Miaka Zaidi ya 60 Baada ya Uhuru,Tanzania Imeshindwa Kuondoa Mizizi ya Ukoloni Kwa Nchi kuwa tegemezi wa Uchumi na Mapato Kwa Jiji Moja tuu la Dar

Miaka Zaidi ya 60 Baada ya Uhuru,Tanzania Imeshindwa Kuondoa Mizizi ya Ukoloni Kwa Nchi kuwa tegemezi wa Uchumi na Mapato Kwa Jiji Moja tuu la Dar

Kama shida Yako ni kuwa na watu wengi kama hoja kuu namba 1 basi haupo,watu wengi wako Dar.

Sababu za watu wengi kujazana Dar nimeshazieleza kwenye hoja hapo Juu.

Ndio athari hiyo ya kuendeleza sera za kikoloni badala ya sera za kiuchumi za mjumuisho.
Jadili sabubu za kuwezesha kuwapunguza na kuwadhibiti
 
Swali fikirishi je ni mkoa gani Tanzania ambao una watu wengi zaidi ukipata jibu mimi kama mfanya biashara nitawekeza huko
Mkoa wenye watu wengi , kaangalie takwimu kabla ya uhuru halafu angalia uwiano wa watu ....Zamani wasomi wengi walihamia Dar kweny chuo kikuu hata viongozi walihamia Dar na kuacha mji yao ...Hii ilitokana na miundombinu mingi kujengwa huko , ikiwa ni pamoja na vyuo na sehemu za biashara .


serikali ilishindwa kufanya ushambazi wa vyanzo vya kiuchumi na kusababisha watu kusambaa sana , utakuja kuona kuna mikoa ilikuwa na watu wengi baadae wahamia kuziendea fursa .....Nyerere alifeli pakubwa hapa ila viongozi wa leo ndio yale yale , wote hawajui wafuatalo .


kwa sasa nenda Dodoma ndio serikali imeelekeza nguvu huko , wanatoa bil 34 kujenga jengo la makumbusho ili mradi tu Dodoma iwe na mejngo mengi .
 
Imekuwa hivyo Kwa sababu tumeshundwa Kuendeleza pale alipoishia.

Hii Nchi inaenda enda tuu haieleweki inataka nini kwenye Maendeleo yake
Waulize CCM chini ya samia. Maana ndo madereva wetu
 
Mkoa wenye watu wengi , kaangalie takwimu kabla ya uhuru halafu angalia uwiano wa watu ....Zamani wasomi wengi walihamia Dar kweny chuo kikuu hata viongozi walihamia Dar na kuacha mji yao ...Hii ilitokana na miundombinu mingi kujengwa huko , ikiwa ni pamoja na vyuo na sehemu za biashara .


serikali ilishindwa kufanya ushambazi wa vyanzo vya kiuchumi na kusababisha watu kusambaa sana , utakuja kuona kuna mikoa ilikuwa na watu wengi baadae wahamia kuziendea fursa .....Nyerere alifeli pakubwa hapa ila viongozi wa leo ndio yale yale , wote hawajui wafuatalo .


kwa sasa nenda Dodoma ndio serikali imeelekeza nguvu huko , wanatoa bil 34 kujenga jengo la makumbusho ili mradi tu Dodoma iwe na mejngo mengi .
Nadhani kwasasa mme elimika vya kutosha hadi mnayaona mapungufu hayo, ndiyo maana nasema tatizo ni jamii, jamii ndiyo inatakiwa ibuni mbinu za kukabiliana na changamoto mkisuburi wanasiasa mtaandika sana humu na kuilaumu serikali bila kupata majibu chanya, ni wanasiasa wachache sana wenye maono na kuthubutu
 
Samia kahamia Arusha , licha ya Dodoma kuwa makao makuu ila naona vikao vyote vimehamia Arusha , hii miji mengine itakuwa lini ?
Hii sio hoja yangu ya msingi Wala Haina impacts yeyote Kwa hoja yangu.

Kinachotakiwa ni Serikali kujenga Majiji mengine Kwenye Kila Kanda.
 
