Miami International Boat Show -Maonyesho makubwa ya boti duniani

Miami International Boat Show -Maonyesho makubwa ya boti duniani

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2018
Posts
5,489
Reaction score
14,091
Miami International Boat Show ni maonyesho makubwa ya boti na vifaa mbalimbali vya majini. Mashindano haya hufanyika katika mji wa Miami huko Marekani na kukutanisha makampuni ya utengenezaji boti,injini za boti,wamiliki wa boti,kampuni za magari na watazamaji wa kawaida.

Kwa upande mwingine hii unaweza ukaita utalii wa boti.

Kwa marekani maonyesho ya Fort Lauderdale International Boat Show katika mji wa California ndio yana eneo kubwa na yanatambulika makubwa ila haya ya Miami ndio yenye kuvutia watu wengi duniani na hutazamwa na wengi.
Hili ni jukwaa la watazamaji na sehemu ya maegesho ya boti.

images.jpeg

images (2).jpeg

USHINDANI
Makampuni makubwa ya kutengeneza boti yamekuwa yakijitahidi kutengeneza boti zenye kasi,nguvu na luxury ili waweze kuibuka vinara na kufanya vizuri kwenye soko. Haya mashindano yamekuwa chachu ya kugunduliwa kwa technology za kisasa.

MAKAMPUNI YA MAGARI NAYO HAYAPO NYUMA
Kampuni mbalimbali za magari nazo zimeingia kushiriki kwa kupitia timu zinazoshiriki au kuingia moja kwa moja.

1.Mercedes Benz
Hawa wamekuwa wakitengeneza boti zenye kasi ila kwenye Miami International boat show huwa wanaingia kwenye Cigarette Team AMG.
ob_419d26_mercury-marine-miami-2.JPG

2. Toyota Lexus Yatch LY650
Hawa nao wametengeneza Yatch kushirikiana na kampuni ya Marquis Yacht na kuunda boti ya kifahari yenye urefu wa futi 65 na kutumia injini za Volvo Penta.

Makampuni mengine yaliyotengeneza boti za kifahari na kasi ni BMW kushirikiana na wabrazili,Audi,Ferrari, Honda,Volvo na Lamborghini.

Kampuni ambazo hufanya vizuri kwenye 10 bora katika mashindano ni Yamaha,Seven Marine,Envirude,Suzuki,Torpedo, Boston Whale na Sea Ray.

ob_6fd731_mercury-marine-miami-6.JPG

ob_05d4ea_mercury-marine-miami-3.JPG

MASHINDANO MENGINE
Licha ya hayo mashindani kuna London Boat show, Monaco Boat show, Dubai Boat show, Japan Boat Show na Australia Boat Show.

Mashindano haya hutumia muda wa wiki moja katika maonyesho ya boti ya kifahari,boti zenye nguvu,boti zenye spidi na ubunifu.Miami Boat Show imeonekana tiketi zake kuwa na being kwa watazamaji kati ya USD150 mpaka 180 kwa mtu mzima kwa siku.
 
Mashindano ya mitumbwi hayafanyiki tena siku hizi, sijui kwanini TBL hawayadhamini tena
Tanzania tulikuwa na Mashindano ya mitumbwi, naona baada ya TBL kuacha kudhamini yakafa.

Michezo ya majini tupo nyuma sana, mwaka juzi kuna mtanzania alienda ughaibuni kucheza mashindano ya mashua akarudi mtupu.Hakupata hata sapoti yeyote hats mwalimu hakuwa naye.
 
Mashindano ya mitumbwi hayafanyiki tena siku hizi, sijui kwanini TBL hawayadhamini tena
Wenzetu Thailand kupitia michezo ya boti na mitumbwi ya mbao wapo mbali sana. Wanafanya modifications za kuweka injini za water pump,power tiller na magari kwenye mitumbwi yao ya mbao na inawasaidia katika uvuvi.
 
Offshore Seamen

Mashindano ya mitumbwi hayafanyiki tena siku hizi, sijui kwanini TBL hawayadhamini tena
Mwanza kuna mzee alifanya modifications za kuweka injini ya Land Rover 109 kwenye boti ya mbao na anabeba abiria huko visiwani.
Na mwingine alitengeneza boti ya mbao na kuwekea injini ya Corolla.
Hata Msasani boats, boti zao zina engine za magari, zinatoa huduma 6a kwenda na kurudi Bongoyo kutokea Slip Way
 
Mashindano ya mitumbwi hayafanyiki tena siku hizi, sijui kwanini TBL hawayadhamini tena
Hata Msasani boats, boti zao zina engine za magari, zinatoa huduma 6a kwenda na kurudi Bongoyo kutokea Slip Way
Pale Slip way kuna vyombo hasa kuna boti zina injini zenye mpak 250Hp na kuendelea.

Saizi kwa wenye injini za gari tuna project tunakutengenezea boti kisha injini yako yoyote ya gari inawekewa gearbox ya marine (ZF gearbox) na mfumo wa jet propulsion.
 
Kwa sasa akitokea mdhamini wa mashindano ya boti kwa Dar. Akiweka umbali wa Slip way kwenda Bongoyo au Slip way-Zanzibar kuna vyombo vitafanyiwa modifications Dar-Zanzibar rekodi inawekwa ya kutumia muda mfupi.
 
Kwa yeyote anaye hitaji kutengenezewa boti za kisasa kwa ajili ya matumizi mbalimbali anaweza akanicheki.

Material ya kutengenezea ni fiber glass,wood na aluminium. Kulingana na hitaji lako.

Injini unaweza kuwekea ya kuagiza toka German au Japan. Na mifumo ya kusukuma si propela ni Jet.Kama una injini ya gari unaweza ukaitumia pia kitacho
ongezwa ni marine gearbox na jet systems.

Sehemu za utengenezaji ni Dar,Tanga,Zanzibar pia popote ulipo boti inaweza ikatengenezewa kutokana na oda.
 
Mkuu Bujibuji karibu uangalie michezo ya pikipiki hapa Tanganyika Packers. Uje utupe na namba za BMW ili jioni vijana waigonge wapate ela.
 
Kwa yeyote anaye hitaji kutengenezewa boti za kisasa kwa ajili ya matumizi mbalimbali anaweza akanicheki.

Material ya kutengenezea ni fiber glass,wood na aluminium. Kulingana na hitaji lako...

Mkuu o boti kubwa ya Uvuvi kwa fibreglass ni sh ngapi?
 
Tuseme upana mita 15 halafu urefu mita arobaini
Vipimo hivyo viwe kwenye foot ikiwa kwa mita huo upana ni mkubwa sana. Na kwa urefu wa mita 40 boti ya fiber glass haitokuwa imara. Mita 40 si haba urefu wa meli au unaitafuta nusu ya uwanja wa mpira.
 
Kikawaida boti zetu huwa zinabeba wavuvi 50

Sasa sijajua wewe size ya boti ya kubeba wavuvi 50 inakuwa size ipi
 
Kwa yeyote anaye hitaji kutengenezewa boti za kisasa kwa ajili ya matumizi mbalimbali anaweza akanicheki.

Material ya kutengenezea ni fiber glass,wood na aluminium. Kulingana na hitaji lako.

Injini unaweza kuwekea ya kuagiza toka German au Japan. Na mifumo ya kusukuma si propela ni Jet.Kama una injini ya gari unaweza ukaitumia pia kitacho
ongezwa ni marine gearbox na jet systems.

Sehemu za utengenezaji ni Dar,Tanga,Zanzibar pia popote ulipo boti inaweza ikatengenezewa kutokana na oda.
Weka no ya simu tafadhali
 
Back
Top Bottom