Michango kuwanusuru viongozi: CHADEMA imekubali hatia?

Michango kuwanusuru viongozi: CHADEMA imekubali hatia?

Interest

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2015
Posts
3,434
Reaction score
7,072
Hili jambo linafikirisha.

Nimefuatilia mwenendo wa kesi ya mauaji ya Akwilina tangu mwanzo mpaka hukumu yake iliyotolewa leo katika Mahakama ya Kisutu, Dar.

Kukubali kulipa faini bila kukata rufaa, ni kwamba viongozi na wafuasi wa CHADEMA wamekubaliana na hukumu kwamba wanayo hatia ya kusababisha kifo cha Akwilina?

Je, ingeamuliwa wafungwe jela wasingekata rufaa? Au pesa imeonekana ni rahisi kupatikana kuliko jaribio la kutokukubaliana na hatia? Hawajali rekodi itakuwaje?

Ni jambo jema kuchangisha umma na kuomba wanachama na wananchi wenye huruma kuwanusuru, lakini inafikirisha sana.

Kwa mwenendo huu, mahakama si inaweza kuanza kutumika kama chanzo kipya cha mapato?

Kwangu hili suala limekaa kibinafsi sana!
 
Wamesema watakata rufaa!Huna information halafu unaandika uzi!Au ulitaka wakate rufaa huku wakitumikia kifungo?Unaweza kukuta hukumu ya rufaa inatoka kifungo kimeisha!
Ni jambo jema kama wamesema. Unayo hiyo taarifa yao tuione?

Kwa sasa ninachoona kinasambazwa ni makusanyo ya michango kila kona. Hata mimi nimechangia kwa nia njema.

Halafu, kama wanakata rufaa huku wanaendelea kuchangisha pesa maana yake si wamekubali kulipa faini? Unalipaje faini kwa kosa ambalo hukutenda?

Naomba unieleweshe hapo.
 
Mtoa mada ipo hivi hukumu iliyotolewa leo haiwezi kutenguliwa kwa kusudio la mshtakiwa kukata rufaa!! Kisheria hukumu huwa inatekelezwa huku taratibu za rufaa zikiendelea!!

Hukumu ya awali itabatilishwa na hukumu ya mahakama ya juu zaidi kwenye shauri hilo!! Ndipo utekelezaji wa adhabu ya awali hukomea hapo
 
Interest,
Sasa tuseme wanakata rufaa,unadhani hiyo rufaa itakuwa inasikilizwa wakiwa nje au wakiendelea kutumikia adhabu?Maana yake wasipolipa inahesabiwa kwamba wamechagua kifungo hivyo wanakwenda jela!Hata wakikata rufaa,wataendelea kusubiri rufaa yao huku wakitumikia kifungo!

So best option ni kulipa ambapo wakishinda rufaa hela inarudishwa kuliko kutolipa na kukata rufaa,maana yake hata ukishinda rufaa basi utakuwa umeshasota na hakuna fidia yoyote unaweza ipata!

Kwa taarifa ya kukata rufaa,angalia humu humu JF ipo!Viognozi wameongea na waandishi wa habari baada ya hukumu!
 
Kulipa faini ni kukubali kosa, maana yake wamekutwa na jinai ivyo ubunge udiwani wasahau

Fafanua hapo sheria inasemaje? Usitake kuwaingiza members kichakani.
 
Tuweke ubinafsi na uvyama pembeni, bali tutangulize utu. Wananchi wenyewe ndio wameanza kuhamasishana kupitia mitandao, CHADEMA wakabariki hilo. Hata CCM pia wameliona hili:
Screenshot_20200311-071723.png


Michango iliyochangwa wakati wa majanga ya kuzama vivuko na Tetemeko, pesa hiyo haikupita BOT wala haikukaguliwa.

Tulishuhudia Raisi akibadili matumizi ya pesa hizo wakati zilichangwa na raia wema ili ziwasaidie wahanga.

Sasa leo CHADEMA inaonekana eti inakiuka sheria kuomba mchango kwa wananchi. Ewe mpenda haki na demokrasia, usisite kutoa mchango wa chochote hata kama ni sh. 1000/=. Tone na tone hujaza ndoo. Tukipatikana watu laki 350,000 tukachangia elfu 1000 kwa kila mmoja, mbona mapema tu ndoo inajaa?

MBONA RAISI KAMTUMA KABUDI AENDE KUOMBA MCHANGO WA ELIMU KWA TRUMP NA WB?
 
Back
Top Bottom