Miaka minne bila Magufuli; Inadequate Power Supply would be history (Umeme usiotosheleza utakuwa historia)

Miaka minne bila Magufuli; Inadequate Power Supply would be history (Umeme usiotosheleza utakuwa historia)

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2021
Posts
1,117
Reaction score
3,153
Akiwa jijini Mwanza,Hayati Rais Daktari John Pombe Joseph Magufuli alisema umeme usiotosheleza Tanzania nzima utakuwa historia,aliyasema hayo wakati akifungua kiwanda cha Victoria Moulders Factory,jumanne ya October 31,2017.Akiwa Muleba,Mwaka 2018 alisema umeme wa Muleba tunauchukua Uganda ila tunajenga mradi wa 33KV ili Muleba ipate umeme wa grid ya taifa,Mwaka 2019 akiwa Rufiji kwenye uzinduzi wa Bwawa la umeme la Julius Nyerere alianza hotuba yake kwa kusema"Napenda nianze kwa kumshukuru Mungu mwingi wa rehema kwa kutuwezesha kuwa hai siku ya leo tunapozindua ujenzi wa Bwawa la Umeme la Julius Nyerere"

Umeme utakaozalishwa Bwawa la umeme la Julius Nyerere haujawahi kuzalishwa katika historia ya nchi yetu,natarajia umeme utakaozalishwa hapa utasaidia kushusha gharama za Umeme nchi nzima,baada ya kifo chake Hayati Rais Magufuli,kulikuwa na strategy kadhaa mfano shirika la Umeme lifutiwe madeni ya trillion kama tatu,to ease liquidity na cash flow ya shirika,ili hela inayobaki iweze kusambaza kujenga na kuunganisha umeme kwenye gridi ya taifa na kuusambaza kwa kasi,strategy ya kuomba kuongeza ama kupandisha gharama ya kuunganishia watu umeme (ilhali demand kubwa) basi kampuni binafsi zipewe kibali ili uongeza kasi ya kusambaza miundombinu na kukubaliwa,

Tafakuri ya kawaida tu hauwezi kuomba ndani ya miaka miwili upandishe unit costs za umeme ili uongeze revenue kwa makusudi ya kusambaza umeme halafu leo huna hiyo kasi ya kuusambaza umeme uliyoifikia! na kama umefutiwa madeni ili kukupa nafuu ya liquidity upate hela ya miradi ya kusambaza umeme,vipi mbona tunaanza tena kununua umeme Ethiopia!? kama umejenga chanzo cha megawatt kubwa na sub stations kadhaa ili usambaze umeme na umeruhusiwa kuongeza unit cost ili mapato yaongezeke uongeze speed ya kusambaza umeme,umeruhusiwa kuongeza kampuni binafsi za kuunganisha umeme ili mapato yaongezeke,upate speed ya kuwaunganishia watu,tukiachia hayo pia tunakopa na kwa miradi ya REA ili kuongeza kasi ya kuwaunganishia watu umeme,halafu leo unasema unanunua umeme Ethiopia kwa sababu uwezi fikia watu kwa speed na pia gharama ni kubwa kuutoa umeme Rufiji hadi Arusha,Je wananchi watakuelewa!?

Tunapomkumbuka Hayati Rais John Pombe Joseph Magufuli nitoe maoni yangu kw Serikali yangu tukufu iongeze speed ya kujenga line za 400KV ili Arusha iwe connected na Bwawa la Mwalimu Nyerere either kupitia Chalize,Tanga au Dodoma na Singida,ule mradi wa ujenzi wa 400KV Chalinze,Dodoma uwe speed up there after ijengwe line ya 400KV Dodoma to Singida,na pia iangaliwe namna ya kujenga 400KV line from Chalinze to Tanga kwa sasa line inayotoka Chalize to Arusha via Tanga sidhani kama inakidhi mahitaji na ni chakavu sana,Naomba niikumbushe Serikali yangu kwamba suluhisho la muda mrefu si kununua umeme tu,bali pia kuimarisha mfumo wa usambazaji wa umeme wa ndani,Tanzania inahitaji kuwekeza zaidi katika High Voltage Direct Current (HVDC) Transmission Lines,ambazo zinaweza kupunguza upotevu wa umeme hadi chini ya 5%.

