Accumen Mo
JF-Expert Member
- May 15, 2022
- 18,036
- 39,882
Sasa ndio mtoe bil 34 ili kuongeza majengo Dodoma , tunataka kila mkoa uwe na hall za mikutano ..Tusikie mwaka huu mkutano mkubwa wa wakuu wa taasisi umefanyika iringa, Manyara , singida , mbeya sio kila siku Arusha tu na Dar .Hii sio hoja yangu ya msingi Wala Haina impacts yeyote Kwa hoja yangu.
Kinachotakiwa ni Serikali kujenga Majiji mengine Kwenye Kila Kanda.
Sasa kama rais muda wote yeye Yuko Dar unategemea nini? Kwa mwaka siku 365, Samia anakaa Dodoma siku zisizozidi 60, siku 300 yuko Dar.Hili la kurudi Sina hakika nalo na Kwa jinsi sheria ilivyowekwa haiwezekani kurudi Dar
Asilimia 90% jmeitoa wapi? Huo ni uongo Dar inachangia asilimia 70% ya makusanyo ila in GPD ya asilimia 17% tu ya nchi nzima!Tumejifunza na kuishi kwenye Maisha ya Historia kwamba Wakoloni Hawakutaka Kupeleka maendeleo kwenye Miji ya maeneo mengine ya Nchi na badala yake wakijenga Jiji Moja tuu kama economic hub ya Uchumi wa kikoloni.
Kwa hapa Tanzania (Tanganyika& Zanzibar), Wakoloni wa Kijerumani na baadae Uingereza walijenga Jiji Moja tuu la Dar kama kitovu Cha uchumi wa kikoloni huku maeneo mengine ya Nchi yakiwa ni mashamba ya uzalishaji wa malighaghafi na manamba Kwa Ajili ya kustawisha uchumi wa kikoloni.
Hata baada ya uhuru wa Tanganyika na Zanzyna hatimage Tanzania, Serikali zimeshindwa kukata Mizizi huo wa Kikoloni Kwa Nchi nzima kutegemea Dar Kwa Kila kitu.
1.Asilimia 90% ya Mapato ya Kodi uanatoka Dar
2.Njia zote za Usafiri na vyombo vya usafiri ni baina ya Mikoani na Kuja Dar na sio Mkoa na Mkoa.eg hakunaga Usafiri wa ndege baina ya Miji ya Nchi isipokuwa kuja Dar halikadhalika na reli.
3.Njia kuu za Uchumi Bado ziko na zinaendelea kuwekeza Dar mfano Bandari,viwanja vya ndege, miundombinu ya usafiri , Miundombinu ya Storage , Taasisi Kuu za kifedha.
4.Huduma za Afya za Kibingwa na Bobezi zote zinapatikana Dar.Licha ya Ukubwa wa Nchi yetu na Wingi wa watu lakini Huduma Zenye hadhi ya Kitaifa mfano Hospitali Zenye kutoa tiba Bobezi zote ziko Dar ,yaani tumeshundwa kujenga hata Kwa Kanda eg MNH,JKIC,Mlonganzila,Maaraba za Tiafa,Mkemia Mkuu wa Serikali nk.
5.Bajeti Kubwa ya Matumizi ya Nchi Kutengwa Kwa Ajili ya Kuendekeza Dar.
Pamoja na Nchi kuendelea kuwa na Uchumi tegemezi Kwa Jiji Moja ila hata matumizi ya Nchi karibia 1/3 yote hutumika kuendekeza Dar eg DMDP 2,BRT Expansion pekee Zina zaidi ya Trilioni 1 Kwa Ajili ya kujenga Barabara za Dar tuu wakati Bajeti ya Tarura ya Nchi nzima haifiki hata hiyo Trilioni 1.
Kwa hali hii sishangai kuona Kuna Mikoa Hadi Leo hii hazijaunganishwa na Lami na Serikali inaona sawa tuu.
Kuendelea Kujenga Nchi ya Utegemezi Kwa Mji mmja haikuwa malengo ya Uhuru Bali ni muendelezo wa sera za Ubaguzi za Kikoloni.
Ikiwa Mikoa itaendea Kuzalisha malighafi Kwa Ajili ya Kuendeleza Dar basi kutakuwa hakuna haja ya kuwa huru.Leo hii Mwanza inaitwa Jiji la Pili Kwa Ukubwa Tanzania lakini ukienda huoni huo Ukubwa badala yake Haina tofauti na Mikoani.
