Michango ya JF inawasaidia Wabunge wanaosoma majadiliano haya

Patriot

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2008
Posts
5,759
Reaction score
4,872
Tukumbuke wabunge wengi elimu ni ndogo kuliko wenye elimu kubwa. Bahati mbaya hawana tabia ya kutafuta washauri kabla ya kujipanga kutoa michango. Lakini nimekuwa na hisia kwamba wapo wanaotafuta michango mizuri kutoka hapa JF.

Kwa wiki nzima nimeangalia baadhi michango ya wabunge. Ninachokiona, sehemu kubwa ya michango inapata ubora kwa michango ya JF. Hii inanifanya niwe na wazo kwa wana JF wanaoona hapa ni sehemu ya mizaha. Wengine wanaifanya hii kuwa ni shemu ya zomea zomea na lugha za kijiweni; mataga, Lumumba, Ufipa, nk.

Kwa miaka ambayo nimekuwa hapa JF nimeona wanachama wapya wakijiunga wakiwa na mijadala chini ya kiwango na baada ya muda, michango yao hubadilika na kuwa ni ya kiwango. Lakini pia wapo wale ambao wamekomaa na kuamini wanajua, wakafunga milango ya kujifunza. Hao hadi leo ni watu wa michango ya chini sana. Naamini tukiitumia vizuri JF udhaifu wa kujenga hoja tunaotoka nao vyuoni, utaondoka. Baadhi mutatusaidia mbele ya safari za kisiasa.
 
Shida ni kuwa kiwango cha kuvunjika moyo ni kikubwa hata wengine wanaona haina maana,taaluma haiheshimiwi tena,mwenye weledi katika utendaji ni adui,sheria,taratibu hats sheria mama zilipuuzwa,unataraji kupata bado mawazo chanya.

Bora wakati huu tunauona mwanzo mpya wenye matumaini ,japo bado ipo kazi kubwa yakufanya ilituende sawa kama taifa.
 
Tukumbuke wabunge wengi elimu ni ndogo kuliko wenye elimu kubwa. Bahati mbaya hawana tabia ya kutafuta washauri kabla ya kujipanga kutoa michango. Lakini nimekuwa na hisia kwamba wapo wanaotafuta michango mizuri kutoka hapa JF.

Kwa wiki nzima nimeangalia baadhi michango ya wabunge. Ninachokiona, sehemu kubwa ya michango inapata ubora kwa michango ya JF. Hii inanifanya niwe na wazo kwa wana JF wanaoona hapa ni sehemu ya mizaha. Wengine wanaifanya hii kuwa ni shemu ya zomea zomea na lugha za kijiweni; mataga, Lumumba, Ufipa, nk.

Kwa miaka ambayo nimekuwa hapa JF nimeona wanachama wapya wakijiunga wakiwa na mijadala chini ya kiwango na baada ya muda, michango yao hubadilika na kuwa ni ya kiwango. Lakini pia wapo wale ambao wamekomaa na kuamini wanajua, wakafunga milango ya kujifunza. Hao hadi leo ni watu wa michango ya chini sana. Naamini tukiitumia vizuri JF udhaifu wa kujenga hoja tunaotoka nao vyuoni, utaondoka. Baadhi mutatusaidia mbele ya safari za kisiasa.

Naona rais kawastukia wabunge kushinda mitandaoni wakitafuta la kusema. Ubaya ni kutokuwa na mawazo yao, lakini pia kosa ni kupeleka wabunge wenye ubora wa chini.
Mambo kama haya ndo ya kujadili hapa JF na kutafuta njia ya kuboresha michango yetu badala ya kuzomeana na kusifia watu hovyo kwa kuwa tu wako chama fulani.
 
Madhara ya uwakilishi wa kupita bila kupingwa.
 
Back
Top Bottom