Michango ya Rambirambi ya Kanumba Yatafunwa

Michango ya Rambirambi ya Kanumba Yatafunwa

Kimbunga

Platinum Member
Joined
Oct 4, 2007
Posts
14,951
Reaction score
9,977
Wanabodi kuna tetesi kuwa michango ya rambirambi kwa ajili ya msiba wa Marehemu Kanumba imetafunwa na kamati ya mazishi.

Kuna habari kwamba zilichangwa pesa kiasi cha shilingi million 51. Kamati inasema imetumia shillingi millioni 48 kwenye mazishi hivyo iliyobaki ni millioni 3 tu! Mama Kanumba anauliza makaratasi ya kuelezea hayo matumizi yako wapi wajumbe wa kamati ya mazishi bado wanajiuma uma!

Pia inaaminika kuna pesa zilikuwa zinatumwa kwenye M pesa na Tigo Pesa ya mtu mmoja maarufu nazo hazijaonekana alipoulizwa akasema amepata laki 3 tu kwa kuwa wengi walikuwa wanatuma shilingi mia tano toka mikoani!

Tusubiri tu punde kitanuka. Bongo kila kitu ni deal!
 
Aiseee hao watu wa kamati wanafanya mambo ya aibu kweli,ni aibu sanaaa,mwakifamba na jb vp?
 
Aiseee hao watu wa kamati wanafanya mambo ya aibu kweli,ni aibu sanaaa,mwakifamba na jb vp?

Mkuu kuna tifutifu huko nadhani mtalisikia tu. Mama anadai kuna wadogo zake marehemu lakini hawakushirikishwa kwenye mipango ya matumizi ya pesa za michango. Huenda hata ile.millioni kumi ya JK nayo imemiss in action
 
Nilihisi haya yatatokea. Hakukuwa na udhibiti wa makusanyo na matumizi ya michango. Kweli "dunia sasa imani imekwisha", kama alivyoimba Hayati Marijani Rajabu. Watu wanakula hata michango ya msiba! Eeh Mola tunusuru.
 
Duh zile suti hazikuwa bure
 
Wanabodi kuna tetesi kuwa michango ya rambirambi kwa ajili ya msiba wa Marehemu Kanumba imetafunwa na kamati ya mazishi. Kuna habari kwamba zilichangwa pesa kiasi cha shilingi million 51. Kamati inasema imetumia shillingi millioni 48 kwenye mazishi hivyo iliyobaki ni millioni 3 tu! Mama Kanumba anauliza makaratasi ya kuelezea hayo matumizi yako wapi wajumbe wa kamati ya mazishi bado wanajiuma uma! Pia inaaminika kuna pesa zilikuwa zinatumwa kwenye M pesa na Tigo Pesa ya mtu mmoja maarufu nazo hazijaonekana alipoulizwa akasema amepata laki 3 tu kwa kuwa wengi walikuwa wanatuma shilingi mia tano toka mikoani!

Tusubiri tu punde kitanuka. Bongo kila kitu ni deal!

Ubinadam kaaaaaaziii kwel!
 
Ishu kama hizo hazikwepeki katika maisha ya kibongo ,
Star kaondoka iweje wenyewe wasinufaike na michango.
TATIZO NJAA PAMOJA NA USIMAMIZI MBOVU KATIKA TARATIBU ZOTE ZA MAZISHI:
 
Wanabodi kuna tetesi kuwa michango ya rambirambi kwa ajili ya msiba wa Marehemu Kanumba imetafunwa na kamati ya mazishi. Kuna habari kwamba zilichangwa pesa kiasi cha shilingi million 51. Kamati inasema imetumia shillingi millioni 48 kwenye mazishi hivyo iliyobaki ni millioni 3 tu! Mama Kanumba anauliza makaratasi ya kuelezea hayo matumizi yako wapi wajumbe wa kamati ya mazishi bado wanajiuma uma! Pia inaaminika kuna pesa zilikuwa zinatumwa kwenye M pesa na Tigo Pesa ya mtu mmoja maarufu nazo hazijaonekana alipoulizwa akasema amepata laki 3 tu kwa kuwa wengi walikuwa wanatuma shilingi mia tano toka mikoani!

Tusubiri tu punde kitanuka. Bongo kila kitu ni deal!
Nilikuwa nategemea sana hayo mambo kwa usharobaro wa kamati ile ,i expected the same issue to rise
 
Duh what a shame,naona hata mdogo wake kanumba hakushirikishwa kwenye mipango yote,yani walichukulia msiba wa kanumba kama ni wa kwao peke yao.wanadhambi sana,shame shame
 
ulizani clouds wanafanya kazi ya kukufanyia matangazo bure
 
Issue kama hii imekuwa inatokeaga mara nyingi baada ya kuzika.Saa nyingine unakuta wala hakuna aliyekula kitu bali ni uzembe kutokuweka mahesabu sawa ambao inawezekana kuchangiwa na majonzi.Kuna kamati nyingine ni wanafamilia wenyewe lakini bado kumekuwa na migogoro mikubwa.
 
Kwa kuwa msiba ni wa msanii, basi kamati ilikuwa ya wasanii, ukusanyaji michango wa kisanii, matumizi ya kisanii, taarifa (ya matumizi) ni ya kisanii. Na sasa watafanya usanii mwingine ili kuipoza familia. Nchi hii ufisadi kila kona. Aibu!
 
Hakuna mtanzania asiyekua fisadi nasema tena ni fursa ndo tunayokosa.Pole mama kanumba
 
JB and Co, hawa jamaa wajanja wajanja sana watakuwa wameishamtimba mama Kanumba.
 
Back
Top Bottom