Miaka mitano iliyopita ulikuwa unaamini nini ambacho leo kimebadili mtazamo wako?

Miaka mitano iliyopita ulikuwa unaamini nini ambacho leo kimebadili mtazamo wako?

Manyanza

Platinum Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
22,269
Reaction score
58,563
Kadiri tunavyokua, tunakutana na watu tofauti, tunaingia kwenye mahusiano, tunajenga urafiki, tunapitia changamoto na kujifunza mambo ambayo wakati mwingine hubadilisha kabisa namna tunavyoutazama ulimwengu.

Huenda miaka mitano iliyopita uliamini kwamba mapenzi ya kweli yanatosha kudumisha uhusiano, lakini leo unaamini kwamba upendo bila heshima, uaminifu na uwajibikaji hauwezi kujenga mahusiano yenye afya.

Huenda uliamini kwamba rafiki wa kweli ni yule anayekuwepo wakati wa furaha, lakini uzoefu umekufundisha kuwa urafiki wa kweli huonekana zaidi wakati wa changamoto.

Au huenda uliamini kwamba kumsaidia kila mtu ni ishara ya utu, lakini sasa umejifunza umuhimu wa kuweka mipaka na kutambua kwamba si kila mtu anayekukaribia ana nia njema.

Ningependa kusikia mitazamo yenu..

Ni jambo gani ulilokuwa unaliamini kuhusu mapenzi lakini uzoefu umekufundisha tofauti?

Je, upendo pekee unatosha kudumisha uhusiano au kuna mambo mengine muhimu zaidi?

Ni lini ulitambua kwamba si kila mtu unayemuita rafiki anaweza kuwa rafiki wa kweli?

Je, kadiri unavyokua unapaswa kuwa na watu wengi katika maisha yako au kuchagua wachache wenye maana?

Ni funzo gani kubwa ulilopata katika miaka mitano iliyopita ambalo limebadili kabisa namna unavyoishi na kuwachukulia watu?

Karibuni tushirikishane uzoefu, sio kwa lengo la kuhukumiana, bali kujifunza kutoka katika mitazamo na safari za maisha za kila mmoja.
Wakati mwingine, jambo tunaloliita mabadiliko ya mtazamo ni matokeo ya uzoefu ambao maisha yametufundisha.
 
a)Upendo pekee hautoshi kudumisha uhusiano.
Inabidi kumjua mwenzi wako mapungufu yake na kuyakubali kuwa hawezi badilika katika hayo, ili maisha yaendelee.

b)kadiri unavyomjua mtu zaidi kiundani ndivyo heshima yako kwake inavyopotea, hivyo tuwachukulie kama walivyo na mapungufu yao na tuheshimu hadhi yao.

c)Kadri ninavyokuwa maisha yananipa fursa ya kubadili watu wapya, kwani watu wapya wana mawazo mapya.
 
Ulie nae leo haujalishi mumeshibana kiasi Gani amini Kuna siku mtapotezana na hamto kuja onana tena, hivo ukiwa na watu leo, watumiwe haswa ukijua wakiondoka hamtokuja kuishi tena kama jana
 
Maisha ni batili, chochote unachofanya hakikisha kinakula furaha hata kwa sekunde hii inaamana kubwa sana utakuja kujua mbele.
 
Back
Top Bottom