile katika mazungumzo aliyosema na mama yangu moja tu nililiwekq moyoni alimwonea huruma sana mama anavyopambana kunilipia ada lakini matokeo yangu hayakuwa mazuri na mwisho wasiku alimwambia mtoto mwenyewe mbona hana akili unahangaika buree.
Maneno yale yalikaa moyoni mwangu, nikasema hiko siku atakuja kujua kwamba akili ninazo ni swala la muda tu.
Matokeo ya kuingia form 2 yakatoka kati ya watu 54 nilikuwa 10 na wanafunzi 24 tulichagukiwa kuingia form 2 kwa wastani wa kuanzia 30%.
Nakumbuka furaha niliyoipata ya kuingia form2 , haikuwa ya kawaida nikamshukuru Mungu na ukawa mwanzo wa mafanikio ktk elimu
Nachotaka kukwambia kijana ,mzazi ndugu, usimkatie tamaa mtoto wako. Wala kumsemeha mabaya
Najua kama wazazi tunakasirika na kuona kama watoto wetu hawako serious na wakati mwingine tunatoa maneno makari juu ya watoto wetu na tunajisahau tulipotoka
Siku moja wakati namfundisha mwanangu hesabu nikakwazika nikajikuta natamka maneno ambayo hayakuwa mazuri, nikamkasirikia mtoto akaenda kwa mama yake kujifunza angalau aje kunishawishi baba yake
Nakumbuka moyoni mwangu nilijiskia hatia nakutakiwa kumwomba msamaha kwa kumkosea nilijua Mungu anasema nami kwa kukosa amani
Nikaomba toba nikafuta maneno yote ambayo nilimtakia mwanangu na kumtakia baraka nikamwita nikamwomba msamaha kwakuwa mkali nikambariki akafurahi akaenda kulalana amani
Tusijaribiwe na shetani kuwalaani watoto wetu. Kwa sababu ukilaani analaaniwa kweli
Basi, njoo wewe, nakusihi unilaanie watu hawa; maana wana nguvu kunishinda mimi. Labda nitawaweza, tupate kuwapiga, niwafukuze watoke katika nchi yangu, kwa maana najua ya kuwa yeye umbarikiye hubarikiwa, na yeye umlaaniye hulaaniwa.
Hesabu-Numbers 22:6