Offshore Seamen
JF-Expert Member
- Mar 9, 2018
- 5,489
- 14,091
Miami International Boat Show ni maonyesho makubwa ya boti na vifaa mbalimbali vya majini. Mashindano haya hufanyika katika mji wa Miami huko Marekani na kukutanisha makampuni ya utengenezaji boti,injini za boti,wamiliki wa boti,kampuni za magari na watazamaji wa kawaida.
Kwa upande mwingine hii unaweza ukaita utalii wa boti.
Kwa marekani maonyesho ya Fort Lauderdale International Boat Show katika mji wa California ndio yana eneo kubwa na yanatambulika makubwa ila haya ya Miami ndio yenye kuvutia watu wengi duniani na hutazamwa na wengi.
Hili ni jukwaa la watazamaji na sehemu ya maegesho ya boti.
USHINDANI
Makampuni makubwa ya kutengeneza boti yamekuwa yakijitahidi kutengeneza boti zenye kasi,nguvu na luxury ili waweze kuibuka vinara na kufanya vizuri kwenye soko. Haya mashindano yamekuwa chachu ya kugunduliwa kwa technology za kisasa.
MAKAMPUNI YA MAGARI NAYO HAYAPO NYUMA
Kampuni mbalimbali za magari nazo zimeingia kushiriki kwa kupitia timu zinazoshiriki au kuingia moja kwa moja.
1.Mercedes Benz
Hawa wamekuwa wakitengeneza boti zenye kasi ila kwenye Miami International boat show huwa wanaingia kwenye Cigarette Team AMG.
2. Toyota Lexus Yatch LY650
Hawa nao wametengeneza Yatch kushirikiana na kampuni ya Marquis Yacht na kuunda boti ya kifahari yenye urefu wa futi 65 na kutumia injini za Volvo Penta.
Makampuni mengine yaliyotengeneza boti za kifahari na kasi ni BMW kushirikiana na wabrazili,Audi,Ferrari, Honda,Volvo na Lamborghini.
Kampuni ambazo hufanya vizuri kwenye 10 bora katika mashindano ni Yamaha,Seven Marine,Envirude,Suzuki,Torpedo, Boston Whale na Sea Ray.
MASHINDANO MENGINE
Licha ya hayo mashindani kuna London Boat show, Monaco Boat show, Dubai Boat show, Japan Boat Show na Australia Boat Show.
Mashindano haya hutumia muda wa wiki moja katika maonyesho ya boti ya kifahari,boti zenye nguvu,boti zenye spidi na ubunifu.Miami Boat Show imeonekana tiketi zake kuwa na being kwa watazamaji kati ya USD150 mpaka 180 kwa mtu mzima kwa siku.