Miaka yangu 6 Jf

Miaka yangu 6 Jf

Khantwe

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2012
Posts
59,415
Reaction score
119,473
Habari zenu wakuu,
Leo nimetimiza miaka sita tangu nimejiunga na huu mtandao wetu pendwa (yaani nilijiunga nikiwa kijana mpaka nimekuwa mzee hahaa). Nampongeza sana mwanzilishi wa JamiiForums kwa kuanzisha hii platform maana ni ya kipekee na ina ladha ya peke yake.
Kusema kweli nimejifunza mengi sana kupitia mada za hapa na zimenisaidia sana katika kubadili mtazamo kuhusu maisha achilia burudani zisizokwisha aisee kweli hii ni stress free zone.
Hum ndani kuna kila kitu, kuna wakati utafurahi, utajifunza,utapenda, utapendwa, utahuzunika, utaumia, yote tumeumbiwa wanadamu cha muhimu ni kusonga mbele huku ukimtegemea Mungu na kuzichukua changamoto kama sehemu ya maisha.
Cha mwisho ninashukuru miaka yangu yote hii sijawahi kula ban [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]. Hili nalo la kujivunia eti, si kwamba mimi ni mwema sana kuzidi akina fulani wanaokula ban kila baada ya siku mbili ( siwataji [emoji87]), ni neema tu.
Nawapenda nyoote hata msionipenda naomba niwatakie heri ya Christmas na mwaka mpya.

NB
Kwa mtu yeyote niliyewahi kumkwaza katika kipindi nilichokuwepo Jf naomba anisamehe hata akinifungukia hapa sehemu niliyomkwaza au ambayo huwa namkera. Mimi wengi nimewasamehe bado wachache tu [emoji87][emoji87][emoji87]
 
Umenifanya nitabasamu!
Dadangu uliijuaje JF ukiwa bado kigoli eti
Nilikuwa kwenye magroup fulani ya kisiasa Facebook watu wakawa wanaiongelea saa nyingine wanaleta link, nikalike page yao baadae na mimi nikajoin, halafu mwanzo nilijua ni forum ya kisiasa tu.
 
Nilikuwa kwenye magroup fulani ya kisiasa Facebook watu wakawa wanaiongelea saa nyingine wanaleta link, nikalike page yao baadae na mimi nikajoin, halafu mwanzo nilijua ni forum ya kisiasa tu.
Hongera sana dadangu mzuri..
Kipindi hicho sijui ndo nilikuwa mwaka wa kwanza jamaniii
 
Cha mwisho ninashukuru miaka yangu yote hii sijawahi kula ban
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
. Hili nalo la kujivunia eti, si kwamba mimi ni mwema sana kuzidi akina fulani wanaokula ban kila baada ya siku mbili ( siwataji
emoji87.png
), ni neema tu.
Na sisi wenye zaidi ya miaka 8 na hatujawahi kuwa banned tunacomment wapi?
 
Back
Top Bottom