Miaka mitano ya kifo cha Kanumba na maendeleo ya bongo muvi

Miaka mitano ya kifo cha Kanumba na maendeleo ya bongo muvi

Innocent Kirumbuyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2014
Posts
4,641
Reaction score
4,457
Wakuu tarehe kama ya leo ilikuwa siku chungu kwa Tanzania na duniani. Ilikuwa ni siku tuliyompoteza ngwiji la kuigiza Steven kanumba

Binafsi hiki kifo kiliniumiza sana miaka imekwenda kwa kasi sana hatimaye leo ni miaka mitano ya kifo chake baada ya miaka hii mitano ya kifo chake ni rasmi kabisa na ni miaka mitano ya kifo cha bongo muvi toka aondoke kanumba hakuna tena kilichoendelea

Bongo muvi imebaki jina tu hakuna aliyevaa viatu vya kanumba Ray aliyekuwa tunamuona ni mpinzani wa kanumba kumbe sivyo alikuwa anabebwa na kanumba yani kwa ufupi tu leo tunaazimisha miaka mitano kifo cha kanumba na bongo muvi wakuu napenda kuuliza nn kifanyike ili bongo muvi irudi kama kipindi cha marehemu kanumba
 
Kuigiza kitu kikaeleweka na kukubalika na jamii, kikapendwa na kununulika ni STADI, ni KARAMA ya mwenyezi Mungu; sio kila mtu anaweza kufanya! Bongo movie waache kuiona tasnia ya filamu kama. Mahali pa kuganga njaa, kwamba mtu akikosa la kufanya basi anarukia kuigiza, la hasha, waende daradani, wajipange upya kimkakati, wajitathmini kwanini wamedorola kiasi hiki tangu kifo cha Stevo! Tabia ya mtu kukurupuka kwenye njozi akaibuka na script isiyo na miguu wala kichwa kisha akakusanya waganga njaa kadha kushoot movie kabla ya kuichambua barabara ni kunajisi tasnia!
 
Ni kweli wengi waliopo bongo muv awana vipaji
 
Naona hizi tarehe zinahusiana kabisa maana hata kiongozi wao amefariki tarehe 6/4. Kanumba alifariki tarehe 7/4.
Hapa kiongozi wao ni Sir Chande.
Kwa hizi hesabu kama huyo kiongozi angefariki leo basi watu wangefunga faili la Kanumba na u-freemason! Ingekuwa verified!!
 
Naona hizi tarehe zinahusiana kabisa maana hata kiongozi wao amefariki tarehe 6/4. Kanumba alifariki tarehe 7/4.
Hapa kiongozi wao ni Sir Chande.
Sir Chande kacheza movie gani mkuu? Au ndio uwezo wa kufikiri umeisha hapo?
 
Apumzike panapistahili.kiukweli huwa nashangaa sana nkiona watu wanavyompa legendary status huyu jamaa.the guy was avarage at best,au ni macho yangu yanaona tafauti.kanumba alikuwa wakawaida sana
 
Bongo movie ilienda na kanumba waliobaki, wamekosa UBUNIFU wanawaza mapenzi na ubishoo tu
 
Apumzike panapistahili.kiukweli huwa nashangaa sana nkiona watu wanavyompa legendary status huyu jamaa.the guy was avarage at best,au ni macho yangu yanaona tafauti.kanumba alikuwa wakawaida sana
Macho yako ndo ya kawaida, acha kutupandisha hasira fall.. Wewe. Wewe una nini kisicho cha kawaida zaidi ya hivi vipost uchwara? Umejua kuandika mstari mmoja wa kiingereza nawe unajiona gwiji? Acha kudharau watu waliozitendea haki karama zao. Wewe karama yako ya umbea tu imekushinda wakati huitaji mtaji wowote zaidi ya maneno.
 
Back
Top Bottom