Nchi kama Brazil na China zimewekeza katika HVDC na zimefanikiwa kupunguza upotevu wa umeme kwa zaidi ya 70%.Tanzania inapaswa kujifunza kutoka kwao,badala ya kutegemea njia za zamani za kusafirisha umeme ambazo zina upotevu mkubwa,ni wakati wa kuwekeza kwenye miundombinu bora ya nishati,pia, ni muhimu kuimarisha substations na transformers ili kupunguza hasara zinazotokea wakati wa kubadilisha voltage ya umeme,hili ni jambo ambalo TANESCO inapaswa kulifanyia kazi kwa haraka.

-Swali la Msingi kutoka kwa Wananchi,kwa nini tununue Umeme nje ya nchi wakati Serikali ilisema Tanzania itajitosheleza na Umeme pindi Bwawa la Umeme la Julius Nyerere litakapokamilika?

Kwanini Tanzania inapanga kununua umeme kutoka nje ya nchi kwa ajili ya Kanda ya kaskazini!?

1. Umeme uliopo katika Gridi ya Taifa unazalishwa kutoka ukanda wa kusini Mashariki na hivyo kulazimika kusafirishwa umbali mrefu kwenda maeneo mbalimbali nchini hali inayosababisha upotevu mkubwa wa umeme.

Tafakuri ya Wananchi;hivi kutoka Morogoro hadi Kilimanjaro na kutoka Ethiopia hadi Kilimanjaro wapi mbali?Kutoka Moshi hadi Ethiopia kunakozalishwa umeme ni kilomita 1400

Na kutoka Rufiji umeme unatoka bwawa la Nyerere hadi Moshi ni kilomita 735

2. Kwa Kanda ya Kaskazini upotevu wa umeme unaosafirishwa umekuwa ukisababisha hasara ya zaidi ya shilingi Bilioni 32 kwa mwaka.

Tafakuri ya Wananchi;hivi kwani tunaponunua umeme kutoka nje ya nchi hatuingii gharama kubwa? Na je suala hili na hilo hapo juu si kitu kimoja tu =UPOTEVU WA UMEME/GHARAMA KUBWA?

3. Kutokana na upotevu huo na usafirishaji mrefu wa umeme, Kandaya Kaskazini imekuwa ikikabiliwa na changamoto kubwa ya kukatika kwa umeme mara kwa mara hali ambayo inawaathiri wananchi.

Tafakuri ya Wananchi;Umeme kukatika hovyo ni tatizo hata Dar es Salaam pale Ubungo na Kinyerezi unapozaliswa umeme wa gesi,ni tatizo hata kule Morogoro Kidatu na Mtera Dodoma.Mpaka sasa hakuna sababu za msingi za kununua umeme wowote kutoka nje ili kuleta mikoa ya Kaskazini. HAKUNA.

Kama sababu ni umbali, Ethiopia ni mbali mnoo kuliko Rufiji.
Kama sababu ni unafuu, huwezi kulinganisha umeme wetu wa bure (tunaouzalisha sasa mpaka hatuna pa kuupeleka) dhidi ya umeme tutakaoununua kutoka nje kwa bei yoyote.

Mwisho wa yoyote, walikuwa wapi kuuleta huo umeme wa Ethiopia (wa bei nafuu na uhakika) wakati wote tulipokuwa tunapitia msoto wa mgao wa umeme kwa sababu ya upungufu wa uzalishaji kabla ya kukamilika bwawa la Nyerere?, na kwanini haukuwa umeme mbadala wa ule umeme wa mitambo ya gesi tuliokuwa tunaununua kwa gharama kubwa?

