Miaka minne ya ndoa mke agundulika ana vvu je anastahiri taraka?

Miaka minne ya ndoa mke agundulika ana vvu je anastahiri taraka?

fundi msati

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2013
Posts
216
Reaction score
91
HABARI!

Poleni wadau, leo naomba msaada wa mawazo haswa yenye mtazamo wa kiimani wenye elimu ya dini KWANZA niwajuze wale wataonishauri kupeleka hili kwenye jukwaa la dini na majukwaa mengine kuwa NILISHINDWA FANYA IVYO ndio maana nipo hapa.

Mimi ni kijana ambae nina elimu inayonisaidia kuchukua udhutu lakini kutokana na nilipo kukosa wasomi nami naonekana USTAADH mara kwa mara watu unifuata na kuomba niwe mshenga kwenye ndoa zao sasa kuna mmoja amekuja kutaka FATUA juu ya tatizo la mke wake.

Walifunga ndoa miaka 4 iliyopita wana mtoto mmoja sasa. Tatizo ni pale mkewe alipo umwa ghafla miezi michache baada ya kujifungua baada ya kwenda huku na huko mke imethibitishwa kuwa ana VVU.

Mume akajitaidi kunusuru maisha yake na sasa yupo vizuri tu,mume amepima mara kadhaa hana vvu.

Anadai kuwa hajiskii vizuri kuishi ktk hali hiyo lakini hajui kwa tamko la dini.
 
- Je, mtoto naye kazaliwa na ugonjwa?
- Kwa mfano angekuwa ni yeye mwanaume kakutwa na hayo maradhi angefanyiza vipi?
- Waende tu kwa washauri wajuzwe namna ya kuendelea kuifurahia ndoa yao.
 
Mwambie jamaa aendelee kupiga kavu kavu coz yeye hawez kuambukizwa
 
msitengane kwa sababu hiyo, kaeni pamoja mumlee mtoto na kupanga mikakati yenu ya kimaendeleo, wazo la kuachana kwa sababu mmoja wenu kaukwaa halina tija!!
 
Kama akigundulika na kansa je? Bado utamtaliki?
 
Swali ni kumbwa kaumwa ndani ya ndoa au la? Hapa inabidi mume akuekezee mahusiano yao yalivo, yani mepenzi yao...kama wanapenda na walikua na maelewano mazuri toka mwanzo na hajawahi kum suspect kama anatoka nje ya ndoa haina haja ya kumpa talaka, anyway talaka ni step ya mwisho kabisa
 
Mwambie jamaa aendelee kupiga kavu kavu coz yeye hawez kuambukizwa

Naunga hoja yako mkuu zipo familia nyingi zinaishi hivyo bila tabu na wanaendelea kuzaa!!!kosa ni lake kwa nini hawakupima kabla ya ndoa?hata hivyo ugonjwa Haumpi mtu talaka labda aongeze mke
 
Naunga hoja yako mkuu zipo familia nyingi zinaishi hivyo bila tabu na wanaendelea kuzaa!!!kosa ni lake kwa nini hawakupima kabla ya ndoa?hata hivyo ugonjwa Haumpi mtu talaka labda aongeze mke

Kweli kabisa leo tukisema tupite kila familia tupimane ndoa za aina hi zitapatikana nyingi tu
 
Vvu huambukizwa kwa njia nyingi sio kwa kujamiiana tu kwahyo asimpe talaka,wakae chini wajue watamleaje mtoto na si kuwaza kutengana

Sent from my iPhone using JamiiForums mobile...
 
Hakuna sababu ya kumuacha kwan VVU huwa haviambukizwi kwa kufanya mapenzi peke yake, Wawaone wataalam ili kupata ushauri nasaha na wakizingatia maelekezo maisha yataendelea kwa raha mustarehe.
 
Ni changamoto kama changamoto zingine waikabili.
 
Sababu za kupata VVU ni nyingi sio lazima awe ametoka nje ya ndoa, kwahiyo naona haina haja ya kumtaliki huyo mama. Waendelee tu kuishi kama mke na mume, hiyo pia ni kwasababu ya mtoto ambaye kwa umri huu mdogo kuwa na divorced parents ni tatizo.
 
- Je, mtoto naye kazaliwa na ugonjwa?
- Kwa mfano angekuwa ni yeye mwanaume kakutwa na hayo maradhi angefanyiza vipi?
- Waende tu kwa washauri wajuzwe namna ya kuendelea kuifurahia ndoa yao.

mkuu sijajua bado kwakua mtoto wao ameambiwa amuachishe sasa. nakitendo kinacho muumiza nipale kuona mtoto wake hanyonyi hali yumdogo sana acha nitamuuliza maratu nitapo mpatia muda
 
Aowe mke mwengine yy akiendelea kuwepo nakupata huduma zote
 
Swali ni kumbwa kaumwa ndani ya ndoa au la? Hapa inabidi mume akuekezee mahusiano yao yalivo, yani mepenzi yao...kama wanapenda na walikua na maelewano mazuri toka mwanzo na hajawahi kum suspect kama anatoka nje ya ndoa haina haja ya kumpa talaka, anyway talaka ni step ya mwisho kabisa

CTU mkubwa!! binti alikua namtoto wake kabla yakuolewa anasoma darasa la 3. aliachana na baba wa huyo mtoto miaka hata 7 imeshafika jamaa tangu kuwanae hawajawahi kua namigogoro kwenye ndoa yao nikiwa ndio mshenga nashahidi wandoa hiyo sijawai kuletewa malala miko hata maramoja hapo kabla yakugundua hilo hajawai kukaanae mbali kwa kipindi hata cha mwezitu, tofauti nasasa uwa akiondoka anakaakwamda mrefu tena bila kujali familia hali iliyopelekea mwanamke aje kulalama na nilipo muuliza mwanaume ndio akasema yote hayo
 
Back
Top Bottom