Kuelekea maadhimisho ya Miaka Miwili ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, wananchi katika kata za Ubungo, Tandale, Manzese, Kijitonyama, Sinza Ndugumbi, Mwananyamala na Makumbusho katika Halmashauri za Manispaa ya Ubungo na Kinondoni zinazopitiwa na Mto Ng’ombe pamoja na Mto Kiboko wamemshukuru Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hasan kwa kazi kubwa iliyofanyika ya kuwaondolea adha ya mafuriko iliyokuwa ikawakabili kwa muda mrefu na kuwafanya wakimbizi katika nyumba zao.
Tazama mwonekano wa sasa wa Mto Ng’ombe uliosafishwa na kujengwa kwa Zege pamoja na kujenga machujio ya maji na mabwawa ya kuhifadhi maji (Detention Ponds) katika eneo la ubungo ili kudhibiti mafuriko na kubali kabisa mandhari ya maeneo yote yanayopitiwa na Mto.
Mto wenye urefu wa kilomita nane nukta saba (km 8.7) umejengwa kupitia Mradi wa DMD ulio chini ya Ofisi ya Rais Tamisemi na kusimamiwa na TARURA.
Dar Es salaam Metropolitan Development Projects Ipo zaidi ya miaka kumi na tano haikuanza enzi za Samia...
Na Pesa ni ya World Bank Mama anahisukaje na miradi ameikuta...Kama kongole apewe JK na Magu.
Kiukweli mradi huo,umeleta AFUENI kwa wakazi wa Sinza,Knyama,Nyamala hadi Kndoni Mkwajuni..maji yanapita kwa kasi hivyo hakuna tena mafuriko..heko kwa World Bank na Uongozi mzima wa DMDP..