Miaka michache mbele miji ya Africa ndiyo itakuwa na hewa chafu zaidi duniani

Miaka michache mbele miji ya Africa ndiyo itakuwa na hewa chafu zaidi duniani

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Miji mingi mikubwa yenye watu wengi inasumbuliwa sana na hewa chafu. Mchafuzi wa kwanza akiwa ni magari. Moshi wa magari unachafua hewa ya miji ya nchi kama India hadi shule zinafungwa na watu wanashauriwa kukaa ndani. Miji ya China ilikuwa na hewa chafu hadi watu wanatembea na mask.

Leo miji hiyo, hasa kwa nchi kama China, magari ya mafuta yanakuwa replaced na magari ya umeme. Nchi nyingi tajiri zinaelekea magari ya umeme kwa kasi sana.

Africa sababu ya umaskini na ukosefu wa mipango tuko polepole sana kuadapt magari ya umeme. Na hapo mbele nchi zikitunga sheria dhidi ya magari ya mafuta tutegemee kupata magari kibao kwa bei chee. Jambo hili litafanya miji ya Africa iwe na hewa chafu zaidi duniani.

Huko mbele tujiandae kunyanyapaliwa na kutotembelewa sababu ya kuwa na hewa chafu.
 
Back
Top Bottom