Michango ni mizuri kwenye makundi yetu ila hii tabia ya kuweka mkeka kwa kila jambo sijui kama ni sahihi

Michango ni mizuri kwenye makundi yetu ila hii tabia ya kuweka mkeka kwa kila jambo sijui kama ni sahihi

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
25,030
Reaction score
61,298
Jamani huu ni mtazamo wangu tu. Mimi napenda sana magroup ya classmates sana sana na ya kazini pia nayapenda uzuri ya kazini hawana tabia kama ya classmate wako sawa tu..haya ma-group yanatupa nafasi ya kuwasiliana, kubadilishana mawazo sometimes kunyapia nyapia baadhi ya mademu ma crash uliokuwa unawakubali enzi hizo huwezi jua huenda ipo siku mkakutana hata dodoma marathon ukajilia mzigo pumbav zao hahahahah

Lakini kuna jambo moja linanipa maswali
Mtu akiugua tu kalazwa kafanyiwa upasuaji sometimes mdogo... mkeka.
Mtu akifiwa na baba... mkeka.

Siyo kwamba kusaidiana ni vibaya. Hapana, kusaidiana ni jambo jema sana tena sana Lakini je ni lazima kila tukio liwe na mkeka na list ya waliotoa?

Inakata stimu sana ndo maana unakuta members wengine unakuta hata hawana vibe tena la ku chart maana washaona kama hakuna maana nyingine ya group zaidi ya michango pekee.

Kama member ameguswa na hali ya mwenzake si anaweza kumtumia msaada wake moja kwa moja? Hata ya matunda, au chochote anachomudu. Msaada unabaki kuwa msaada hata bila kutangazwa kwenye group. Na hata hivyo mtu kama kaumwa nini anahitaji kwa group zaidi ya yaq matunda tu maana sidhani hata kama michango inaweza tosha kwa matibabu..

Kwa maoni yangu lakini naona mikeka iwe zaidi kwenye shughuli zinazohitaji maandalizi ya pamoja kama harusi ambayo target ni kwamba changia pia upewe kadi kama mgeni mwalikwa...Lakini kwenye kuugua au dharura za mtu binafsi, tusiweke mazingira yanayofanya watu wajisikie kama kuchangia ni lazima.

Huu ni mtazamo wangu tu. Au nyie mnaonaje? Je, mikeka ya kila tukio inajenga umoja au taratibu inaanza kuondoa ule uhuru wa kusaidiana kwa hiari?
 
upo sahh.. ila kwa kawaida mnapotaka unda kundi n muhm mkaweka taratibu za group zitakazowaongoza kufkia malengo ya grp huska. hvo kama awali mliweka utaratbu wa kuchangiana apo hakuna namna..
 
Mkeka ni wa msiba tu ndio ninaweza kuchanga . Mkeka wa sherehe ya harusi sioni ulazima wake. Suala la kuumwa pia ni binafsi kila mmoja awajibike na familia yake kama ni kuchanga basi huyo anaeumwa awe ameomba kusaidiwa baada ya kuelemewa na gharama
 
Uko sahihi mkuu kwa asilimia mia
 
Yaani michango ya rambirambi nayo watu wanaita Mikeka?. Nikiona hilo jina tu siwezi kuchangia.
 
Mkeka ni muhimu....mfano mchango wa msiba, ni muhimu watu kujua ni kina nani wanashiriki/wanachangia kwenye matukio ya kijamii ? Na je ni kina nani hawachangii ?

Hii itasaidia kuweka kumbukumbu sawa, mtu akipatwa na tatzo na hachangii wenzake watu wanakula buyBinu ! Binafsi ndo nilivyo, kama naona huna taimu na watu kwenye mambo ya msingi ukipatwa na shida hata sijigusi !

Nb... mambo ya harusi, send-off, birthday, sijui kitchen party mambo ya kumtoa mtoto sijui 40 na upuuzi wa hio sitoi hela yangu... starehe zako zisisumbue watu wengine!

Msiba na ugonjwa ndo mambo nazingatia tu
 
Mkeka ni wa msiba tu ndio ninaweza kuchanga . Mkeka wa sherehe ya harusi sioni ulazima wake. Suala la kuumwa pia ni binafsi kila mmoja awajibike na familia yake kama ni kuchanga basi huyo anaeumwa awe ameomba kusaidiwa baada ya kuelemewa na gharama

Mm pia... msiba na ugonjwa ndo nachanga tu.... mengine sitoi hela yangu yangu ! Harusi sijui send-off na upuuzi wa hivo sitoi pesa yangu...na wewe usinichangie ...simple ! Ndugu kibao jamaa na marafiki nimewakaushia kisa mamichango yasiyo na maana ! Alafu mfano harusi kuna ujinga chini ya laki unaweza usipewe kadi
 
Wengine wanakwambia chini ya laki hupati card.
Mkeka mwezi huu
Wagonjwa wa 4+
Kuolewa
Kitchen party
Usiku wa vyombo
Harusi
Kuvunja kamati
Fagia nyumba.
Hapo bado una mzazi ,familia hawapo kwenye mikeka.
Unashika kichwa unasema "inhii" in MAGU voice
 
Back
Top Bottom