Miaka mitatu tangu kuuwawa kwa Alphonsi Mawazo.

Miaka mitatu tangu kuuwawa kwa Alphonsi Mawazo.

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,497
Reaction score
4,775
1.Mwaka sita wa sabini,nyota ilianza waka
Ulifika duniani,shujaa na wetu kaka
Nuru yako maishani,ikaanza kumulika
Twakukumbuka shujaa,mpambanaji Mawazo.


2.Ulofundisha Bondeni,vyema ukaelewa
Wanafunzi darasani,maarifa walidaka
Elimu nzuri kichwani,kwa bidii wakashika
Twakukumbuka shujaa,mpambanaji Mawazo.


3.Siasa za jukwaani,nako ukaanza wika
Kuanza na udiwani,upite pwani na nyika
Sera zo za akilini,kwingi zikatawanyika
Twakukumbaka shujaa,mpambanaji Mawazo.


4.Wananchi Sombetini,bado wanakukumbuka
Hadi Geita jamanj,machozi yabubujika
Huzuni kubwa moyoni katu huto sahulika
Twakukumbuka shujaa,mpambanaji Mawazo.


5.Ulondoka duniani,kweli ulipotamka
Mapanga mengi mwili,damu zikachuruzika
Maumivu ya kichwani,na rohoni yalifika
Twakukumbuka shujaa,mpambanaji Mawazo.


6.Hukufanya uhaini,lakini uliteseka
Kukwondoa limwenguni,wao walifurahika
Kweli ipite pembeni,kwao ili tarajika
Twakukumbuka shujaa,mpambanaji Mawazo.


7.Hazitofika mwishoni,harakati kufanyika
Kwa kumizana mwilini,damu hovyo kumwagika
Twajengana akilini,Amani inatoweka
Twakukumbuka shujaa,mpambanaji Mawazo.


8.Twajenga taifa gani,kwa mambo yanayozuka
Kuuwawa wapinzani,jambo lakuchukizika
Kwenye nchi ya Amani,laana inajengeka
Twakukumbuka shujaa, mpambanaji Mawazo.


9.Majonzi bado chamani,ni lini yatafutika
Na machozi mashavuni,yanazidi bubujika
Haki mefichwa gizani,vigumu kufarijika
Twakukumbuka shujaa, mpambanaji Mawazo.


10.Siku moja twaamini,haki yo watatamka
Kama siyo duniani,ni akhera tukifika
Tukiwa kwenye mizani,hukumu kutimilika
Twakukumbuka shujaa mpambanaji Mawazo.


SHAIRI-TWAKUKUMBUKA MAWAZO
MTUNZI-Idd Ninga,Tengeru Arusha.
+255624010160
Iddyallyninga@gmail.com
 
Alphonce Mawazo
IMG_20181114_114308.jpeg
 
Ni hatari sana na dhambi kubwa sana damu kumwagwa bila hatia bila wahusika kuchukuliwa hatua, hao watakuwa wauwaji sugu, hawatapata amani kama hawataacha kuua tena na tena.

Vv
 
Najiuliza tu hivi siku ikitokea mtoto wa marehem akawa Rais wa bongoland!!
Kuna wajukuu wa watu flani watapata tabu sana!!!
 
Back
Top Bottom