Miaka Zaidi ya 60 Baada ya Uhuru,Tanzania Imeshindwa Kuondoa Mizizi ya Ukoloni Kwa Nchi kuwa tegemezi wa Uchumi na Mapato Kwa Jiji Moja tuu la Dar

Kwa Sasa Wana mantiki na hoja kwamba Bado miundombinu yote weseshi haijatengamaa Kwa Dodoma so wanalazimika kuendelea kuzurura Dar na Arusha.

Hoja ya msingi ni Je hiyo miundombinu inavyotakiwa huko Mji Mkuu inajengwa?
 
Sasa kama Mapato zaidi ya 70% inategemea mJi mmja wewe unaona ni Afya kiuchumi Kwa Nchi yenye watu zaidi ya mil.65?
 
Sasa ndio mtoe bil 34 ili kuongeza majengo Dodoma , tunataka kila mkoa uwe na hall za mikutano ..Tusikie mwaka huu mkutano mkubwa wa wakuu wa taasisi umefanyika iringa, Manyara , singida , mbeya sio kila siku Arusha tu na Dar .
Ukiwa na Uchumi mdogo unaenda hatua Kwa hatua ndio maana napendekeza tuanze kujenga Majiji ya Kikanda ,Yako mature na kuanza kuwa chaos tunasogeza Huduma Mikoani hivyo hivyo.

Ila kwenda kiujimla.jumla na Kienyeji kienyeji ndio maana hakuna tulichofaulu Kwa usahihi Toka Uhuru
 
Shida Yako ni Nini kama Dar 90% ya makusanyo yanatoka Dar na dar inaambulia angalau 20% ya maku sanyo hayo Sasa shida Iko wapi!?
 
Sasa kama Mapato zaidi ya 70% inategemea mJi mmja wewe unaona ni Afya kiuchumi Kwa Nchi yenye watu zaidi ya mil.65?
Haya mambo yako dunia nzima kuna commercial centre kubwa ambazo huwa na mapato mengi kuliko sehemu nyingine mfano Rwanda Kigali ndipo asilimia kubwa ya mapato ya nchi hutoka ukienda Kenya Nairobi ndio inaongoza kwa mapato makubwa kuliko hata mombasa kwenye bandari

Ukienda Uganda Kampala ndio inaongoza

Sio kitu cha ajabu hicho
 
Imekuwa hivyo Kwa sababu tumeshundwa Kuendeleza pale alipoishia.

Hii Nchi inaenda enda tuu haieleweki inataka nini kwenye Maendeleo yake
Umeongea ukweli mtupu.
Ila umeshindwa kusema wazi, CCM ndiyo imetufikisha hapa.

Tunahitaji mawazo mapya toka kwa watu wapya na taasisi mpya(chama).
Hii italeta ushindani katika uwajibikaji.
Vinginevyo tutabaki kama tulivyoanza milele yote.
 
Dunia nzima wapi huko? Kwa hiyo huko Dunia nzima ndiko 80% ya Mapato zinatoka kwenye Mji mmja?

Huu ni ujinga wa hapa Tanzania na Vinchi vingine vya mlengi wa kikoloni kama Uganda.

Hata hivyo Kwa Uganda ni Uongo,Entebe pale Kuna Airport ya Kimataifa inaongoza pesa nyingi kushinda Kampala.

Mwisho kinachotakiwa ni kupunguza utegemezi wa Kila kitu kwenye Mji mmja,walaui iwe chini ya 40% .

Vinginevyo siku mkipogwa mabomu hapo Nchi yote Iko paralysed.
 
Kumbe wewe jamaa unajitoaga tu akili.Umeandika jambo la msingi sana huu ndo tafsiri sahihi ya maana ya kufungua nchi.sio ile tafsiri nyingine mnayoisifiaga.
 
Kumbe wewe jamaa unajitoaga tu akili.Umeandika jambo la msingi sana huu ndo tafsiri sahihi ya maana ya kufungua nchi.sio ile tafsiri nyingine mnayoisifiaga.
Wala sijajitoa akili,Kila siku Huwa naandika Madini
 
Serikali kujaribu kuvifikia Vijiji Ili kupunguza umaskini lakini Tija yake imezidi kuwa ndogo Kwa sababu

Sababu kubwa ni mhimili wa executive *serikali kuu mizizi yake kuingia katika kuzuia majadiliano huru katika mhimili wa Bunge na mhimili wa Mahakama bila kusahu mhimili wa 4 Vyombo vya habari kutekwa nyara na walio madarakani.