Matokeo ya sera hizo za kikoloni ni kuzidi kuongezeka Kwa gap la umaskini baina ya watu wa Mjini(Dar) na Mamilioni ya watu wa Vijijini (Mkoani).
Ushauri
Kumekuwa na juhudi kiduchu Kwa miaka ya karibuni Kwa Serikali kujaribu kuvifikia Vijiji Ili kupunguza umaskini lakini Tija yake imezidi kuwa ndogo Kwa sababu Bado soko kuu la bidhaa na Huduma zinapatikana Dar hivyo kutoa mwanya Kwa wachuuzi na madalali kujinufaisha Kwa jasho la watu wa Mikoani.
Naishauri Serikali kwamba Ili lengo la kusogeza maendeleo Kwa watu wengi hususani wa Vijijini (Mikoani) , Serikali ijenga walau Majiji Makuu Kwa Kila Kanda ambayo yatakuwa na miundombinu na Huduma kama zinazopagikana Dar Kwa lengo la kuwa na industrial centers Mpya ambazo zitakuwa ndio masoko ya wakulima na production centres.
Kwa kufanya hivyo tutasambaza maendeleo Kwa haraka huko Vijijini na kuondoa au kupunguza utegemezi wa Uchumi na Kila kitu Kwa Dar.Nchi za Ulaya na Asia Hazina Maendeleo Wala uchumi unaotegemea Jiji Moja kama huku Kwetu Tanzania.
Kwamba Leo hii nikitaka Kupeleka mbuzi Oman eti lazima niende Dar Kwa sababu kule ndiko Kuna maabara na ndege au meli za uhakika na sio eneo jingine,Sasa uchumi wa hivi ni muendelezo wa ukoloni.
My Take
Nampongeza Marehemu Magufuli Kwa hatua za makusudi kabisa za Kujenga Dodoma,walau tunaanza kuona Jiji lingine kubwa likizaliwa na ambalo litakuwa economic hub.
Hatua hizi ziendelee Kwa Kujenga Majiji ya Kiuchumi na Biashara Kwa Kila Kanda ambayo yatawekewa miundombinu yote mikubwa ya kiuchumi na kijamii.
Vision 2050 Ilizingatie Hilo jambo Kwa kuwa ndio itakuwa centers za kusogeza maendeleo Kwa haraka Mikoani na Wilayani.
Tanzania sio Dar pekee. Pia soma Kwanini hadi leo makao makuu ya mikoa 18 bado kuunganishwa kwa barabara za lami? Je, ni umasikini, ukubwa wa nchi au ufisadi na kukosa akili?
Unaweza kuuliza hata kuhamia huko Dodoma kuna mantiki ipi ? Vikao kila siku wanakaa Arusha na Dar ....Wangeacha tu kupeleka majengo mengi huko ...kila wizara ikae kikanda sio lazima zote zikae Dodoma maana mambo ni yale yale ya kwenda Nje ya mkoa kufanya semina.Sasa kama rais muda wote yeye Yuko Dar unategemea nini? Kwa mwaka siku 365, Samia anakaa Dodoma siku zisizozidi 60, siku 300 yuko Dar.
Taasisi nyingi za serikali bado zina ofisi Dar, nyingi zimehamia Dodoma kisiasa, unakuta mkurugenzi tu ndio ana ofisi Dodoma huku operation wote wako Dar. Hata gharama za uendeshaji wa serikali umekua wa gharama sana kwa sababu watu siku zote wako intransit, Dodoma, Dar.
Ni changamoto sana.
Siku zote nimekua najiuliza why wizara ya kilimo iwe Dar wakati kilimo kinafanyika Mbeya, Iringa, Katavi, Rukwa, Ruvuma na mikoa mingine?Unaweza kuuliza hata kuhamia huko Dodoma kuna mantiki ipi ? Vikao kila siku wanakaa Arusha na Dar ....Wangeacha tu kupeleka majengo mengi huko ...kila wizara ikae kikanda sio lazima zote zikae Dodoma maana mambo ni yale yale ya kwenda Nje ya mkoa kufanya semina.
Unaweka vip TPA makao makuu yakae Dodoma , mbona wizara ya utalii ina jengo kule Arusha? Wekeni hata wizara ya uvuvi pale kanda ya ziwa ....wizara ya kilimo kule Mbeya ..Mmbo ya Anga wekeni hata pale kilimanjaro .
