Prince Tumbo
JF-Expert Member
- Apr 5, 2013
- 910
- 247
Ndg wanabodi, wafanyakazi [wa umma na taasisi binafsi] wamekuwa wakikatwa fedha kutoka kwenye mishahara yao kila mwezi na mwajiri nae kumwekea mfanyakazi kiasi cha fedha kwenye fedha hiyo kama "social security" baada ya kuacha kazi au kustaafu. Hoja yangu hapa ni pale ambapo fedha hiyo hata kama ikikaa huko miaka 35 huwa haiongezeki [haizai riba au ongzeko la thamani ya fedha] wakati fedha hiyo inatumiwa kwenye miradi ya kibiashara na hukopwa na serikali kwa ajiri ya miradi mikubwa [tunaifaham]. Fedha yoyote huongezeka thamani mwaka hadi mwaka [japo hushuka pia] fedha ya mwanachama hubaki kiasi hichohicho licha ya kukaa muda mrefu na bado hufanyiwa biashara kikamilifu. Naomba wataalam wa uchumi watusaidie, je,huu sio unyonyaji, sheria hii ya hifadhi ya jamii imekaa vizuri hapo? Wadau wa michango hii mbona hatushirikishwi kwenye miradi hii, gawiwo la faida kwa mwanachama analipataje [halipo]? Mbona michango yetu haiongezeki kadri thamani ya fedha linapoongezeka? Kama serikali inajikopesha fedha hii ni kwa sababu gani mwanachama asikopeshwe na taasisi hizi zikageuzwa kuwa taasisi za mikopo kwa wanachama kama serikali hujikopesha fedha ya walala hoi?...hebu tuchangie juu ya hizi changamoto, naomba kuwasilisha