Is music a universal language? Ndio but sio kwa 100% kwanini?
despacito imeimbwa kiispanyola na wasanii wakubwa ambao wameshakita mizizi kwenye muziki globally, nchi zinazozungumza kiispanyola ni nyingi sana karibia Latino america yote wanazungumza kiispanyola plus Hispania vyenyewe so ni rahisi muziki wao kupenya, wakongo : wakongo wanaimba kilingala,kiswahili na kifaransa, kifaransa ni international language inazungumzwa afrika na nchi tu inazungimzwa ulaya so ni rahisi wao kupenya, wahindi waliliteka soko la dunia kupitia movies then nyimbo zao tukazijua kupitia muvi zao na nyimbo zote za kihindi zilizopenya na kuhit bongo hata worldwide tulizijua kupitia muvi zao na ndio maana mpaka Leo kuna watu wanaamini zile nyimbo zimeimbwa na kina sharukan,salman khan,ajay devgan,akshay Kumar n.k nikikuambia unitajie hao wasanii walioimba hizo nyimbo huwezi kuwataja labda u google nje ya hizo movie zao unamjua mwanamuziki gani wa India? India kwenye soko la dunia inajulikana dunia nzima katika nyanja mbalimbali za burudani na michezo mfano kriketi n.k sisi Tanzania hatujulikani popote muziki wetu bado uko chini sana yaani sana tu kwenye soko la dunia lugha tunayotumia inazungumzwa east Africa tu ukienda duniani huko hawaijui lugha ya kiswahili na wachace wanaoijua wanadhani ni ya Kenya unaanzaje kupata attention na kupenya ulaya bila kitumia lugha wanazozielewa au wasanii wenye soko ulaya na marekani,uarabuni i mean asia? Hapa Africa nchi zinazoelewa na kuzungumza lugha ya kifaransa na kiingereza ni nyingi kuliko zinazoelewa na kuzungumza kiswahili, unapenyaje? Halafu sisi muziki wetu ni fusion yaani mchanganyiko wa muziki mingi bado hatuna muziki wetu hata Nigeria nao muziki wao ni fusion watu kwenye muziki wao hapa afrika ni south afrika wana kwaito yaani ukisikia tu mdundo unajua hii kwaito haifanani na muziki mwingine