Michango makanisani chanzo umaskini

Michango makanisani chanzo umaskini

Zero Competition

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2018
Posts
347
Reaction score
553
Hivi ushawahi kujiuliza kwanini siku hizi michango makanisani imekuwa mingi kuliko miaka ya zamani ??

Siku hizi kumekuwa na michango mingi sana makanisani kiasi kwamba hupelekea baadhi ya waumini kuacha kuhudhuria makanisani kwaajiri ya ibada

Halafu Kuna tabia moja imezuka kwamba inapotokea muda wa kutoa sadaka mnalazimishwa na wasimamizi kwamba mwende tu mbele mkapite kisha mrudi kukaa. Zamani kama ulikuwa huna sadaka ulikuwa unaweza ukakaa tu kwenye benchi pasipo kufika pale mbele lakini siku hizi hali imekuwa tofauti kdg ambapo wasimamzi hulazimisha waumini kupita pale mbele kwenye kikapu hata kama hauna sadaka sasa hii ni kama vile kuaibishana.

Imefikia wakati tunaona makanisa kama kituo cha polisi mana ukitaka kuhudhuria unatakiwa ujipange kwelikweli na michango

Wewe kama mdau wa JmiiForums unalizungumziaje suala hili ?
 
Anzisheni makanisa yenu makao makuu yawe Africa...michango yenu ibaki Africa na mjenge himaya zenu Africa... vinginevyo michango yenu inajenga empire za watu.... makanisa yatendelea kumilikiwa na wenyewe...
 
Hili nalo neno
 
Utakufa watakuja kukuombea usamehewe dhambi zako na uende peponi, Mwanao atarithi hiyo dini naye ataenda kanisani atatoa sadaka mwishoni naye atakufa lakini wamiliki wa Kanisa wapo Ulaya na documets zote za makanisa... Na viongozi huko ni Wazungu...
 
Dah hao jamaa wanachoboa mahubiri yao siku hizi ni kutoa tu, mtu anazunguka anaanzia mbali ataokoteza vifungu vya biblia lakini mwisho wa siku point ni kutoa hela.

Hakuna tena mahubiri ya kuhamasisha upendo baina ya watu, kutenda mema na mengine yanayofanana na hayo.

Mi napenda ndugu zetu waislamu, mawaidha yao ni yao siku zote wanahubiri upendo , aman na kukataa dhuluma. Kama kuna mchango wowote basi wataenda direct kwenye point.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utakufa watakuja kukuombea usamehewe dhambi zako na uende peponi, Mwanao atarithi hiyo dini naye ataenda kanisani atatoa sadaka mwishoni naye atakufa lakini wamiliki wa Kanisa wapo Ulaya na documets zote za makanisa... Na viongozi huko ni Wazungu...
Daah hatari sana aisee
 
Michango makanisani sio umaskini ndio kujitegemea kwenyewe huko labda nikupe maana ya kizungu ili usione tabu " donations".

Miaka ya nyuma makanisa "mama" yalikua yanatoa fedha ili kuendesha makanisa ya hapa nyumbani.

Kwa sasa hakuna misaada tena ndio maana tunapaswa kuchangia.

Serikali nayo iachane na maswala ya kuendesha nchi kwa kutegemea misaada.

Tumeweza kwenye makanisa tuende mpaka na serikalini huko.

Tujitegemee.
 
Kuna mzee mmoja wa kanisa aliwahi kuongea kipindi kilee but it was out of 🎤, "yaani sadaka zimepungua sana, wachungaji wanalalamika mzee kabana sana"

Juzi alilopoka "angalau hivi sasa watu wanatoa sana na mibaraka inaonekana"
 
Nimecheka juu ya mada zinazoendelea kwenye hii jamii forum
Sipo upande wowote na nachukia sana udini ukabila ktk maisha yangu
Narudi kwenye hoja sasa!
Mtoa mada anasema kuna watu wapo ulaya wao wanapokea tuu sadaka kutoka kwa nchi zetu au makanisa yaliyopo Afrika si kweli kwanza ajitathimini maana yupo na uzima tele
Inaonekana hajawahi kuwa na mgonjwa akalazwa bugando?(Roman)au
Akalazwa KCMC? (Lutheran)au
Hana mtoto anayeaoma alharamain/kinondoni Muslim?(Islamic)
Afikirie hapo then aje na hoja mpya!
 
Utakufa watakuja kukuombea usamehewe dhambi zako na uende peponi, Mwanao atarithi hiyo dini naye ataenda kanisani atatoa sadaka mwishoni naye atakufa lakini wamiliki wa Kanisa wapo Ulaya na documets zote za makanisa... Na viongozi huko ni Wazungu...
Umeongea ukweli mtupu..tunatengeneza empire za wazungu..bora tuanzishe makanisa ya hapahapa afrika..tutajirishane sisi kwa sisi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kwani na haya makanisa ya uzinifu ya kinabii hakuna sadaka?
Je, HQ iko Ulaya?
Hayo makanisa kila JPL wanahakikisha wanawaparaza waumini jtatu waanze upya
 
Umeongea ukweli mtupu..tunatengeneza empire za wazungu..bora tuanzishe makanisa ya hapahapa afrika..tutajirishane sisi kwa sisi.

#MaendeleoHayanaChama
Unasubir nin na akati tayari Mwamposa, Mwingira, Lusekelo, Gwajima, Kakobe, Masanja na baadae Joti yoote haya ni makanisa ya kibantu wy dont u join?
 
Tokea wazungu wajitoe kufadhiri baadhi ya haya makanisa imekua ni kukabana kweli kweli....wengine hadi tumeingiwa uvivu wa kusali maana ukifikiria ni lazi.a ujipange kweli mfukoni angala 20 iwemo kwenye pocket...na hii ndio imefanya wengi siku hizi kuhama makanisa na kutimkia kwa akina mitume na manabii
 
Mimi mngeweza kunielezea fungu la 10 linafikaje kwa Mungu ningeshukuru sana
 
Back
Top Bottom