Shida sio mkoloni,bali fikra zetu na matendo yetu,ni aibu kwa taifa lenye umasikini wa kutupwa,kutumia 10T kwenye reli,yalikuwa makosa makubwa sana.Leo hii nimesoma kule X, serikali inampango wa kutumia 34b,kujenga makubusho ya maraisi huu ni upumbavu na uzuzu.
34b kujenga makumbusho ya marais? Unbeleivable , what fuk is this?
 
Nadhani kwasasa mme elimika vya kutosha hadi mnayaona mapungufu hayo, ndiyo maana nasema tatizo ni jamii, jamii ndiyo inatakiwa ibuni mbinu za kukabiliana na changamoto mkisuburi wanasiasa mtaandika sana humu na kuilaumu serikali, ni wanasiasa wachache sana wenye maono na kuthubutu
Wabuni kitu gani sasa , intake ya watu Dar kila mwaka inapokea maelfu ya wanafunzi ...Wanafunzi hao wanabaki baada ya kumaliza chuo ndio wanaongeza shughuli za kiuchumi .

Katika uchumi lazima kuwepo na kitu kinafanya watu wawe na muingiliano , Mikoani wanafanya kilimo ila muingiliano bado mdogo
 
Wabuni kitu gani sasa , intake ya watu Dar kila mwaka inapokea maelfu ya wanafunzi ...Wanafunzi hao wanabaki baada ya kumaliza chuo ndio wanaongeza shughuli za kiuchumi .

Katika uchumi lazima kuwepo na kitu kinafanya watu wawe na muingiliano , Mikoani wanafanya kilimo ila muingiliano bado mdogo
Nini kifanyike, what are the possible solutions
 
We Jamaa ni ngumu kuelewa.Sababu zinazosababishwa mrundikano Dar ndio inatakiwa kujengwa Mikoani japo Jiji Moja Kila Kanda Wala hutoona huo mrundikano
Mbona mikoani watu wapo wengi kwasasa na maisha yao ya kila siku hayategemei dar mfano mimi nina miaka zaidi ya 6 sijaenda dar, the world is at my finger tips
 
Mbona mikoani watu wapo wengi kwasasa na maisha yao ya kila siku haitegemei dar mfano mimi nina miaka zaidi ya 6 sijaenda dar, the world is at my finger tips
Wapi huko ambako hawategemei Dar? Mkoa gani huo?
 
Tumejifunza na kuishi kwenye Maisha ya Historia kwamba Wakoloni Hawakutaka Kupeleka maendeleo kwenye Miji ya maeneo mengine ya Nchi na badala yake wakijenga Jiji Moja tuu kama economic hub ya Uchumi wa kikoloni.

Kwa hapa Tanzania (Tanganyika& Zanzibar), Wakoloni wa Kijerumani na baadae Uingereza walijenga Jiji Moja tuu la Dar kama kitovu Cha uchumi wa kikoloni huku maeneo mengine ya Nchi yakiwa ni mashamba ya uzalishaji wa malighaghafi na manamba Kwa Ajili ya kustawisha uchumi wa kikoloni.

Hata baada ya uhuru wa Tanganyika na Zanzyna hatimage Tanzania, Serikali zimeshindwa kukata Mizizi huo wa Kikoloni Kwa Nchi nzima kutegemea Dar Kwa Kila kitu.

1.Asilimia 90% ya Mapato ya Kodi uanatoka Dar

2.Njia zote za Usafiri na vyombo vya usafiri ni baina ya Mikoani na Kuja Dar na sio Mkoa na Mkoa.eg hakunaga Usafiri wa ndege baina ya Miji ya Nchi isipokuwa kuja Dar halikadhalika na reli.

3.Njia kuu za Uchumi Bado ziko na zinaendelea kuwekeza Dar mfano Bandari,viwanja vya ndege, miundombinu ya usafiri , Miundombinu ya Storage , Taasisi Kuu za kifedha.

4.Huduma za Afya za Kibingwa na Bobezi zote zinapatikana Dar.Licha ya Ukubwa wa Nchi yetu na Wingi wa watu lakini Huduma Zenye hadhi ya Kitaifa mfano Hospitali Zenye kutoa tiba Bobezi zote ziko Dar ,yaani tumeshundwa kujenga hata Kwa Kanda eg MNH,JKIC,Mlonganzila,Maaraba za Tiafa,Mkemia Mkuu wa Serikali nk.

