Michango ya wafanyakazi NSSF,PSPF na PPF ni Unyonyaji..

Prince Tumbo

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2013
Posts
910
Reaction score
247
Ndg wanabodi, wafanyakazi [wa umma na taasisi binafsi] wamekuwa wakikatwa fedha kutoka kwenye mishahara yao kila mwezi na mwajiri nae kumwekea mfanyakazi kiasi cha fedha kwenye fedha hiyo kama "social security" baada ya kuacha kazi au kustaafu. Hoja yangu hapa ni pale ambapo fedha hiyo hata kama ikikaa huko miaka 35 huwa haiongezeki [haizai riba au ongzeko la thamani ya fedha] wakati fedha hiyo inatumiwa kwenye miradi ya kibiashara na hukopwa na serikali kwa ajiri ya miradi mikubwa [tunaifaham]. Fedha yoyote huongezeka thamani mwaka hadi mwaka [japo hushuka pia] fedha ya mwanachama hubaki kiasi hichohicho licha ya kukaa muda mrefu na bado hufanyiwa biashara kikamilifu. Naomba wataalam wa uchumi watusaidie, je,huu sio unyonyaji, sheria hii ya hifadhi ya jamii imekaa vizuri hapo? Wadau wa michango hii mbona hatushirikishwi kwenye miradi hii, gawiwo la faida kwa mwanachama analipataje [halipo]? Mbona michango yetu haiongezeki kadri thamani ya fedha linapoongezeka? Kama serikali inajikopesha fedha hii ni kwa sababu gani mwanachama asikopeshwe na taasisi hizi zikageuzwa kuwa taasisi za mikopo kwa wanachama kama serikali hujikopesha fedha ya walala hoi?...hebu tuchangie juu ya hizi changamoto, naomba kuwasilisha
 
Nikweli mdau mimi ni miongoni mwa wadau wa uchum hapa nchin japo sijigambii...na nazitumia hizo istitution ila ukweli nikwamba wanajijali zaidi na sio kujali wanachama......kainterest wanatoa ila ukilinganisha na law ya creadit creation...ni kwamba hawana tofauti na monopolist in market structure.......wakati sisi ndo tulitakiwa tue shareholder......mbaaaaya sana
 

very right mkuu, wanachama hukopa benki na kwineko wakati wana taasisi yao ambayo inaweza kuwapa mikopo, badala yake taasisi inamonoplise na inakopesha wengine kuliko wanachama, mbaya zaidi viongozi wetu wanataka kuweka zuio la kujitoa. Hapo kuna tatizo kubwa na wanachama lazima tupige kelele hata kupitia kwa wabunge wetu
 
Na hapohapo walivigawagawa vyama vya wafanyakazi ili kukosa sauti ya pamoja,bila wafanyakazi kuungana pamoja wataendelea kunyonywa maisha yao yote.
 
mi wananiboa sana, eti wanasubiri tufe ndo wasomeshe watoto wetu. loh!

Badala waweke utaratibu tuwe tunakopa pesa zetu badala kuendelea kulizwa na mabenki wakati wamekalia pesa zetu kibao
 
mi wananiboa sana, eti wanasubiri tufe ndo wasomeshe watoto wetu. loh!

Badala waweke utaratibu tuwe tunakopa pesa zetu badala kuendelea kulizwa na mabenki wakati wamekalia pesa zetu kibao

Mifuko hii naona ni neema kwa viongozi, fedha hizi zinajengewa vyuo, maghorofa mareeeeefu, then tunambiwa mpaka tuzeeke ndipo tupewe...CHADEMA HII TUNAWAPA HOJA TENA YA KUSHINDIA KWENYE UCHAGUZI MKUU...tumechoka na wizi...
 
Mifuko hii naona ni neema kwa viongozi, fedha hizi zinajengewa vyuo, maghorofa mareeeeefu, then tunambiwa mpaka tuzeeke ndipo tupewe...CHADEMA HII TUNAWAPA HOJA TENA YA KUSHINDIA KWENYE UCHAGUZI MKUU...tumechoka na wizi...

mkuu hiyo nyekundu ilipigwa ajua
 
Tapeli akitaka kukuibia, atakiletea kipande cha chupa olive achukue almasi yako. Hii mifuko ni ya kitaleli, Kama inasubiri mwanachama afe ndiyo ianze kuonyesha moyo wa huruma wa kununua jeneza na kusomesha watoto huu si utapeli! Inatakiwa imsaidie kwanza mwanachama akiwa hai kwa kumpa makazi mazuri na uhakika wa maisha baada ya kustaafu. Kinacho fanywa sasa hivi ni Utapeli na wizi mtupu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…