Jambo lililo wazi ni kwamba, wale wote wanaomponda Ruge na THT, wao binafsi wala watu wa karibu yao hawajafanya hata 5% ya yale yaliyofanywa na Ruge/THT... wanabaki tu kupiga kelele.
Ruge amebadili game. Kutoka watu kuimba imba kwa kujifurahisha hadi kufanya mziki kibiashara. Biashara ya mziki ni kama biashara nyingine. Ushindani na mbinu mbalimbali lazima zitumike ili kufanikiwa. Tatizo liko kwenye mindset ya wanamuziki waaiojitambuaGame imekuwa ngumu sana,unaposikia wadau wanasema muziki umekuwa biashara basi ujue ni biashara haswa. Ruge ana mazuri yake,ila pia ana mapungufu yake mengi tu...all in all ndio ubepari wenyewe inabidi ukubali hali halisi.
Ila kiukweli muziki umekuwa mgumu sana, tunapoelekea tunaweza tusiinjoi muziki mzuri tena na talents bali watu wenye connection...Pesa inatumika isivyo kawaida, fitna ndio usiseme.