5.Bajeti Kubwa ya Matumizi ya Nchi Kutengwa Kwa Ajili ya Kuendekeza Dar.
Pamoja na Nchi kuendelea kuwa na Uchumi tegemezi Kwa Jiji Moja ila hata matumizi ya Nchi karibia 1/3 yote hutumika kuendekeza Dar eg DMDP 2,BRT Expansion pekee Zina zaidi ya Trilioni 1 Kwa Ajili ya kujenga Barabara za Dar tuu wakati Bajeti ya Tarura ya Nchi nzima haifiki hata hiyo Trilioni 1.

Kwa hali hii sishangai kuona Kuna Mikoa Hadi Leo hii hazijaunganishwa na Lami na Serikali inaona sawa tuu.

Kuendelea Kujenga Nchi ya Utegemezi Kwa Mji mmja haikuwa malengo ya Uhuru Bali ni muendelezo wa sera za Ubaguzi za Kikoloni.

Ikiwa Mikoa itaendea Kuzalisha malighafi Kwa Ajili ya Kuendeleza Dar basi kutakuwa hakuna haja ya kuwa huru.Leo hii Mwanza inaitwa Jiji la Pili Kwa Ukubwa Tanzania lakini ukienda huoni huo Ukubwa badala yake Haina tofauti na Mikoani.

Matokeo ya sera hizo za kikoloni ni kuzidi kuongezeka Kwa gap la umaskini baina ya watu wa Mjini(Dar) na Mamilioni ya watu wa Vijijini (Mkoani).

Ushauri
Kumekuwa na juhudi kiduchu Kwa miaka ya karibuni Kwa Serikali kujaribu kuvifikia Vijiji Ili kupunguza umaskini lakini Tija yake imezidi kuwa ndogo Kwa sababu Bado soko kuu la bidhaa na Huduma zinapatikana Dar hivyo kutoa mwanya Kwa wachuuzi na madalali kujinufaisha Kwa jasho la watu wa Mikoani.

Naishauri Serikali kwamba Ili lengo la kusogeza maendeleo Kwa watu wengi hususani wa Vijijini (Mikoani) , Serikali ijenga walau Majiji Makuu Kwa Kila Kanda ambayo yatakuwa na miundombinu na Huduma kama zinazopagikana Dar Kwa lengo la kuwa na industrial centers Mpya ambazo zitakuwa ndio masoko ya wakulima na production centres.

Kwa kufanya hivyo tutasambaza maendeleo Kwa haraka huko Vijijini na kuondoa au kupunguza utegemezi wa Uchumi na Kila kitu Kwa Dar.Nchi za Ulaya na Asia Hazina Maendeleo Wala uchumi unaotegemea Jiji Moja kama huku Kwetu Tanzania.

Kwamba Leo hii nikitaka Kupeleka mbuzi Oman eti lazima niende Dar Kwa sababu kule ndiko Kuna maabara na ndege au meli za uhakika na sio eneo jingine,Sasa uchumi wa hivi ni muendelezo wa ukoloni.

My Take
Nampongeza Marehemu Magufuli Kwa hatua za makusudi kabisa za Kujenga Dodoma,walau tunaanza kuona Jiji lingine kubwa likizaliwa na ambalo litakuwa economic hub.

Hatua hizi ziendelee Kwa Kujenga Majiji ya Kiuchumi na Biashara Kwa Kila Kanda ambayo yatawekewa miundombinu yote mikubwa ya kiuchumi na kijamii.

Vision 2050 Ilizingatie Hilo jambo Kwa kuwa ndio itakuwa centers za kusogeza maendeleo Kwa haraka Mikoani na Wilayani.

Tanzania sio Dar pekee. Pia soma Kwanini hadi leo makao makuu ya mikoa 18 bado kuunganishwa kwa barabara za lami? Je, ni umasikini, ukubwa wa nchi au ufisadi na kukosa akili?
Huwezi kutoa ushauri wa msukule wa mzee mbowe mlishindwa hata kumnunulia makamamu mwenyekiti gari kwa matumizi ya ofis
 
Back
Top Bottom