Kuna muda natamani, tuishi kama zamani../
ila sijui mkuda gani, alievuruga amani/
Amani ya ndoa haipatikani, kila kitu ananikosoa hata uwe utani/
Sioni tena raha ya kukaa nyumbani, yaani bora uishi vitani kuliko ndoa isio na amani../
Upendo umefika mwisho, wapendanao wanajinyonga/
Wengine ni vitisho, kama mikwara ya Mandonga/
Hakuna upatanisho, kila mmoja anachonga/
Kifo ndio hitimisho, hata kama alikukonga/
Unaempenda hakupendi kama uteja wa unga/
Usiye mpenda haendi kama kamba umemfunga/
Dharau haijengi siyo tofari la nyumba/
Mapenzi yana mengi bwana mdogo chunga/
Mnunulie simu wenzako wampe vocha/
Jifanye mwalimu ajifanye kocha/
Mpe za kujikimu akakufanye ndondocha/
Yanakata stimu mapenzi ulofa/
Hiyo bastola unayonunua, haitaua kabisa vibaka/
Bali mwenyewe utajiua, utakapokuta mkeo wamempakata/
Wachache wana mapenzi ila tenzi kuwapata/ hauwezi bila Mwenyezi utadata/ kindezi kisa penzi atakukamata/
Kwa mwenye Benz atakuacha/ hauna malezi linavuja pakacha/ hata uwe mbezi na pesa ya kutakata/ bado utafanyiwa ushenzi kwa muuza kashata/
Ule muda unasaka mahitaji, ili Family njaa isijelala/
Wife yupo kifuani kwa mshikaji, huku akikuita fala/
Mapenzi hayana Falsafa, hata uwe umesoma sana/
Mapenzi yanaleta maafa, sio Tarime mpaka Tanga wanauwana/