Unasikia kuwa makao makuu ya Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA kuhamishiwa Dodoma. Shirika la Reli Tanzania TRC ilitakiwa makao yake makuu, karakana n.k yawe Tabora katika kitovu cha muunganiko wa vipande vya reli kuelekea Kigoma Rwanda, DR Congo, Mwanza na DSm.
Mji wa Mbeya ukitakiwa iwe makao makuu ya TAZARA ili kuwa karibu na Zambia na Lubumbashi DRC kufukuzia fursa kwa ukaribu. Iringa ingekuwa TANROADS makao yao. Bukoba vyuo vikuu vyote vingejichimbia huko kwa maprofesa n.k

Mfano sasa hivi badala ya Mahakama Judiciary kuhamia Dodoma mhimili huu ungehamishiwa Arusha kuwa karibu na korti ya kikanda na kimataifa hivyo majaji pamoja na jaji mkuu kuwa mbali


Bunge la Jamhuri ya Muungano lingekuwa Unguja huku Dodoma ni mji mkuu wa serikali ya Muungano wakati Dar es Salaam iwe mji mkuu wa serikali ya Tanganyika.

Kwa mgawanyo huu ungesambaza keki ya Taifa na kuvutia uwekezaji Dodoma, Arusha, Unguja na Dar es Salaam n.k

Sumbawanga iwe makao makuu ya utafiti wa kilimo, maeneo mapya ya ranchi kubwa za mifugo, mashamba makubwa ya kilimo cha biashara yaunganishe miji ya Mbeya, Sumbawanga, Mpanda, Kasulu, Kigoma hadi Mutukula kwa barabara na reli.

Kusini Lindi, Mtwara na Ruvuma uwekezaji mzito wa gesi, makaa ya mawe, umeme na kilimo kikubwa.

TOKA MAKTABA :
KURUDISHA UHURU WA MIHILIMI MITATU YA DOLA TANZANIA, KATIBA ITAMKE KILA MHIMILI UWE NA MAKAO YAKE KTK MIJI TOFAUTI

Dodoma ibaki kuwa makao ya serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Dar es Salaam iwe makao makuu ya serikali ya serikali ndogo ya Tanganyika ili muhimili wa dola usiote tena mizizi mpaka ndani ya mhimili wa Bunge kama ilivyokuwa wakati wa awamu ya tano Bunge kumezwa na mhimili wa dola.

Mji wa Arusha uwe makao makuu ya mhimili wa Mahakama Kuu ili jaji mkuu na mahakama ya rufani wabaki huko mbali siyo kila siku wanahudhuria hafla za wafanyakazi wa serikali kuu na mikoa wakiapishwa na kwa namna hii ya mgawanyo wa mihimili, Mahakama iwe huru toka minyororo na jinamizi lililoundwa ktk awamu ya tano. Arusha ni makao ya korti ya Afrika Arusha | Search Results | African Court on Human and Peoples' Rights , EACJ www.eacj.org , UN Korti za masuala ya maovu dhidi ya binadamu International Residual Mechanism for Criminal Tribunals May Conclude Most Cases by May 2021, Its President Tells Security Council | Meetings Coverage and Press Releases hivyo Mahakama Kuu ya Tanzania na Jaji Mkuu wa Tanzania Judiciary of Tanzania | Home watakuwa wanabadilisha mawazo na wasomi wenziwe kuhusu namna bora ya Mahakama za Tanzania kujiendesha kwa uhuru na kumaliza mrundikano wa kesi kwa kuwa kila siku wanahudhuria hafla zote za mhimili wa serikali .


The Many Capitals of South Africa​

South Africa's three capital cities are strategically placed throughout the country, each hosting a separate segment of the nation's government. When asked about a single capital, most people would point to Pretoria.


  • Pretoria is the administrative capital. It is home to the executive branch of the South African government, including the President of the Cabinet. The city also hosts many departments of government and foreign embassies.
  • Located in the province of Gauteng, Pretoria is in the northeast part of South Africa and near the city of Johannesburg.
  • Cape Town is the legislative capital. It is home to the country's legislative parliament, including the National Assembly and National Council of Provinces.
  • Located in the southwest corner of South Africa in the province of Western Cape, Cape Town is the second-largest city in population.
  • Bloemfontein is considered the judicial capital. It is home to the Supreme Court of Appeal, the second-highest court in South Africa. The Constitutional Court (the highest court) is located in Johannesburg.
  • Located in the province of Free State, Bloemfontein is in the center of South Africa.
 
Ishu sio kuongoza ishu ni asilimia zikiwa kubwa sana kwa mji mmoja haileti afya ,angalia south africa joburg inaongoza lakini haifiki hata asilimia 60 ya mapato ya nchi
 
Ishu sio kuongoza ishu ni asilimia zikiwa kubwa sana kwa mji mmoja haileti afya ,angalia south africa joburg inaongoza lakini haifiki hata asilimia 60 ya mapato ya nchi
Ni Aibu na jambo la ajabu Nchi kutegemea 80% ya Mapato kutoka Mji mmja.
 
Ni CCM Ndio wameshindwa sio nchi dogo.

Kama Wasira bado yuko kwenye safu ya Uongozi unategemea kitu kipya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…