Tukumbuke wabunge wengi elimu ni ndogo kuliko wenye elimu kubwa. Bahati mbaya hawana tabia ya kutafuta washauri kabla ya kujipanga kutoa michango. Lakini nimekuwa na hisia kwamba wapo wanaotafuta michango mizuri kutoka hapa JF.
Kwa wiki nzima nimeangalia baadhi michango ya wabunge. Ninachokiona, sehemu kubwa ya michango inapata ubora kwa michango ya JF. Hii inanifanya niwe na wazo kwa wana JF wanaoona hapa ni sehemu ya mizaha. Wengine wanaifanya hii kuwa ni shemu ya zomea zomea na lugha za kijiweni; mataga, Lumumba, Ufipa, nk.
Kwa miaka ambayo nimekuwa hapa JF nimeona wanachama wapya wakijiunga wakiwa na mijadala chini ya kiwango na baada ya muda, michango yao hubadilika na kuwa ni ya kiwango. Lakini pia wapo wale ambao wamekomaa na kuamini wanajua, wakafunga milango ya kujifunza. Hao hadi leo ni watu wa michango ya chini sana. Naamini tukiitumia vizuri JF udhaifu wa kujenga hoja tunaotoka nao vyuoni, utaondoka. Baadhi mutatusaidia mbele ya safari za kisiasa.