Upigaji mtupu , huo mji wa Dodoma wanataka wawekeze huko wafanye biashra , maisha yatakuwa juu ....Siku zote nimekua najiuliza why wizara ya kilimo iwe Dar wakati kilimo kinafanyika Mbeya, Iringa, Katavi, Rukwa, Ruvuma na mikoa mingine?
Wizara ya Madini ikae Dar wakati uchimbaji uko kanda ya ziwa? Wizara ya Ulinzi inafanya nini Dar. Mifuko ya hifadhi za jamii inafanya nini Dar. Concentration ya taasisi na idara za serikali sehemu moja ndio inaleta huu ujinga.
Mimi habari ya Nyerere iliyonisikitisha sana ni ile ya yeye kubomoa mifumo ya uongozi ya vyama vya ushirika na serikali za mitaa ili kuua autonomy ya taasisi hizo kwa vile zilikuwa na nguvu sana; zilikuwa zikipambana na serikali kuu kuzuia kuingiliwa kwa madaraka yao kiholela.Umenikumbusha usemi wa ndugunaization, kwasasa itakuwa ccmnaization ama uchawanaization, kitaalamu tunaita unyumbu wa kisiasa.
Unyumbu wa kisiasa ni tabia ya watu wanao pewa dhamana kuahirisha kufikiri kwa nafsi kwasababu ya kujipendekeza, kulitumikia kundi fulani kwa masilahi binafsi ama uoga kwa viongozi wao bila utii, (unafiki), a.k.a kujizima data neno zuri zaidi ni kuahirisha kufikiri kizalendo
Saluni nzuri ziko Dar ulitaka akae Dodoma?Magufuli alitaka kuijenga Dodoma angalau kupunguza congestion Dar es Salaam lakini Samia yeye amemua kurudi Dar. Ni changamoto sana.
Hebu jiulize kiwanda kama General tyre cha Arusha mpaka Leo Kipo pale kama gofu.unajiuliza ni nini kinazuia kukifufua na matairi ni biashara ya uhakika na mpira tunauwezo wa kulima.Yaani ni kama kuna li mzimu mkubwa umesimama mbele yeti unasema "Bakia hapohapo"Mwalimu Nyerere alisambaza viwanda sehemu mbalimbali kama Moprocco na Canvas Morogoro, kiltex na bia ,Arusha, Chuma na Mbolea Tanga, Tanbond na Super Ghee Mwanza na kadhalika.
Siku hizi viwanda vyote ni Dar,Bagamoyo na Pwani kwa ujumla sababu Dar imejaa na huko ni karibu nayo.
Kwa hali hii Dar itaendelea kuwa mlipaji Kodi mkubwa na Kamwe Dodoma haitaifikia hata mama Kila siku yupo Dar.
Unadhani wafanyabiashara walijenga Jiji la Dar Kwa bahati mbaya? Jibu ni hapana ni Kwa sababu Serikali imeweka incentives zote hapo Dar,nani aende Mikoani ambako hakuna hizo incentives?Mleta mada waweza kuwa na hoja lakini kulaumu serikali sio sahihi
Mfano wajenzi wa jiji la Dar es salaam City ni wafanyabiashara binafsi
Majengo yote makubwa ya biashara unayoaona Dar asilimia kubwa waliojenga ni wahindi na waarabu walioanzisha makazi yao na biashara Dar
Serikali haijengi miji wala vijiji wananchi wenyewe kwa shughuli za kiuchumi ndio hujengq miji ndio unakuta jiji kama kahama au mji wa Geita limeibuka sababu hiyo
Mji huibuka kwa kuanzia ni kuwa trade centre ndivyo hata majiji yote duniani yaliibuka hivyo yawe London, Paris,nk haikujengwa na serikali kuwa majiji
Maabara ya Taifa ya Kilimo ziko Dar na Sasa Dom na taasisi zingine zinazofanana na hizo zinazojihusisha na Kilimo,uvuvi nk.Siku zote nimekua najiuliza why wizara ya kilimo iwe Dar wakati kilimo kinafanyika Mbeya, Iringa, Katavi, Rukwa, Ruvuma na mikoa mingine?
Wizara ya Madini ikae Dar wakati uchimbaji uko kanda ya ziwa? Wizara ya Ulinzi inafanya nini Dar. Mifuko ya hifadhi za jamii inafanya nini Dar. Concentration ya taasisi na idara za serikali sehemu moja ndio inaleta huu ujinga.
Mara zote sio mara Moja Moja, sijawahi andika pumba.Kumbe mara moja moja unatoaga hoja za maana,hongera sana.