KwetuKwanza
Senior Member
- Mar 13, 2023
- 127
- 245
Ilikuwa Machi 3, 2021 Siku ambayo aliyekuwa Waziri wa Nishati wakati huo Medard Kalemani alipoweka jiwe la msingi ujenzi wa kituo cha kupozea umeme (Sub Station) Mkoa wa Simiyu.
Hafla ya kuweka Jiwe la Msingi ilifanyika katika eneo la Imalilo, eneo ambalo lilichaguliwa kituo kijengwe ni nje kidogo ya mji wa Bariadi.
Shamra Shamra za siku hiyo zilikuwa kubwa sana, zikiashiria kituo kinakwenda kujengwa na Mkoa wa Simiyu kuondokana na adha kubwa ya katikakatika kwa umeme ambayo utokea kila mara.
Adha hii, ni kama kuna mtoto anachezea switch ya umeme anawasha, na kuzima, ndivyo umeme wa Simiyu ulivyo, watalaamu walisema tatizo hicho linasababisha na Mkoa wa Simiyu kukosa kituo cha kupozea umeme.
Yaani wanasema njia za kusafirisha umeme ni ndefu, kutoka Shinyanga, kutoka Mwanza na Kutoka Mara, hivyo umbali huo kuna mambo mengi yanatokea ikiwemo wanyama kugusa nyanya n.k.
Wana Jukwaa la Jamii Forums mnajua hoja yangu hapa ni Nini? Mwaka wa Tano huu, yaani ni mwaka wa tano Serikali inajenga kituo cha kupozea Umeme Mkoa wa Simiyu.
Yaani imekuwa kichekesho, mpaka inatia kinyaa, wananchi wa mkoa huu tunajiuliza zile mbwembwe, shamra shamra za siku ille Kalemani anaweka jiwe la msingi zilikuwa na maana gani?
Mpaka sasa hakuna kituo kilichojengwa na hakuna dalili za kituo kujengwa, kwenye hilo eneo la Imalilo limebaki Jiwe lile tu la Msingi ambalo lilijengwa tu, au labda hicho ndicho kituo.
Kero ya katakata kwa umeme mkoa wa Simiyu ipo pale pale na sasa ni kama imezidi kupita kiasi, kila siku viongozi wa mkoa na tanesco ni ngonjela tu, kituo kitajengwa, kitajengwa, mara kinajengwa, mara mkandarasi yupo site, lakini ukienda kuangalia hakuna kitu.
Wana Simiyu tunajiuliza kwani katika mkoa wetu kuna shida gani, Miaka mitano kabisa tunajenga kituo cha Umeme? Kituo gani kinajengwa muda wote huo, Je Kalemani alikuwa anatudanganya? Je Serikali ya CCM inawadanganya wananchi? Miaka mitano kituo kinajengwa, na kinachojengwa ni hewa tu.
Pia soma
~ TANESCO yatoa majibu kuhusu ufafanuzi wa majibu ya Mradi wa Kupoza Umeme Mkoani Simiyu
~ TANESCO: Tuliona tunasumbuana na Mkandarasi wa Mradi wa Imalilo tumeamua kuuendeleza na Wataalam wa ndani