4. Ununuzi wa umeme kutoka Ethiopia kupitia Kenya utasaidia kuondoa changamoto ya kukatika kwa umeme mara kwa mara na kuokoa upotevu mkubwa wa umeme unaokwenda katika kanda hiyo.
Tafakuri ya Wananchi;hayo hayo tayari mmeyazungumzia number 3, 2 na 1 hapo juu???Aidha, tunayo-pool of Electrical Engineers hapa nchini tena wengine ni PhD holders wabobevu kwenye tafiti,si kungefanyika project ya uvumbuzi kukabiliana na upotevu mkubwa huo wa umeme angalau upotevu ufikie asilimia 0.0005 ya upotevu wa sasa? Au kama vipi tuwaite marafiki zetu wa damu wachina tuwape mchongo huo,tuone show itakavyokuwa hapo! Hoja ni kwamba, unakozalishwa ni Ethiopia ina maana humo njiani haupotei?

Kama tunahesabia umbali kutoka Kenya, basi pia hata huu wa rufiji tutahesabia umbali pale mkoa jirani uliounganishwa na grid ya taifa.

Kwa namna nyingie, humu bongo, kila mkoa huwa unapokea umeme grid ya taifa na mkoa mwingine unachukulia pale kama ambavyo wao watachukulia Kenya.

Wakija na hoja ya umbali kunakozalishwa umeme, Ethiopia ni mbali kuliko rufiji.

Degree holder akiwa mtaani:In summary,In Abundance of Water a Fool is Thirsty....

Kwamba Ethiopia wameweza kuleta Umeme mpaka huku bila kupata huo upotevu ambazo sisi tunapata kwa kusambaza mpaka pale tu ?!!! na zile pesa alizotumia Mwezi wa kwanza akiwa anasuka mfumo upya alikuwa anasuka nini Nywele ?

Na tunapopanga kuuza nje tutakuwa tunauza na kusafirisha vipi bila huo upotevu unaopatikana sasa ?

This is insulting our intelligence..., hata kama kuna upotevu ni through incompetence kama nje wanauza kwa bei rahisi basi tufunge uzalishaji tununue kabisa zote kutoka nje..., hii ndio pakacha linavuja badala ya kuliziba unaongeza juhudi ya kulijaza....

Nimalizie kwa tafakuri jadidi hasa kwa wale waliosomeshwa na Serikali,pesa iliyotumika kusomesha wasomi isilete laana kwa Taifa la Tanzania,tunayo-pool of Electrical Engineers hapa nchini tena wengine ni PhD holders wabobevu kwenye tafiti,nawaita kwa sauti ya Hayati Rais John Pombe Joseph Magufuli mfanye project ya uvumbuzi kukabiliana na upotevu mkubwa huo wa umeme angalau upotevu ufikie asilimia 0.0005 ya upotevu wa sasa,nimejaribu kuwaza tuu! au kama vipi tuwaite marafiki zetu wa damu wachina tuwape mchongo tuone show itakavyokuwa hapo!

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of business administration in international business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publications;-
-Assessment on the effects of microfinancing on poverty reduction.
 
Magufuli yuko very over rated, naye alikuwa ni fisadi tu kama masisiyemu mengine
 
Insha ndeefu,pumba tupu,umeme haujawi kuwa kidogo nchi hii' Kati ya 2012 mpaka leo,shida ni miundombinu ya kuusafirisha
 
Uchawa hulea maovu ya wakubwa hata kama mchawa anayaona mouvu, kikubwa apate damu ya kunywa kama chawa
 
Tunaye Rais awamu ya sita, ambaye aliipokea miradi ikiwa Hoi na chini ya asilimia 30,ameweza yeye ni mshindi, tumpe kura zote, October amalizie na kazi zingine,
#mitano tena!
 
Back
Top Bottom